Mchungaji Matsai: Waluteli Wana tabia ya kuongea sana na kulalamika, kuna mmoja alitaka kuzuia Ujenzi wa Ubungo Plaza Rais Mkapa akamdhibiti!

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,004
142,036
Mchungaji Matsai wa KKKT Kimara amewataka Waumini wa Kanisa hilo kuacha tabia ya kuongea sana na kulalamika lalamika na badala yake wafanye kazi kwa bidii

Matsai amesema kuna mluteli mmoja alikuwa Kiongozi serikalini na alijaribu kuzuia Ujenzi wa Ubungo Plaza kwa madai taratibu hazijafuatwa Bahati mzuri Rais Mkapa aliingilia Kati na kumkemea. Leo hii Ubungo Plaza inachangia pakubwa Kwenye uchumi wa nchi

Kadhalika Matsai amekemea tabia ya kumkosoa Rais na kusema ni maadili ya hovyo kabisa, " hawa Marais wetu wangekuwa wanasoma kila wanachoandikwa mitandaoni wangeweza kufa kabla ya wakati Wao" amesisitiza mchungaji

Katika Performance Management hatuangalii Process bali tunachozingatia ni Matokeo, amemalizia mchungaji Matsai

Nawatakia Dominica njema!
 
Kwa hiyo mtu akitoa maoni yake tunaanza kuangalia dhehebu lake?ndio tukagundua walutheri wanalalamika sana?
Mchungaji umetokota ,huwezi kuangalia result bila uagalia process
Mwendazake alifanya mengi ila process za kishetani
Hata we mchungaji umetuchangisha sadaka nyingi kununua adhi mbele ya kanisa kumbe ni hifadhi ya barabara.
Sadaka zetu zimeenda bure kea sababu uliignore process hukufuatilia wizarani kipindi kanisa linauziwa hifadhi ya barabara au lilikuwa ni dili tu ulitupiga
Rais pia ni mtu,kusemwa kunamjenga kuliko kumsifia hata anapokosea
 
Awaambie ccm waondoe umaskini wa kukosa mtundu ya choo mashuleni na ufisadi...., ndio kelele zitaisha
 
Kwa hiyo mtu akitoa maoni yake tunaanza kuangalia dhehebu lake?ndio tukagundua walutheri wanalalamika sana?
Mchungaji umetokota ,huwezi kuangalia result bila uagalia process
Mwendazake alifanya mengi ila process za kishetani
Hata we mchungaji umetuchangisha sadaka nyingi kununua adhi mbele ya kanisa kumbe ni hifadhi ya barabara.
Sadaka zetu zimeenda bure kea sababu uliignore process hukufuatilia wizarani kipindi kanisa linauziwa hifadhi ya barabara au lilikuwa ni dili tu ulitupiga
Rais pia ni mtu,kusemwa kunamjenga kuliko kumsifia hata anapokosea
"Viongozi wa kweli mtawatambua kwa matunda yao"

Kiukweli huyu jamaa now days ameshaanza kulewa umaarufu, na matunda yake kwenye jamii yetu yanaanza kutia mashaka.

Anyway, tumwombee neema.
 
Mchungaji Matsai wa KKKT Kimara amewataka Waumini wa Kanisa hilo kuacha tabia ya kuongea sana na kulalamika lalamika na badala yake wafanye kazi kwa bidii

Matsai amesema kuna mluteli mmoja alikuwa Kiongozi serikalini na alijaribu kuzuia Ujenzi wa Ubungo Plaza kwa madai taratibu hazijafuatwa Bahati mzuri Rais Mkapa aliingilia Kati na kumkemea. Leo hii Ubungo Plaza inachangia pakubwa Kwenye uchumi wa nchi

Kadhalika Matsai amekemea tabia ya kumkosoa Rais na kusema ni maadili ya hovyo kabisa, " hawa Marais wetu wangekuwa wanasoma kila wanachoandikwa mitandaoni wangeweza kufa kabla ya wakati Wao" amesisitiza mchungaji

Katika Performance Management hatuangalii Process bali tunachozingatia ni Matokeo, amemalizia mchungaji Matsai

Nawatakia Dominica njema!
Kwa hiyo mtu akibaka na akazalisha mtoto,aachwe kwakuwa mtoto ni muhimu katika jamii?
 
Back
Top Bottom