Gorgeousmimi
JF-Expert Member
- Jun 21, 2010
- 9,296
- 7,669
Mahitaji
Jinsi ya kutayarisha
- Kuku wa kienyeji 1
- Nyanya mbili zilizomenywa na kukatwakatwa
- Kitunguu maji kikubwa kimoja kilichomenywa na kukatwa
- Nyanya ya kibati vijiko viwili vya supu
- Kitunguu swaumu kijiko kimoja cha supu
- Chumvi kiasi
- Pilipili manga kijiko kimoja cha chai
- Juisi ya limau/ndimu kiasii
- Uzile ulosagwa
Jinsi ya kutayarisha
- Mtayarishe kuku na umkate vipande kama kawaida,mtie kitunguu swaumu,pilipili manga,chumvi na uzile ulosagwa kijiko kimoja. Muinjike jikoni na Mfunike viungo vikolee muache atokote mpaka maji ya kauke,muongezee maji kiasi cha kumfunika kuku,mfunike na muache achemke.
- Akikaribia kuvia half way through mtie kitunguu maji na nyanya pamoja na nyanya ya kibati,ongezea uzile kijiko kimoja kingine cha chai na muache aendelee kuiva taratibu.Unaweza kuingezea maji ukipenda ili uwe na mchuzi mwingi.
- Mkamulie limau na adjust chumvi.
- Mchuzi huu mtam sana ukiula na wali wa nazi.