Mdada amwaga chozi, imeniumiza moyo sana

Mdada amwaga chozi, imeniumiza moyo sana

Jana nilitumwa na bosi wangu kwenda kuchukuwa document katika kampuni moja hivi. Nilipofika sikumkuta secretary, niliambiwa ameenda lunch. Nikamkuta kijana mmoja ambaye ni bosi wake na ndiye aliyekuwa anawasiliana na bosi wangu.

Yule kijana akampigia simu afahamu document zilipo. Yule dada akamwambia amezifungia kwenye kabati yake na ufungua anao yeye. Inaonyesha sehemu aliyoenda kupata lunch pana umbali kidogo.

Aliporudi yule kijana alimfokea sana, yule kaka akamaliza hasira zake kwa kumwambia kwa tabia zako ndio maana wanaume wa kukuoa wanakukimbia.Yule dada alianza kulia mpaka na mimi nusu nilie. Nikimwangalia hivi, umri wake waweza kuwa kati ya miaka 34-36.

Tuchunge ulimi ndugu zangu, maneno yanauma.
Sijaelewa hivi hapa tulitakiwa kusimpathy na mwenye topic au ni vipi?? kama sijaelewa hv
 
Sidhani kama huyo kaka amewahi kumtaka huyo binti kama ingekuwa hivyo binti asingelia kwa sababu angejustfy kwamba umesema hivyo kwa sababu nilikukataa ila huyo binti kutokana na frustration za umri labda amekuwa akijiachia sana kwa wanaume ili apate wa kumuoa na matokeo yake anapata maplay boy mpaka amedharaulika.sikia kila mwanaume anahitaji mtu ambaye ni standard na siyo jamvi la wageni kwa hiyo arekebishe tabia.kilio chake hakikutokana na kauli tu ya huyo bro ila ilitokana na ukweli wa maisha halisi anayopitia remember what can not kill u make u stronger so its a time for the girl to be strong n make the right decision.
 
pangechimbika wangu na mimi ningempa lake alaaa kwa maana ni boss ndo atumie cheo chake vibaya no way....

basi fanya haraka usije chelewa waanze kukusema vbaya mabosi.
 
Jana nilitumwa na bosi wangu kwenda kuchukuwa document katika kampuni moja hivi. Nilipofika sikumkuta secretary, niliambiwa ameenda lunch. Nikamkuta kijana mmoja ambaye ni bosi wake na ndiye aliyekuwa anawasiliana na bosi wangu.

Yule kijana akampigia simu afahamu document zilipo. Yule dada akamwambia amezifungia kwenye kabati yake na ufungua anao yeye. Inaonyesha sehemu aliyoenda kupata lunch pana umbali kidogo.

Aliporudi yule kijana alimfokea sana, yule kaka akamaliza hasira zake kwa kumwambia kwa tabia zako ndio maana wanaume wa kukuoa wanakukimbia.Yule dada alianza kulia mpaka na mimi nusu nilie. Nikimwangalia hivi, umri wake waweza kuwa kati ya miaka 34-36.

Tuchunge ulimi ndugu zangu, maneno yanauma.

Kwa kampuni ninyofanyia kazi hilo tu linatosha kumfukuzisha kazi huyo aliyesema maneno hayo. Kwa sababu hizi kampuni za kimataifa hazipendi mambo ya kipuuzi kama hayo. Ni bora mtu hata kama umeudhika usitoke nje ya mada, yaani kama suala ni funguo basi ziongelewe funguo na umuhimu wa docoments. Ss suala la personal kazini linakujaje jamani? Je, customer care hapo limezingatiwa? Hizo tunasema ni kampuni za vichochoroni tu haziwezi kuwa kampuni hizo.
 
dada amshukuru Mungu kwa kila jambo,siku hiyo MUNGU aliiweka ili amshukuru kwa hilo,kulia sio lazima sana,cha msingi ni kumshukuru BWANA WA SABATO.
 
Emotional abuse, ikikutana na weak personality, majanga.
Ningekuwa mie, ningempa jibu hilo hadi angeshangaa na roho yake.

Dada kila mtu ana weak points zake dada, Na hili la kuachwa mama halina mjanja. Hata uweje lazima utaumia tu.
 
Hela bila kuelimika ni tatizo.Kilichomuuma huyo dada zaidi ni kwamba boss ana mtusi mbele ya mgeni.Shule husaidia kumfanya mtu awe mstaarabu,hao ndio wale shule ya msingi waliobahatika kupata hela
 
Kawaida ya ukweli. Uliza CCM serikali 3 uone!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom