Mchuzi wa nyanya ya kibati

Gorgeousmimi

JF-Expert Member
Jun 21, 2010
9,296
7,666
Mahitaji

  • Kuku wa kienyeji 1
  • Nyanya mbili zilizomenywa na kukatwakatwa
  • Kitunguu maji kikubwa kimoja kilichomenywa na kukatwa
  • Nyanya ya kibati vijiko viwili vya supu
  • Kitunguu swaumu kijiko kimoja cha supu
  • Chumvi kiasi
  • Pilipili manga kijiko kimoja cha chai
  • Juisi ya limau/ndimu kiasii
  • Uzile ulosagwa

Jinsi ya kutayarisha


  1. Mtayarishe kuku na umkate vipande kama kawaida,mtie kitunguu swaumu,pilipili manga,chumvi na uzile ulosagwa kijiko kimoja. Muinjike jikoni na Mfunike viungo vikolee muache atokote mpaka maji ya kauke,muongezee maji kiasi cha kumfunika kuku,mfunike na muache achemke.
  2. Akikaribia kuvia half way through mtie kitunguu maji na nyanya pamoja na nyanya ya kibati,ongezea uzile kijiko kimoja kingine cha chai na muache aendelee kuiva taratibu.Unaweza kuingezea maji ukipenda ili uwe na mchuzi mwingi.
  3. Mkamulie limau na adjust chumvi.
  4. Mchuzi huu mtam sana ukiula na wali wa nazi.
Cc farkhina, Mrs Kharusy, FirstLady, Angel Nylon, Revocatus Kashaga HP1, Honey Faith, xiexie, rasai, ICHANA, tama, Mwananchi, ladyfurahia
20140608_163637.jpg
20140608_163644.jpg
 
Shoga kuku huyu wa kienyeji nlionae mie anawivaa masaa 2 naimba nyimbo zote jikoni ndio awive lol

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
huyo ndo anafaa haswa wallahi we muwekee moto mdogo tu aive taratibu....mchuzi huu mtamu,haukinaishi maana hauna mafuta waweza ule mpaka basii....
 
pishi tamu sana hili gorgeousmimi naomba pia utuwekee recipe za kukaanga maini ili yawe matamu na kuku wa kukaanga, nitashukuru
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom