Mchungaji Peter Msigwa ashikwa pabaya Iringa mjini

View attachment 885836
-Kasi ya RC Hapi yamtia yamtia hofu ya kung’olewa ubunge 2020

-wivu wamtesa ataka ashirikishwe kuwashughulikia wazembe, Asema RC Hapi anapata sifa peke yake
NA JOANITHA KIWALE

MBUNGE wa Iringa mjini, Peter Msigwa,ameingiwa hofu na kasi ya utendaji kazi wa mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi na kusema kasi hiyo haiwezi kumtoa katika nafasi yake ya Ubunge mwaka 2020.

Amesema kasi ya Hapi, kuwawajibisha wafanyakazi wazembe imekuwa kubwa na kutaka kazi hiyo waifanye kwa pamoja kwa kile alichoeleza mkuu huyo anataka kujijenga peke yake.

Alisema hata dhana ya mkuu wa mkoa wa Iringa ya kuwataka wananchi wabadilike kifikra na kuwa na maendeleo mapya(dhana iliyopewa jina la Iringa mpya),haikupaswa kutolewa na kiongozi huyo.

Mchungaji Msigwa alitoa kauli hiyo jana mjini Iringa, ikiwa ni siku chache tokea mkuu wa mkoa huo, Ally Hapi,afanye ziara kwa ajili ya kushughulikia kero za wananchi na kutatua.

Kufuatia ziara hiyo ya RC Hapi masuala mbali mbali yaliibuliwa, ikiwa ni pamoja na kubaini uzembe wa baadhi ya watendaji katioka mkoa huo na kuamua wachukuliwe hatua.

Katika mkutano wake wa jana na waandishi wa habari Mchungaji Msigwa, alisema Rc Hapi,amekuwa mkali kwa wafanyakazi wasiotekeleza wajibu wao,tofauti na viongozi waliomtangulia katika nafasi hiyo ndani ya mkoa wa Iringa
.
“Lazima mjue kiongozi wa kweli hufurahi na kupongeza mafanikio ya wengine pasipo kuona gele, pamoja na kwamba mimi ni mbunge kwa tiketi ya Chadema, nimejipambanua wazi wazi kutambua mchango wa viongozi wanaofanya vizuri”alisema Msigwa.

Madai anayolalamikia Msigwa kuwa hakushirikishwa ni pamoja na kitendo cha RC Hapi, kutaka afisa maendeleo wa Iringa asimamishwe kazi, kwa sababu alishindwa kuwapa walemavu wa kusikia, fedha za kushughulikia changamoto zao.

Pia alilalamikia kitendo cha Hapi,kuulizia sababu ya wananchi kutozwa kiasi cha 12800 katika hospitali ya Iaringa ilihali serikali imeshatoa maelekezo juu ya wagonjwa kutokutozwa fedha.

Mchungaji Msigwa katika taarifa yake kwa waandishi hiyo jana alieleza kuwa amekerwa na hatua ya mkuu wa mkoa huo, kumuweka ndani diwani wa viti maalum Chdema,aliyeamuru nyumba ya mwananchi ivunjwe pasipo kuwa na ruhusa ya mipango miji

Miongoni mwa mambo ambayo Msigwa analalamikia ni uamuzi wa mkuu wa mkoa huo, kuzuia madiwani kupewa tenda za halmashauri hiyo, kwa kile alichoeleza kuwa itakuwa ni vigumu kwao kuhoji ubadhirifu wowote katika miradi hiyo.
Msigwa ni big head usije kumlinganisha na hao average brain..!
 
mtoa mada ninaomba cv yako kabla sijajibu ili nijue naongea na nani......
mimi nimehudhulia mikutano yake na hasa siku ya kufunga hapo mwembe togwa na hotuba ya mh.msigwa na waandishi wa habari kiufupi tafuta namna nyingine ya kutumika....
kwa upande wa kero alizokuwa anatatua kama mlivyokuwa mnasema ni kusumbua tu wananchi na kuwadhalilisha... kwa mfano kila anayetoa kero utamsikia mkuu wa mkoa akise wee na nanii hi kero yako nendeni mkaongee uko nyuma ya jukwaaa.... aje mwingine.....kwa hiyo huko ndookutatua kero???? ....
Alafu jamaa ana viamli vya kijinga ginga sana eti anamuamlisha RPC alinde wananchi ili wacheze mziki hadi saa tano usiku... asante wananchi maana hakubaki mtu Iringa ina kumbi za starehe kama LA PARTE NA VIP na sio kucheza kwenye vumbi
Mimi nilikuwa iringa hivi juzi ingawa sijahudhuria mikutano ya RC ila nilipata feedback za mikutano yake kwenye vigenge vya watu wa kawaida kama stendi pale na sokoni . Wengi wanafurahia aina yake ya uongozi hasa hasa madudu ya hospitali na pia yule mzee aliyebomolewa nyumba yake kutokana na chuki za kisiasa zimewagusa wengi. Kama jamaa ataendelea na mwendo huu basi mkoa huu atauweza maana manyanyaso mengine wanayofanyiwa wananchi yanatia kichefuchefu.
 
Back
Top Bottom