Msandawe Halisi
JF-Expert Member
- Nov 5, 2010
- 647
- 351
Jana nilitumwa na bosi wangu kwenda kuchukuwa document katika kampuni moja hivi. Nilipofika sikumkuta secretary, niliambiwa ameenda lunch. Nikamkuta kijana mmoja ambaye ni bosi wake na ndiye aliyekuwa anawasiliana na bosi wangu.
Yule kijana akampigia simu afahamu document zilipo. Yule dada akamwambia amezifungia kwenye kabati yake na ufungua anao yeye. Inaonyesha sehemu aliyoenda kupata lunch pana umbali kidogo.
Aliporudi yule kijana alimfokea sana, yule kaka akamaliza hasira zake kwa kumwambia kwa tabia zako ndio maana wanaume wa kukuoa wanakukimbia.Yule dada alianza kulia mpaka na mimi nusu nilie. Nikimwangalia hivi, umri wake waweza kuwa kati ya miaka 34-36.
Tuchunge ulimi ndugu zangu, maneno yanauma.