christopher Hermes
Member
- Sep 30, 2014
- 34
- 25
-Kasi ya RC Hapi yamtia yamtia hofu ya kung’olewa ubunge 2020
-wivu wamtesa ataka ashirikishwe kuwashughulikia wazembe, Asema RC Hapi anapata sifa peke yake
NA JOANITHA KIWALE
MBUNGE wa Iringa mjini, Peter Msigwa,ameingiwa hofu na kasi ya utendaji kazi wa mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi na kusema kasi hiyo haiwezi kumtoa katika nafasi yake ya Ubunge mwaka 2020.
Amesema kasi ya Hapi, kuwawajibisha wafanyakazi wazembe imekuwa kubwa na kutaka kazi hiyo waifanye kwa pamoja kwa kile alichoeleza mkuu huyo anataka kujijenga peke yake.
Alisema hata dhana ya mkuu wa mkoa wa Iringa ya kuwataka wananchi wabadilike kifikra na kuwa na maendeleo mapya(dhana iliyopewa jina la Iringa mpya),haikupaswa kutolewa na kiongozi huyo.
Mchungaji Msigwa alitoa kauli hiyo jana mjini Iringa, ikiwa ni siku chache tokea mkuu wa mkoa huo, Ally Hapi,afanye ziara kwa ajili ya kushughulikia kero za wananchi na kutatua.
Kufuatia ziara hiyo ya RC Hapi masuala mbali mbali yaliibuliwa, ikiwa ni pamoja na kubaini uzembe wa baadhi ya watendaji katioka mkoa huo na kuamua wachukuliwe hatua.
Katika mkutano wake wa jana na waandishi wa habari Mchungaji Msigwa, alisema Rc Hapi,amekuwa mkali kwa wafanyakazi wasiotekeleza wajibu wao,tofauti na viongozi waliomtangulia katika nafasi hiyo ndani ya mkoa wa Iringa
.
“Lazima mjue kiongozi wa kweli hufurahi na kupongeza mafanikio ya wengine pasipo kuona gele, pamoja na kwamba mimi ni mbunge kwa tiketi ya Chadema, nimejipambanua wazi wazi kutambua mchango wa viongozi wanaofanya vizuri”alisema Msigwa.
Madai anayolalamikia Msigwa kuwa hakushirikishwa ni pamoja na kitendo cha RC Hapi, kutaka afisa maendeleo wa Iringa asimamishwe kazi, kwa sababu alishindwa kuwapa walemavu wa kusikia, fedha za kushughulikia changamoto zao.
Pia alilalamikia kitendo cha Hapi,kuulizia sababu ya wananchi kutozwa kiasi cha 12800 katika hospitali ya Iaringa ilihali serikali imeshatoa maelekezo juu ya wagonjwa kutokutozwa fedha.
Mchungaji Msigwa katika taarifa yake kwa waandishi hiyo jana alieleza kuwa amekerwa na hatua ya mkuu wa mkoa huo, kumuweka ndani diwani wa viti maalum Chdema,aliyeamuru nyumba ya mwananchi ivunjwe pasipo kuwa na ruhusa ya mipango miji
Miongoni mwa mambo ambayo Msigwa analalamikia ni uamuzi wa mkuu wa mkoa huo, kuzuia madiwani kupewa tenda za halmashauri hiyo, kwa kile alichoeleza kuwa itakuwa ni vigumu kwao kuhoji ubadhirifu wowote katika miradi hiyo.