Mchungaji Rwakatare amtaja Shetani kujitetea | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchungaji Rwakatare amtaja Shetani kujitetea

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by bibikuku, Jun 16, 2011.

 1. bibikuku

  bibikuku JF-Expert Member

  #1
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 16, 2011
  Messages: 828
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mchungaji Rwakatare atoampya Baraza la Maadili

  Mwananchi - Thursday, 16 June 2011
  Nora Damian

  MBUNGE wa Viti maalum (CCM), Mchungaji Getrude Rwakatare jana alitoa mpya mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma alikofikishwa kujieleza kwa nini hakujaza fomu ya kutangaza mali zake, baada ya kudai kuwa shetani ndiye amepoteza fomu hizo.
  Dk Rwakatare alisema hayo wakati akihojiwa na mwanasheria wa baraza hilo Getrude Cynacus.

  Katika utetezi wake, Dk Rwakatare alitumia maneno kama pepo, shetani na Mungu yalitawala.Mchungaji huyo alijitetea kuwa yeye alijaza fomu hizo na kuziwasilisha katika ofisi za bunge lakini hajui nini kilichotokea hadi fomu hizo zisifike kunakohusika.

  "Mambo mengine ni shetani tu, shetani ana nguvu sana kila mahali yuko,"alisema Mchungaji huyo na kuongeza kuwa: "Kazi yenyewe ya kujaza fomu ni ya dakika 10 tu sio kwamba unafanya mtihani Cambridge hivyo halikuwa zoezi kubwa kwangu hadi mimi nishindwe kujaza,"alisema.

  Alisema yeye hakuwa na wasiwasi kabisa kwamba angeweza kuwa mmoja wa watu ambao hawakujaza fomu hizo kwasababu alizijaza na kuzirejesha Ofisi ya Bunge.

  Dk Rwakatare pia alionyesha nakala ya fomu hiyo anayodai kuijaza na kudai kuwa ana uzoefu wa muda mrefu katika fomu hizo na kwamba kila mwaka amekuwa akizijaza.

  "Tutaamini vipi kama nakala hiyo ni halali pengine ulikuwa nayo nyumbani na jana ukaitoa copy. Je hukusaini kokote wakati uliporudisha fomu hizo?" alihoji mwanasheria wa baraza hilo Getrude Cynacus.

  Akijibu swali hilo Dk Rwakatare alisema wakati wa kuchukua fomu hizo ilikuwa lazima kusaini lakini kurudisha haikuwa lazima.

  Baadhi ya mahojiano baina ya Mchungaji huyo na Mwanasheria huyo wa baraza yalikuwa hivi:

  Mwanasheria: Unasema ulijaza fomu, mbona hazikufika kwetu?

  Rwakatare: Hilo litakuwa ni pepo tu. Mimi nilirejesha na Mungu ni shahidi.

  Mwanasheria: Umeng'ang'ania shetani hivi huyo shetani ni nani?

  Rwakatare: Ni roho chafu ambaye kazi yake ni kuharibu na kufanya mambo yaende vibaya.

  Mwanasheria: Sasa huoni kama anakupeleka pabaya?Baada ya swali hilo, Mchungaji Rwakatare hakujibu kitu alikaa kimya.

  Mwanasheria huyo aliliomba baraza hilo litupilie mbali utetezi wa Mchungaji huyo kwa sababu amekiri kutofanya ufuatiliaji.

  Hata hivyo akizungumza nje ya baraza hilo na waandishi wa habari, Dk Rwakatare alisema tangu uanze mchakato wa fomu hizo, hajasafiri kwenda mahali kokote na kwamba anashangaa kwanini hawakumpigia simu kumuuliza kama alijaza au la.

  "Mimi sijasafiri kwenda kokote na wala nilikuwa sina wasiwasi kabisa kwa sababu nilijaza fomu na kuzirejesha, wangeweza kunipigia simu na ningeweza kuja," alisema.

  Alipoulizwa na waandishi wa habari haoni kama kuna haja ya kuwakemea mashetani, Mchungaji huyo hakujibu kitu aliamua kuingia kwenye gari yake na kuondoka.

  Katika hatua nyingine, Mbunge wa Mpanda Vijijini kupitia CCM, Moshi Kakoso naye alifikishwa kwenye baraza hilo jana na kuitupia lawama ofisi ya bunge kwa madai kuwa alijaza fomu na kuzikabidhi kwa wahudumu wa ofisi hiyo.

  "Sijafurahia kuitwa katika baraza hili ni kitendo ambacho si kizuri. Naomba nipewe nafasi ya kujaza fomu nyingine ili nitekeleze sheria za nchi,"alisema Kakoso.Alisema yeye hana mali za kutisha kiasi cha kumfanya ashindwe kujaza fomu hizo na kulalamikia ofisi ya bunge kuwa haiko makini katika utunzaji wa kumbukumbu.

  Mbunge huyo pia alipoulizwa na Mwenyekiti wa baraza hilo Jaji Damian Lubuva kuhusu kumpa muhudumu wa ofisi ya bunge nyaraka muhimu kama hizo, alijitetea kuwa hilo ni bunge lake la kwanza na kwamba alidhani kuwa alikuwa sahihi kumpa muhudumu huyo.

  "Hata mawasiliano ya barua kuja Mpanda yanachukua muda mrefu sana na kutufanya sisi wengine tuonekane tumekiuka sheria,"alisema Kakoso.

  Baada ya kusikiliza utetezi wa wabunge hao, Jaji Lubuva alisema watatoa uamuzi na mapendekezo yao kwenye mamlaka zinazohusika.

  Baraza hilo litaendelea leo ambapo Mbunge wa Mbinga Magharibi John Komba, diwani kutoka Geita Elias Okomu na Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Sumbawanga Edwin


  Kweli shetani mbaya sana. Kwanini anamfanyia hivi Mchungaji Rwakatare?
   
 2. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #2
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Akihojiwa na Baraza La Maadili ya viongozi wa umma, kwa nin hajawasilisha fom yake juu ya mali zake, Mama. Mch. Rwakatare ameacha watu hoi kwa kusema hajawasilisha fomu yake juu ya mali zake kwa sababu shetani amepoteza fomu yake! Kwa maoni yangu, IWEJE SHETANI APOTEZE FOMU YA MCHUNGAJI? JE HUYU SI ANACHANGANYA SIASA NA DINI?
   
 3. MKWECHE

  MKWECHE JF-Expert Member

  #3
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 299
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Mkubwa Bila Chanzo aka Source Au Ulikuwepooo?
   
 4. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #4
  Jun 16, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Mama Lwakatare alimaanisha kwamba huko maofisini inaweza kuwa misplaced kwakuwa devil yupo kila mahali
   
 5. yutong

  yutong JF-Expert Member

  #5
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 1,604
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Kayataka mwenyewe kilichomtuma aende huko ni nini? sasa anaaibika hivyohivyo tunaona. Mi naweza kumsaidia kutaja mali zake hapa;
  1. anamiliki kanisa kubwa ambapo waumini wake wengi ni matajiri wazito hivyo sadaka yake yalaaaaa.... sio mchezo
  2. anamiliki shule na vyuo kwa jina senti meriis
  3. anamiliki gari ya kifahari aina ya nyundo
  4. mali nyingine nyingi
   
 6. maishapopote

  maishapopote JF Gold Member

  #6
  Jun 16, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 2,000
  Likes Received: 957
  Trophy Points: 280
  dah hii kali...lkn kiukweli huwezi changanya dini na siasa moja itakushinda tuuu
   
 7. Kigogo

  Kigogo JF-Expert Member

  #7
  Jun 16, 2011
  Joined: Dec 14, 2007
  Messages: 20,498
  Likes Received: 1,453
  Trophy Points: 280
  huyu mi hata simuelewagi anaongeaga nini bungeni....
   
 8. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #8
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280
  wahuni wanatumia mwavuli wa dini kuwalaghai watu walio na mateso duniani ambayo yameshidwa kupata majawabu. kama vile wagumba, watu ambao hawana nguvu za kiume etc wanakwenda huko kutegeme super natural powers wapone magonjwa ambayo scientifically they will never heal!!!!
   
 9. Safety last

  Safety last JF-Expert Member

  #9
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 4,224
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Kama kuna wanawake wanamcha Mungu wasanii mwekeni Lwakatare ni msanii balaa
   
 10. figganigga

  figganigga JF-Expert Member

  #10
  Jun 16, 2011
  Joined: Oct 17, 2010
  Messages: 14,971
  Likes Received: 6,601
  Trophy Points: 280
  kwani huyu mama unafikiri hawazi kusema hivyo?huyu ndo aliye waaminisha waumin wake eti jk kachaguliwa na Mungu.
   
 11. Bundewe

  Bundewe JF-Expert Member

  #11
  Jun 16, 2011
  Joined: Jun 14, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Kweli shetani noma!!! Yaani wabunge wooooote, kaamua kumuangusha Mchungaji .....na kaweza, du!
   
 12. delabuta

  delabuta Senior Member

  #12
  Jun 16, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 179
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hana lolote huyu mama ni tapeli wa kimataifa kupitia kwa yesu, muogopeni sana .
   
 13. W

  WildCard JF-Expert Member

  #13
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,477
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  Namshangaa EL anakwenda kuwatafuta akina TB Joshua kule Nigeria wakati watu wa aina hiyo tunao wengi tu hadi Bungeni.
   
 14. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #14
  Jun 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Sekretarieti ya maadili ya viongozi imekataaa kupokea fomu za mchungaji Dkt.G.Rwakatare za kujaza mali zake kwa maelezo kuwa mchungaji huyo akuzirejesha fomu hizo wakati muafaka na kwamba analidanganya Braza la maadili.Mchungaji Rwakatare alifikishwa kwenye baraza hilo janana kuhojiwa ni kwa nini hakujaza fomu hizo na kuzirejesha katika tume ya maadili,alisema labda fomu hizo zilianguka mikononi mwa shetani kwa mujibu wa mchungaji huyo ambaye ni mbunge viti maalumu(ccm).
   
 15. Pota

  Pota JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2011
  Joined: Apr 8, 2011
  Messages: 1,813
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  "if you can get a free milk, why keep a cow?" nakipenda sana kibwagizo chake hiki.
   
 16. S

  SURA SIO SOHO Member

  #16
  Jun 16, 2011
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 43
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Inawezwkana bana,coz hata shetani ana power yake,
   
 17. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  It was all over all news yesterday
   
 18. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2011
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,200
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  imebidi nicheke tu maana nimekumbuka wakati niko form tw0 seminarini miaka hiyo ku....ilitokena nikaumia mguu wakati wa mechi then jumatatu nikaavaa viatu na kuingia darasani ..sasa wakati nikiwa darasan mguu ukauma sana na nikaamua kurudi chumbani kuvua viatu ili nivae open shoes...sikuomba ruhusa kuingia room...na ndipo baba ngombera (rector)akanikamata na liponiuliza nilijibu sikuomba ruhusa ya kuingia room..aliponibana sana nikasema nilipitiwa na shetani.....nakumbuka alinipa adhabu ya kukaa chini ya mwembe toka asubuhi hadji jioni ili nijadili na huyo shetani kwa nini alitoka huko na kunichukua darasanio had chumbani bila ruhusa......

  ndipo nikajua shetani wa mtu ni mtu mwenyewe na mawazo yake......
   
 19. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #19
  Jun 16, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mwanasheria: Mheshimiwa Mchungaji, umesema unafahamu matakwa ya kiongozi kutoa tamko.

  Mchungaji: Ndiyo, na nilikuwa nikitoa mwaka hadi mwaka.

  Mwanasheri: Unasema ulipozirejesha fomu zako hukusaini popote, kwa nini.

  Mchungaji: Kwa sababu kulikuwa na foleni ya wabunge na kila mtu alikuwa anarejesha na mimi nilikuwa na haraka.

  Mwanasheria: Mchungaji unasema uongo, kwa nini hukusaini, sekretarieti itakuamini vipi, kwani hata hiyo nakala ni ile fomu ambayo uliichukua halafu hukuirudisha au katika ofisi za bunge ulikorejesha kuna mtu anakuchukia ndiyo maana hakuirejesha sehemu inakohusika.

  Mchungaji: Hapana, lakini inawezekana ilifika mikononi mwa shetani. Nilikuwa sina wasiwasi nilijua zimefika na niko salama kwani suala hili ni sawa na mtu anajiona yuko ndani ya nyumba lakini kumbe yuko nje na simba anakuja kumkamata.

  Mwanasheria: Unasema ofisi ya Spika ndiko ulikokabidhi, mbona ndiyo waliotuletea majina yenu au unataka kutuambia ofisi hiyo hawako makini na kutunza kumbukumbu.

  Mchungaji: Mimi sisemi kama kuna hujuma, ila ni shetani tu.

  Mwanasheria: Unazungumzia shetani kila mara, huyu shetani ni nani.

  Mchungaji: Ni roho chafu.

  Mwanasheria: Ndani ya dunia hii ya sayansi unaweza kuamini hayo.

  Mchungaji; Ndiyo, yupo huyu shetani na kama Mungu angeshuka leo hii angesema ukweli kuwa nimerudisha fomu hizo.

  Wakati mwanasheria huyo akiendelea kulishawishi baraza lisiamini utetezi wa Mchungaji huyo kwa kusisitiza kuwa nakala hiyo fomu yake iko nyumbani kwa Mchungaji ambayo hakuirejesha kwenye tume.

  Kauli hiyo ilimlazimu Jaji Lubuva kuingilia kati kuwa anachozungumza mwanasheria huyo ni tuhuma na hana ushahidi wowote, hivyo aendelee kuuliza maswali ya msingi ingawa mwanasheria huyo alisisitiza kuwa ni ukweli kwani hakuna nakala halisi, aliendelea na maswali.

  Mwanasheria: Unasema ulikwenda kwenye ofisi ndogo za Tume ya Maadili pale Dodoma, je, ulijitambulisha kwa maofisa wa Tume?

  Mchungaji: Ah! sikujitambulisha, wananijua si unajua mimi ninafahamika sana, nilipofika tu pale walianza kuniita, 'mchungaji, mchungaji, bwana asifiwe!

  Mwanasheria; Lakini Mchungaji mimi sikufahamu!

  Mchungaji: Ah! leo si ndiyo wajina umenifahamu? (Mwanasheria huyo anaitwa Getrude).

  Hata hivyo, mwanasheria huyo aliliomba baraza kutupilia mbali utetezi wa mbunge huyo na kumchukulia hatua kali.

  Hata hivyo, Mchungaji Rwakatare aliendelea kujitetea, "Mimi nimerudisha fomu hizo Mungu ni Shahidi".

  Baada ya kumalizika kwa utetezi huo, Jaji Lubuva alisema baraza litatoa mapendekezo kwa upande mwingine unao husika kwa hatua zaidi.

  Baada ya hatua hiyo Mchungaji Rwakatare aliwainamia wanasheria na kisha meza ya majaji na kutamka "Mungu awabariki sana" kisha kutoka nje.

  Mbunge mwingine aliyefikishwa jana katika baraza hilo ni Bw. Moshi Kakoso wa Mpanda Vijijini (CCM) ambaye naye anasubiri uamuzi wa baraza.

  Pindi wabunge hao watakapopatikana na hatia, adhabu wanazostahili kuzitumikia ni kufukuzwa kazi (Ubunge), kushushwa cheo, kujiuzulu au kuonywa.

  Kwa mujibu wa orodha ya viongozi wa umma watakaofikishwa kwenye baraza la madili, hadi Juni 24, mwaka huu ni 23 wakiwemo wabunge tisa, sita kati yao tayari wamekwishahojiwa. Watatu waliobaki na Mbinga Magharibi (CCM), Bw. John Komba na wa Hai (Chadema), Bw. Freeman Mbowe.

  Wengine ni madiwani, wakurugenzi, mahakimu, majaji na Balozi wa Tanzania nchini Malaysia, Bw. Abdul Cisco Mtiro.

  Baraza hilo linaongozwa na Jaji Mstaafu Lubuva akisaidiwa na Jaji Mstaafu Khamis Msumi na Katibu Mkuu Mstaafu Bw. Gaudios Tibakwatila.
   
 20. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #20
  Jun 16, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  huyu mama kichaa kweli teh!
   
Loading...