Mchungaji: Wazito wanahusika dawa za kulevya

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797

Na Marietha Mkoka

BAADHI ya viongozi wakuu serikalini, wanadaiwa kuwa vinara wa biashara ya mihadarati wakiwatumia raia kutoka nje wanaokuja kwa kivuli cha dini.

Tuhuma hizo nzito zilitolewa Dar es Salaam jana na Mchungaji William Mwamalanga aliyedai kuwa viongozi hao huwatumia raia wa nje kuingiza na kusafirisha dawa za kulevya, wakati mwingine wakitumia vyeti bandia vya dini ili kupenyeza au kuvusha dawa hizo.

Mwamalanga alitaja raia hao wanaonunua vyeti ‘bandia’ vya dini kwa sh milioni 1.5, wengi wanatoka Ghana, Nigeria, Kenya, Somalia na DR Congo, ambao hujigawa kwenye madhehebu tofauti, huku akiainisha njia za kusafirishia magendo hayo kuwa ni viwanja vya ndege vya kimataifa vya Julius Nyerere (JNIA),
Kilimanjaro (KIA) na ule wa Zanzibar.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ambayo Tanzania Daima ina nakala yake, mchungaji huyo aliweka wazi njia nyingine zinazosafirisha dawa hizo kuwa ni mipaka ya Tunduma na Zambia, Kyela na Malawi na Bandari ya Dar es Salaam.

“Maeneo hayo kwa sasa yanayojulikana kama sugu kwa kuingiza na kusafirisha nje ya nchi dawa za kulevya, ni Dar es Salaam, Mbeya, Lindi, Tanga, Mwanza na Unguja,” alisema.

Alisema kutokana na biashara hiyo kuingia mikononi mwa baadhi ya vigogo hao, kuna haja ya kuunda kamati ya maadili na haki za jamii, na kuvunjwa kwa tume ya kuratibu dawa za kulevya, badala yake kibaki kikosi cha polisi cha kupambana na dawa hizo chini ya Kamanda Godfrey Nzowa.

“Kesi za vigogo hazisikilizwi, badala yake huachiwa, jambo linalohatarisha ustawi wa taifa, kutokana na udhaifu huo, tunaendelea kushuhudia Watanzania wakifungwa nje ya nchi kutokana na sakata hilo, hii ni aibu,” alisema nchungaji huyo katika taarifa yake.

Naye Sheikh Amir Mohamed, alieleza kwamba, endapo serikali haitachukua tahadhari mapema kuhusu biashara hiyo, ipo hatari kwa taifa kupoteza nguvukazi, hususan vijana ambao kwa asilimia 80 hutumia dawa hizo.

Sheikh Amir alisema dawa zinazokamatwa, hurudi mitaani kwa njia za panya na kuingia kwenye mzunguko, huku akieleza kwamba viongozi safi wa dini wamejipanga kupambana na suala hilo linalosababisha wanafunzi wengi kushindwa kumaliza masomo yao, huku wengine wakifeli.

Hivi karibuni, Kamanda Nzowa alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza kwamba, biashara haramu ya dawa za kulevya imeongezeka hususan katika robo ya kwanza ya mwaka huu iliyoishia Machi.

Yeah nilikuwa nashangaa na dini nyingi zimejaa nchini viongozi wa dini hizo wengi ni Watu Wa Nje kama Nigeria n.k Na baadhi niliona wanakwenda Ikulu kutoa rambirambi za kuzama kwa Meli ile ya Zanzibar na BriefCase imejaa pesa, nikashangaa hawana Bank Account na kumpa Rais Check kuliko Mlundo wa Pesa?

Hii inatutia Aibu, Hizi dini bila kuangaliwa ndizo zitakazotuharibia wananchi wetu.

Na, kama ni kweli hapo ndio unajua uwalakini wa Azimio la Zanzibar
 
dah baba mchungaji wataje tu hao watu kama unawajua hata kama wataachiwa lakini tutakuwa tumewajua...
 
Wachungaji walioshikwa wanajulikana tena walikuwa na kanisa lao kabisa hapa, au mmesahau? anajaribu kujitetea. Na wale walioshikwa na vipande vya albino?
 
Huyo mchungaji anauma maneno kwa kusema 'viongozi wa juu'. Anatakiwa kusema wazi kuwa IKULU inahusika kwenye biashara ya madawa ya kulevya...
 
Source Tanzania Daima

BAADHI ya viongozi wakuu serikalini, wanadaiwa kuwa vinara wa biashara ya mihadarati wakiwatumia raia kutoka nje wanaokuja kwa kivuli cha dini.

Tuhuma hizo nzito zilitolewa Dar es Salaam jana na Mchungaji William Mwamalanga aliyedai kuwa viongozi hao huwatumia raia wa nje kuingiza na kusafirisha dawa za kulevya, wakati mwingine wakitumia vyeti bandia vya dini ili kupenyeza au kuvusha dawa hizo.

Mwamalanga alitaja raia hao wanaonunua vyeti ‘bandia’ vya dini kwa sh milioni 1.5, wengi wanatoka Ghana, Nigeria, Kenya, Somalia na DR Congo, ambao hujigawa kwenye madhehebu tofauti, huku akiainisha njia za kusafirishia magendo hayo kuwa ni viwanja vya ndege vya kimataifa vya Julius Nyerere (JNIA), Kilimanjaro (KIA) na ule wa Zanzibar.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari ambayo Tanzania Daima ina nakala yake, mchungaji huyo aliweka wazi njia nyingine zinazosafirisha dawa hizo kuwa ni mipaka ya Tunduma na Zambia, Kyela na Malawi na Bandari ya Dar es Salaam.

“Maeneo hayo kwa sasa yanayojulikana kama sugu kwa kuingiza na kusafirisha nje ya nchi dawa za kulevya, ni Dar es Salaam, Mbeya, Lindi, Tanga, Mwanza na Unguja,” alisema.

Alisema kutokana na biashara hiyo kuingia mikononi mwa baadhi ya vigogo hao, kuna haja ya kuunda kamati ya maadili na haki za jamii, na kuvunjwa kwa tume ya kuratibu dawa za kulevya, badala yake kibaki kikosi cha polisi cha kupambana na dawa hizo chini ya Kamanda Godfrey Nzowa.

“Kesi za vigogo hazisikilizwi, badala yake huachiwa, jambo linalohatarisha ustawi wa taifa, kutokana na udhaifu huo, tunaendelea kushuhudia Watanzania wakifungwa nje ya nchi kutokana na sakata hilo, hii ni aibu,” alisema nchungaji huyo katika taarifa yake.

Naye Sheikh Amir Mohamed, alieleza kwamba, endapo serikali haitachukua tahadhari mapema kuhusu biashara hiyo, ipo hatari kwa taifa kupoteza nguvukazi, hususan vijana ambao kwa asilimia 80 hutumia dawa hizo.

Sheikh Amir alisema dawa zinazokamatwa, hurudi mitaani kwa njia za panya na kuingia kwenye mzunguko, huku akieleza kwamba viongozi safi wa dini wamejipanga kupambana na suala hilo linalosababisha wanafunzi wengi kushindwa kumaliza masomo yao, huku wengine wakifeli.

Hivi karibuni, Kamanda Nzowa alikaririwa na baadhi ya vyombo vya habari akieleza kwamba, biashara haramu ya dawa za kulevya imeongezeka hususan katika robo ya kwanza ya mwaka huu iliyoishia Machi.

My concern
Tufanyeje?
 
Hawa vigogo si ndio walimdanganya rais kuwa wachungaji wanaingiza madawa....kumbe wachungaji maslahi
 
vigogo wa madawa ya kulevya wakikamatwa nchi itayumba.!
 
Back
Top Bottom