Mchungaji Mwakipesile: Namuunga mkono Tundu Lissu kwenda Ngorongoro kuongea na Wamasai lakini ananikeraga anapomsema vibaya Hayati Magufuli!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
83,978
141,994
Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile amesema ni Haki yake ya kikatiba mh Tundu Antipas Lisu kwenda Ngorongoro kuongea na Wamasai walioko kwenye najaribu makubwa.

Mchungaji Mwakipesile amesema huwa anapishana na Tundu Lisu katika mambo mengi na hasa pale anamsemaga vibaya shujaa Magufuli lakini hilo haliondoi Ukweli kwamba Lissu ni Kiongozi makini na huwa anamuombea kwa Mungu wa mbinguni aje kuliongoza Taifa hili.

Nawatakia Jumatatu Njema 😄
 
Magu alifanya mambo mengi ya hovyo yanayotugharimu mpaka leo hii ikiwamo kuvuruga uchaguzi na athari zake ni pamoja na hili Bunge la ajabu kabisa lililopitisha mkataba mbovu wa bandari.

Ni Bunge hili pia limeshindwa kusimamia hata hii issue ya Ngorongo .

Ni chini ya utawala wa Magu, Tundu Lissu alikuwa auwawe na mpaka leo hakuna aliekamatwa.

Ni utawala wa Magu uliovunja mikataba mingi kienyeji na matokeo yake tuna kesi kibao kwenye mahakama za kimataifa na nyingine tumeshindwa na kutakiwa kulipa mabilioni ya shilingi kama adhabu/fidia ya kuvunja mikataba kiholela.

Ni katika utawala wake, nchi iliingia gharama kubwa za kurudia uchaguzi kwa hoja za kipuuzi kabisa za watu kuunga juhudi mkono na kutia nchi hasara kwasbabu za kijinga kabisa.

Ni Magu huyu kaja na rundo la miradi ya matrilioni pasipo kuwa na chanzo cha uhakika cha kupata hela kugharamia hiyo miradi matokeo yake tumekopa kupitiliza na deni la Taifa sasa limepaa kupitiliza.
 
Je kumsema vibaya ndo kumkomesha au kumuadhibu huko alipo?
 
Iwe fundisho Kwa wengine.Kumbuka kuna Watoto,mke, Dada, Kaka zake na ndugu.Hao ndio Target haswaaa Wajue ndugu yao alidhulumu watu.Wajue kwamba unapofanya maovu ukiwa kiongozi siku ukifariki tutakusimanga tu🤔
Umemuelewa vibaya mno.
 
Iwe fundisho Kwa wengine.Kumbuka kuna Watoto,mke, Dada, Kaka zake na ndugu.Hao ndio Target haswaaa Wajue ndugu yao alidhulumu watu.Wajue kwamba unapofanya maovu ukiwa kiongozi siku ukifariki tutakusimanga tu🤔
Lingekuwa ndiyo fundishi unafikiri wangeenda kusaini lile li IGA? na bado unawesema wakiwa hai na tena wakiwa madalakani na wanasikia na wanaweza kufanya maamuzi ila bado wamekaza shingo kuwa lile dude liko sawa halina shida.
 
Magu alifanya mambo mengi ya hovyo yanayotugharimu mpaka leo hii ikiwamo kuvuruga uchaguzi na athari zake ni pamoja na hili Bunge la ajabu kabisa lililopitisha mkataba mbovu wa bandari.

Ni Bunge hili pia limeshindwa kusimamia hata hii issue ya Ngorongo .

Ni chini ya utawala wa Magu, Tundu Lissu alikuwa auwawe na mpaka leo hakuna aliekamatwa.

Ni utawala wa Magu uliovunja mikataba mingi kienyeji na matokeo yake tuna kesi kibao kwenye mahakama za kimataifa na nyingine tumeshindwa na kutakiwa kulipa mabilioni ya shilingi kama adhabu/fidia ya kuvunja mikataba kiholela.

Ni katika utawala wake, nchi iliingia gharama kubwa za kurudia uchaguzi kwa hoja za kipuuzi kabisa za watu kuunga juhudi mkono na kutia nchi hasara kwasbabu za kijinga kabisa.

Ni Mafisadi huyu kaja na rundo la miradi ya matrilioni pasipo kuwa na chanzo cha uhakika cha kupata hela kugharamia hiyo miradi matokeo yake tumekopa kupitiliza na deni la Taifa sasa limepaa kupitiliza.
Sasa kama mkataba yenyewe ni kama hii ya IGA kama una akili timamu kwanini usivunje? Si bora yeye ata alitutungia sheria kuwa mikataba inayohusu Rasimali za Taifa itakayoingiwa iende Bungen at least alijaribu kuweka uwazi wananchi wajue rasimali zao zinatumikaje kuliko huyu anaetaka kwenda kuondoa hicho kifungu ili iwe siri?

Wabunge wa CCM hakuna ambae atakuja kupinga kitu kilichowasilishwa na Serikali ata siku moja, awe ametoka kwenye uchaguzi wa 2015, 2020, au 2025 usije mtagemea mbunge alietokana na CCM aje kukataa hoja iliyowasilishwa mezan na Serikali ata siku moja sababu wanaogopa kufukuzwa uanachama na hatimae kukosa Ubunge.
 
johnthebaptist huyu mchungaji ni wa kanisa gani na yupo wapi? Maelezo yako hayajitoshelezi kabisaa
Huyu Mchungaji yuko huko Mbeya na ana kanisa lake- CCM wanamjua sana na kila siku anamtuhumu mtu fulani wa usalama wa taifa kwamba alimuulia mtoto wake ili wamunyamazishe lakini ndio kwanza chura kapigwa teke. Ana clip zake nyingi tu youtube... mtafute, sio kila kila kutafutiwa.
 
Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile amesema ni Haki yake ya kikatiba mh Tundu Antipas Lisu kwenda Ngorongoro kuongea na Wamasai walioko kwenye najaribu makubwa.

Mchungaji Mwakipesile amesema huwa anapishana na Tundu Lisu katika mambo mengi na hasa pale anamsemaga vibaya shujaa Magufuli lakini hilo haliondoi Ukweli kwamba Lissu ni Kiongozi makini na huwa anamuombea kwa Mungu wa mbinguni aje kuliongoza Taifa hili.

Nawatakia Jumatatu Njema
Shujaa wako wa mchongo
 
si hakuna watu kule ngorongoro walishahamishiwa huko Tanga au kuna watu upande mwingine?
 
Magu alifanya mambo mengi ya hovyo yanayotugharimu mpaka leo hii ikiwamo kuvuruga uchaguzi na athari zake ni pamoja na hili Bunge la ajabu kabisa lililopitisha mkataba mbovu wa bandari.

Ni Bunge hili pia limeshindwa kusimamia hata hii issue ya Ngorongo .

Ni chini ya utawala wa Magu, Tundu Lissu alikuwa auwawe na mpaka leo hakuna aliekamatwa.

Ni utawala wa Magu uliovunja mikataba mingi kienyeji na matokeo yake tuna kesi kibao kwenye mahakama za kimataifa na nyingine tumeshindwa na kutakiwa kulipa mabilioni ya shilingi kama adhabu/fidia ya kuvunja mikataba kiholela.

Ni katika utawala wake, nchi iliingia gharama kubwa za kurudia uchaguzi kwa hoja za kipuuzi kabisa za watu kuunga juhudi mkono na kutia nchi hasara kwasbabu za kijinga kabisa.

Ni Magu huyu kaja na rundo la miradi ya matrilioni pasipo kuwa na chanzo cha uhakika cha kupata hela kugharamia hiyo miradi matokeo yake tumekopa kupitiliza na deni la Taifa sasa limepaa kupitiliza.
JPM alikuwa muungwana sana kwa wananchi wa Tanzania kwa kufanya maamuzi ambayo ambay ilikuwa vigumu mno mtu mwingine kujitoa ufahamu kushughulika nayo bila kujali athari zilizojitokeza ikiwemo hata kuhatarisha maisha yake kwa faida ya wengi
1. Bunge hili linahusikaje na JPM ambapo wapo viongozi ndio wanaolisimamia kwa sasa na wana akili timamu na elimu za kutosha?
2. Kwani JPM yumo ndani ya bunge lililopo sasa na kwamba ndiye anayewaongoza kuridhia kila kitu ikiwemo huo mktabata wa IGA myeyusho?
3. Alyepo kwenye jumba jeupe na kiti cha dhahabu unamsifia kwa demokrasia na kutenda haki ameshindwaje kuwasimamia wakati JPM hayupo kukujibu hoja zako za kizinduna na mufilisi?
4. Walotaka kumwua mh TA Lissu wanahusikaje na JPM ambaye hakuwepo eneo la tukio wala uthibitisho wa kuwatuma?
5. Aliyepo madarakani kwa sasa na unamwamini kwa demokrasia na kutenda haki ameshindwaje kuwakamatawatuhumiwa hao kama wapo kama ameweza kuwaondoa viongozi wote walioteuliwa na JPM?
6. Unathibitishaje kwamba huyo aliyepo madarakani kwa sasa na wewe unayelalamika kumrushia lawama JPM ambaye hayupo kujibu hoja yako hukuhusika na tukio hilo la jaribio la kuua ili kumchafua mwamba JPM kwa sababu za kisiasa?
7. Mikataba mibovu inayonyonya rasilimali za taifa unategemea ivunjwe kistaarabu na kwa kubembekleza kwa sababu zipi?
8. Mbona humshambulii aliyeingia mikataba iliyopelekea hadi JPM kuchukua maamuzi magumu kwa niaba ya nchi ili kunusuru uhuru na maslahi ya taifa kwa vizazi vingi vijavyo?
9. Kurudia uchaguzi kwa sababu zilizoainishwa na katiba ni takwa la kisheria kwa hiyo hoja ya kwamaba ni sababu za kipuuzi kuunga mkono juhudi za serikali kutoka upinzani kwanini wewe na wenzio msiwajibishwe na kutiwa kitanzi kwa kukubali kuhongwa au kushawishiwa kwa njia yoyote ili ulambe asali kwa kivuli cha maridhiano batili, na haramu yasiyoshirikisha vyama vingine vya siasa, taasisi zisizo za kiraia na jamii zingine vyote kwa sababu zenu za kibinafsi na kiharifu dhidi ya mali za umma?
10. Miradi mikubwa (grand and white elephant projects) kama unavyita si ndioinayoliheshimisha taifa kwa sasa au unajitoa ufahamu kwa makusudi na kwa kuonesha bayana upande jinsi ulivyokuwa na chuki zako binafsi dhidi ya JPM?
11. Ikulu na serikali kuhamia Dodoma ni azimio la serikali tangu mwaka 1973 hajalianza JPM, yeye katekeleza kiukamilifu kwa vitendo bila kuingiza siasa za visingizio?
12. Ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) ilifanywa ili kuendana na mahitaji ya miundo mbinu ya kisasa inayoharakisha shughuli za kiuchumi, kurahisisha mawasiliano na uchukuzi kwa muda mwafaka
13. Ujenzi wa bwawa la umeme la JKN Hydro power huko Rufiji ni wazo la muasisi wa taifa la Tanzania Julius Kambarage Nyerere hivyo JPM ambaye siku zote alipenda vitendo na matokeo akalitekeleza bila kusikiliza wakwamishaji na wezi wa rasilimali za taifa kwa faida zao binafsi
14. Ujenzi na upanuzi wa barabara za njia nane Dar-Morogoro ni uamuzi na utekelezaji wa dira ya mipango ya serikali kwa muda mrefu ; kama ilivyo ada yeye JPM alianza kufanya kwa vitendo ijapokuwa alikumbana na upinzani mkubwa kutoka kwenu wezi na wakiukaji wa sheria
15. Ununuzi wa ndege kadhaa za serikali kwa niaba ya Watanzania ulifanywa ili kuendana na usindani wa biashara, uchukuzi wa kisasa na mwasiliano kwa kulingana na teknolojia ili kukuza uchumi kwa dima ya maendeleo ya taifa
16. Kukataa ujenzi wa bandari ya Bagamoyo na Dar bila kuzingatia maslahi ya nchi kwa kumilikishwa wawekezaji wa nje na kuwatelekeza wazawa kwa faida ya watu wachache
17. Ujenzi wa madaraja kama (Busisi-Kigongo huko Mwanza) kama sehemu ya eneo la Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuhakikisha shughuli za kiuchumi wa ndani na nje ya nchi kama Rwanda, Burudni na Uganda zinaboreshwa kukidhi huduma hiyo lakini pia ni haki ya wanchi wa eneo hilo kuwa miundo mbinu ya kisasa kurahisisha usafiri na shughuli za kiuchumi lakini pia usalama
18. Ujenzi wa meli katika maziwa makuu ya Viktoria na Tangayika kwa manufaa ya uchumi wa nchi na haki ya raia kupata usafiri majini vya uhakika na salama
19. Ununuzi wa rada nne kuongozea ndege kwa ajili ya usalama wa nchi na kupunguza gharama za kulipia kwamwendeshaji wa kigeni kutokea Kenya
20.Ujenzi wa mahakama mpya za kisasa na kufunga mitambo ya TEHAMA ilikukuza ufanisi na kuharakisha utolewaji wa haki kwa wananchi
21. Deni la taifa limepaa baada ya awamu ya sita kuingia madarakani kwa kukopa kiasi kikubwa cha pesa za kigeni na kupoteza uwezo wa kuuza bidhaa nchi za nje ili kupata mapato ya kigeni kwa dola pamoja na hayo hakuna kitu chochote cha kuonekana chenye hadhi na alama ya kidumu kifanyika kusadifu mikopo iliyochukuliwa zaidi ya kulea ufisadi wa kutisha bila hatua yoyote kuchukuliwa dhidi ya waharifu zaidi kuhamishwa kwenda eneo jingine
22. Ujenzi wa fly over bridge Dar ni mipango ya serikali kwa kulingana na changamoto wanazokabiliana nazo wananchi katika utekelezaji wa majukumu yao ya kuchangia kukuza uchumi na pato la taifa
23. Badala ya kumsimanga aliyesaini IGA ya mikataba tofauti 30 ikiwemo posta, bandari na mbuga za wananyama bla kuzingatia madhara dhidi ya uhuru na usalama wa nchi wewe unamrushia uchafu huo JPM aliyekuwa amejibainisha hadharani kudhibiti wizi kama wewe uliyekuwa miongoni mwao kwa kutegemea kipato kwa kulingana na hati ya malipo ya mshahara baada ya kukamilisha kazi uliyopewa kufanya katika muda maalum wa makubaliano (salary slip)?
24. Gharama za umeme kushushwa katika kufungiwa wananchi vijijini na maeneo mengine kwa kulingana na tathimini ya hali ya kiuchumi ya wakazi wake (shiling 27,000) ili awe mlipaji endelevu wa hiyo nishati badala ya gharama za kibiashara za shilingi 330,000/= hadi 1,600,000/= kwa sasa lakini hakuna tija umeme kila siku unakatwa bila sababu za msingi hivyo shirika kuzidi kudorora pamoja na kwamba wanalipisha kiwango kikubwa mno kwa sasa
25. Kudhibiti upandishaji holela wa bei za biadhaa za mafuta ya gari, mafuta ya kula na vyakula vya aina mbalimbali
26. Uboreshaji wa hospitali za wilaya na mikoa na kununua mitambo saidizi kubaini magonjwa sugu kwa kutumia T-Scan, MRI nk
27. Kudhibiti upungufu wa pesa za kigeni kwa kushughulika na wafanyabiashara wabinafsi wenye lengo la kudhoofisha uchumi wa nchi
28. Kudhibiti magenge ya kiharifu yaliyoibuka huko Mkuranga,, Kibiti na Rufiji maarufu kama (MKIRU) pamoja na waasi kutoka Msumbiji kaskazini waliokuwa wamejichanganya na raia Mtwara vijijini hasa ziwani na mnazi bay
29 Kudhibiti walanguzi wa korosho huko Mtwara na Lindi
30 Kudhibiti pesa ya Tanzania kushuka thamani kama inavyoonekana leo

Mtamsema vibaya lakini laana itakuwa juu yenu wakati mnawasema vizuri walio hai lakini huku wakitenda mabaya zaidi majuto mjukuu kwenu mtayaishi bila matumaini yoyote.

Acheni kuongelea ubaya wa JPM jikite kueleza kwanini sasa hivi hali ni mbaya zaidi wakati mna viongozi mnaowaamini lakini wanashindwa kuwakwamua?
 
Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile amesema ni Haki yake ya kikatiba mh Tundu Antipas Lisu kwenda Ngorongoro kuongea na Wamasai walioko kwenye najaribu makubwa.

Mchungaji Mwakipesile amesema huwa anapishana na Tundu Lisu katika mambo mengi na hasa pale anamsemaga vibaya shujaa Magufuli lakini hilo haliondoi Ukweli kwamba Lissu ni Kiongozi makini na huwa anamuombea kwa Mungu wa mbinguni aje kuliongoza Taifa hili.

Nawatakia Jumatatu Njema 😄
Ila Magufuli hakukukera alipoamuru apigwe risasi! Hakukukera alipozuia viongozi kumtembelea hosipitali! Hskukukera alipo waadhibu waliomtembelea hosipitali!
 
Mchungaji Mbarikiwa Mwakipesile amesema ni Haki yake ya kikatiba mh Tundu Antipas Lisu kwenda Ngorongoro kuongea na Wamasai walioko kwenye najaribu makubwa.

Mchungaji Mwakipesile amesema huwa anapishana na Tundu Lisu katika mambo mengi na hasa pale anamsemaga vibaya shujaa Magufuli lakini hilo haliondoi Ukweli kwamba Lissu ni Kiongozi makini na huwa anamuombea kwa Mungu wa mbinguni aje kuliongoza Taifa hili.

Nawatakia Jumatatu Njema
Mwakipesile kama ndiyo wewe umepigwa risasi zote zile kwa amri ya Magufuli ungeacha kumlaani?
 
Back
Top Bottom