Rais Samia Suluhu Hassan ametoa nafasi ya kipekee na ya kihistoria ya kuongea na vijana wa nchini hii

Fahami Matsawili

Senior Member
Mar 8, 2018
172
153
Vijana Wenzangu Rais wetu Mpendwa Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa nafasi ya kipekee na adhimu ya kuongea na Vijana wa Tanzania kupitia vijana wa mkoa wa Mwanza yapo Masuala mtambuka (Cross cutting issues) za Vijana.

Tukampokee kwa wingi na kumsikiliza kwa umakini mkubwa, Rais wetu anawapenda Vijana wa Tanzania, na ikimpendeza yeye akaona inafaa akatupa nafasi ya kumwambia chochote basi itumieni nafasi hiyo kwa hekma, busara, nidhamu ya hali ya juu kumwambia mahitaji yetu Vijana mkuu wa nchi na Amiri jeshi mkuu.

Mwaka 2016, Wizara ya kilimo nchini Tanzania ilizindua mkakati wa miaka mitano wa ushiriki wa vijana katika sekta ya kilimo, Mifugo na uvuvi(2016-2021). Mkakati ambao muda wake unaisha mwaka huu baada ya miaka mitano kuisha sasa, Mkakati huu ulilenga kuhamasisha ushiriki wa vijana katika sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi ukilenga kuwawezesha vijana kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kuweza kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi kama dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025 inavyoelekeza.

Katika mkakati huu, yapo malengo 10 ya kimkakati (Stragetic Goals - SO) ambayo yameainishwa katika mkakati huo. Malengo hayo ni:

SO 1: Kuwezesha upatikanaji wa ardhi na uwekezaji kwa vijana; hii inatokana na vijana wengi kukosa mitaji ya kuwekeza kwenye kilimo, ambapo mkakati huo ulitegemea kuwezesha vikundi 10,000 vya vijana katika kuwapatia ardhi hadi mwaka 2021.

SO 2: Kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa vijana kwa ajili ya kuwekeza kwenye kilimo; changamoto kubwa ya vijana katika uwekezaji ni mitaji.

Lengo hili la kimkakati lililenga vijana waweze kujiunga katika vikundi mbalimbali ili waweze kukopesheka na taasisi za kifedha, Mkakati ulilenga kufikia 25% ya vijana nchini katika kuwaelimisha juu ya fursa za mikopo zilizoko nchini hadi mwaka 2021, 25% ya vijana nchini kuunganishwa na mifuko ya dhamana kwa ajili ya kupata mikopo hadi mwaka 2021, Kushirikisha Saccos/Amcos 169 kwenye kupata mitaji kwenye kilimo hadi 2021 na Kuhusisha vyama vya kukopa(Vicoba) 5,000 kwenye mikopo ya kilimo.

SO 3: Kuwezesha upatikanaji wa pembejeo, zana za kisasa za kilimo na huduma wezeshi kwa vijana kwenye kilimo, mkakati huu unawapa pia fursa vijana kushiriki kwenye biashara za usambazaji wa pembejeo ili kusaidia vijana wenzao kupata pembejeo kwa wakati.

Lengo hili la kimkakati lililenga kuanzishwa kwa vituo 10 vya usambazaji wa pembejeo vinavyomilikiwa na vijana, na kufikia vikundi vya vijana 1,500 katika usambaji wa pembejeo nchini.

SO 4: Kuwezesha maendeleo na ujenzi wa miundo mbinu ya umwagiliaji; Lengo hili la kimkakati lililenga kuwezesha vijana kuweza kupata rasilimali za maji ili kurahisisha uzalishaji mashambani. Lengo hili lililenga kuwafikia 25% ya vijana nchini katika kuendesha na kusimamia miradi ya umwagiliaji.

SO 5: Kuimarisha masoko ya mazao ya kilimo nchini; Kutokana na tatizo la upatikanaji wa masoko, vijana wengi wameonekana kuzalisha lakini hawapati masoko ya uhakika, Lengo hili la kimkakati linalenga kuondoa Vikwazo vyote vya kimasoko ikiwemo kuimarisha mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuimarisha mfumuko wa bei, kuwekeza kwenye miundo mbinu ya kilimo na kuimarisha ubora wa bidhaa za mazao ya kilimo, kuunganisha vijana na mifumo ya taarifa za masoko. Lengo hili la kimkakati lililenga hadi 2021, wizara kuondoa Vikwazo vya kimasoko, kukarabati maghala 10 ya kuhifadhia mazao, kujenga maghala mengine 10, vikundi 20 vya vijana kupewa mafunzo ya uongezaji thamani (Value addition) na ubora wa bidhaa.

SO 6. Kuwezesha jitihada za kuzuia madhara ya mabadiliko ya tabia nchi na matumizi ya Teknolojia; Mkakati huu ulilenga kushirikisha taasisi za utafiti kuzalishaji teknologia wezeshi za kuzuia na kustahimili mabadiliko ya tabia nchi katika miradi inayohusisha vijana na matumizi ya mashine katika sekta ya kilimo kwa vijana,

SO 7. Kuhimiza utoaji wa elimu ya ujasiliamali utaalam katika kilimo; Mkakati huu ulilenga kusaidia vijana kuweza kupata elimu ya utaalam katika kilimo na ujasiliamali, kama tunavyojua kuwa kilimo ni sayansi, hivyo utaalam wa namna ya kuzalisha ni muhimu sana kwa vijana. Lengo hili la kimkakati linalenga kufikia vikundi 100 vya vijana katika kupata elimu ya utaalam wa kilimo na ujasiliamali nchini hadi mwaka 2021, Kusaidia vijana 100,000 nchini kupata huduma za ugani.

SO 8. Kuunganisha vijana na program mbalimbali wezeshi katika kilimo na ujasiliamali; lengo hili la kimkakati lililenga kuwezesha vijana kuunganishwa na program mbalimbali zinazotolewa na taasisi kama MVIWATA, SUGECO, ANSAF na PASS. Lengo hili la kimkakati lililenga kufikia vikundi vya vijana 500 nchini hadi mwaka 2021.

SO 9. Kukifanya kilimo kuwa kazi rasmi kwa vijana; Wizara ya kilimo ililenga kuifanya sekta ya kilimo kuwa kazi rasmi kwa vijana, tofauti na mtazamo wa sasa wa vijana ambao wanaichukulia sekta ya kilimo kama kazi yenye adhabu na taabu nyingi.

Lengo hili la kimkakati lililenga kuwafikia vijana mbalimbali kwa kufanya midahalo 10 mikubwa ya ushiriki wa kilimo kwa vijana hadi mwaka 2021.

SO. 10. Kuinua uelewa wa vijana kuhusu mambo mtambuka(Cross cutting issues) kama mambo ya Ukimwi, michezo, mazingira, afya na kuhusisha makundi maalum, kama walemavu na kadhalika

Lengo hili la kimkakati lililenga kufikia 25% ya vijana kuhusu elimu juu ya kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi na mambo mengine ya kimtambuka.

Chanzo: National Strategy for Youth Involvement in Agriculture (NSYIA) 2016-2021

Fahami Matsawili Juma.

IMG_5253.jpg

IMG_5255.jpg

IMG_2650.jpg

IMG_5669.jpg

IMG_5915.jpg

IMG_5363.jpg

IMG_2582.jpg
 
Wewe jamaa Huwa ni Chenga tu .Hujawahi kuwasemea vijana kazin yako Huwa ni kutafuta fursa za kuteuliwa lakini Naona ulisahaulika.

Kwani tatizo la vijana unazani viongozi hawalijui? Hapo zinapigwa siasa tu uko mladi siku ziende.

Kwa kukusaidia TATIZO LA VIJANA NCHI HII NI KUWEZESHWA KIUCHUMI TU.eiza kupitia AJIRA au mikopo FULLSTOP.
Zaidi ya hapo ni porojo tu.
 
Yaani unaleta bandiko na mastrategic plan ya vijana muda ukiwa umetamaladi, hii kwangu siyo sawa mkuu.

Unaishi afrika ukitambua ugonjwa wa vijana wa bara hili ni kukosa umoja na upendo sisi kwa sisi so, wkt mwingine kukumbushana hata kama kati ya vikundi 20 vilipatikana 2 ni faida kubwa sana badala ya hiki nilicho kisoma hapo juu.

Bimkubwa hataongea kuhusu mkakati unaoisha sababu haukuwa wake although anaweza kupitia humo ili kutonajisi njia aliyoipitia na hizi mambo zinapaswa kunyunyiziwa kwa vijana wasio egemea kwenye siasa course wanasiasa si watu wa kuwaamini.
 
vijana wenzangu msiniangushe
bangi tunanunua na kuvuta kwa kujificha sana
huku beer zinauzwa kila kona
Aisee bangi ihalalishwe tena tuje na mkakati wa kuifanya iwe zao kuu la kibiashara
 
Hao TADB wakiwa seriouslabda masna ukienda wanakuzingua big time mara leta hiki mara kile hufiki utaacha tu .....wanasumbua mno sidhani vijsna na vikundi vyao kuna wanaopata chochote wale hula pesa bure labda asas huko wanawapa sio vijana fukara
 
Unakuta mbunge anajisifia kusema watu wangu. Huku hao watu wakiteseka, fukara. Shule majengo shida, huduma za afya tabu. Mtu mmoja analipwa mamilioni.
Hakuna haki. Wabunge wenyewe majimboni hawaonekani. Wakienda Bungeni maswali ni yale yale toka nazaliwa hakuna linalo badilika. Utasikia korosho, Pamba, ufugaji, madini, elimu. Hivi haya yote hayajapata ufumbuzi toka wakati wa Nyerere hadi Leo! Miaka 60 tunaongelea jambo lile lile!
Ulaya ya miaka ya hamsini na tisini ilikuwa masikini si kama ya Leo. China, Malyasia, India, Korea na nyinginezo walikuwa masikini.
Je sisi watanzania tumelaniwa nini? Nyerere alitupatia viwanda leo vyote hakuna.
Shida ni nini? Nilibahatika kufanya kazi serikalini, nilipo ingia nilishangaa mengi. Hapo nikajua Tanzania kwendelea ni kazi. Tutapiga mark time.
Tunahitaji kubadili mfumo wa kiutumishi. Tunahitaji kubadili matumizi ya fedha na mshahara. Tunahitaji kubadili mfumo wa utekelezaji wa miradi.
Pia kubadili mfumo wa Bunge. Na kuwa na wabunge wachache. Kufuta viti maalum. Na wabunge wawajibishwe mara wanapokuwa si wawajibikaji.
Hivyo tunahitaji muundo mpya wa serikali. Hata baraza la mawaziri hatuhitaji utitiri wa mawaziri.

Kuna mtaalamu wa ujenzi ni Afisa mkubwa walijenga barabara isiyo na kiwango ktk kumhoji akanambia akijenga ya kiwango yeye na familia yake watakula nini?
Anajua hyo isiyo na kiwango baada ya muda itahitaji matengenezo hivyo atapata fedha. Nilichoka!

Afisa mmoja mkubwa anateuliwa na Rais akanambia usipo kula fedha ya serikali wengine wanakula. Usiangalie kuendeleza nchi. Jiendeleze mwenyewe.
Baada ya muda niliona niache kazi ya serikali na kufanya kazi katika mashirika ya kimataifa.

Tuombeni na kudai Katiba mpya. La sivyo hata vyama shindani vikiingia bado ni yale yale.
 
UPUUZI MTUPU!
Vijana Wenzangu Rais wetu Mpendwa Mhe Samia Suluhu Hassan ametoa nafasi ya kipekee na adhimu ya kuongea na Vijana wa Tanzania kupitia vijana wa mkoa wa Mwanza yapo Masuala mtambuka (Cross cutting issues) za Vijana.

Tukampokee kwa wingi na kumsikiliza kwa umakini mkubwa, Rais wetu anawapenda Vijana wa Tanzania, na ikimpendeza yeye akaona inafaa akatupa nafasi ya kumwambia chochote basi itumieni nafasi hiyo kwa hekma, busara, nidhamu ya hali ya juu kumwambia mahitaji yetu Vijana mkuu wa nchi na Amiri jeshi mkuu.

Mwaka 2016, Wizara ya kilimo nchini Tanzania ilizindua mkakati wa miaka mitano wa ushiriki wa vijana katika sekta ya kilimo, Mifugo na uvuvi(2016-2021). Mkakati ambao muda wake unaisha mwaka huu baada ya miaka mitano kuisha sasa, Mkakati huu ulilenga kuhamasisha ushiriki wa vijana katika sekta ya kilimo,mifugo na uvuvi ukilenga kuwawezesha vijana kushiriki katika shughuli za kiuchumi ili kuweza kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi wa nchi kama dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2025 inavyoelekeza.

Katika mkakati huu, yapo malengo 10 ya kimkakati (Stragetic Goals - SO) ambayo yameainishwa katika mkakati huo. Malengo hayo ni:

SO 1: Kuwezesha upatikanaji wa ardhi na uwekezaji kwa vijana; hii inatokana na vijana wengi kukosa mitaji ya kuwekeza kwenye kilimo, ambapo mkakati huo ulitegemea kuwezesha vikundi 10,000 vya vijana katika kuwapatia ardhi hadi mwaka 2021.

SO 2: Kuwezesha upatikanaji wa rasilimali fedha kwa vijana kwa ajili ya kuwekeza kwenye kilimo; changamoto kubwa ya vijana katika uwekezaji ni mitaji.

Lengo hili la kimkakati lililenga vijana waweze kujiunga katika vikundi mbalimbali ili waweze kukopesheka na taasisi za kifedha, Mkakati ulilenga kufikia 25% ya vijana nchini katika kuwaelimisha juu ya fursa za mikopo zilizoko nchini hadi mwaka 2021, 25% ya vijana nchini kuunganishwa na mifuko ya dhamana kwa ajili ya kupata mikopo hadi mwaka 2021, Kushirikisha Saccos/Amcos 169 kwenye kupata mitaji kwenye kilimo hadi 2021 na Kuhusisha vyama vya kukopa(Vicoba) 5,000 kwenye mikopo ya kilimo.

SO 3: Kuwezesha upatikanaji wa pembejeo, zana za kisasa za kilimo na huduma wezeshi kwa vijana kwenye kilimo, mkakati huu unawapa pia fursa vijana kushiriki kwenye biashara za usambazaji wa pembejeo ili kusaidia vijana wenzao kupata pembejeo kwa wakati.

Lengo hili la kimkakati lililenga kuanzishwa kwa vituo 10 vya usambazaji wa pembejeo vinavyomilikiwa na vijana, na kufikia vikundi vya vijana 1,500 katika usambaji wa pembejeo nchini.

SO 4: Kuwezesha maendeleo na ujenzi wa miundo mbinu ya umwagiliaji; Lengo hili la kimkakati lililenga kuwezesha vijana kuweza kupata rasilimali za maji ili kurahisisha uzalishaji mashambani. Lengo hili lililenga kuwafikia 25% ya vijana nchini katika kuendesha na kusimamia miradi ya umwagiliaji.

SO 5: Kuimarisha masoko ya mazao ya kilimo nchini; Kutokana na tatizo la upatikanaji wa masoko, vijana wengi wameonekana kuzalisha lakini hawapati masoko ya uhakika, Lengo hili la kimkakati linalenga kuondoa Vikwazo vyote vya kimasoko ikiwemo kuimarisha mfumo wa stakabadhi ghalani ili kuimarisha mfumuko wa bei, kuwekeza kwenye miundo mbinu ya kilimo na kuimarisha ubora wa bidhaa za mazao ya kilimo, kuunganisha vijana na mifumo ya taarifa za masoko. Lengo hili la kimkakati lililenga hadi 2021, wizara kuondoa Vikwazo vya kimasoko, kukarabati maghala 10 ya kuhifadhia mazao, kujenga maghala mengine 10, vikundi 20 vya vijana kupewa mafunzo ya uongezaji thamani (Value addition) na ubora wa bidhaa.

SO 6. Kuwezesha jitihada za kuzuia madhara ya mabadiliko ya tabia nchi na matumizi ya Teknolojia; Mkakati huu ulilenga kushirikisha taasisi za utafiti kuzalishaji teknologia wezeshi za kuzuia na kustahimili mabadiliko ya tabia nchi katika miradi inayohusisha vijana na matumizi ya mashine katika sekta ya kilimo kwa vijana,

SO 7. Kuhimiza utoaji wa elimu ya ujasiliamali utaalam katika kilimo; Mkakati huu ulilenga kusaidia vijana kuweza kupata elimu ya utaalam katika kilimo na ujasiliamali, kama tunavyojua kuwa kilimo ni sayansi, hivyo utaalam wa namna ya kuzalisha ni muhimu sana kwa vijana. Lengo hili la kimkakati linalenga kufikia vikundi 100 vya vijana katika kupata elimu ya utaalam wa kilimo na ujasiliamali nchini hadi mwaka 2021, Kusaidia vijana 100,000 nchini kupata huduma za ugani.

SO 8. Kuunganisha vijana na program mbalimbali wezeshi katika kilimo na ujasiliamali; lengo hili la kimkakati lililenga kuwezesha vijana kuunganishwa na program mbalimbali zinazotolewa na taasisi kama MVIWATA, SUGECO, ANSAF na PASS. Lengo hili la kimkakati lililenga kufikia vikundi vya vijana 500 nchini hadi mwaka 2021.

SO 9. Kukifanya kilimo kuwa kazi rasmi kwa vijana; Wizara ya kilimo ililenga kuifanya sekta ya kilimo kuwa kazi rasmi kwa vijana, tofauti na mtazamo wa sasa wa vijana ambao wanaichukulia sekta ya kilimo kama kazi yenye adhabu na taabu nyingi.

Lengo hili la kimkakati lililenga kuwafikia vijana mbalimbali kwa kufanya midahalo 10 mikubwa ya ushiriki wa kilimo kwa vijana hadi mwaka 2021.

SO. 10. Kuinua uelewa wa vijana kuhusu mambo mtambuka(Cross cutting issues) kama mambo ya Ukimwi, michezo, mazingira, afya na kuhusisha makundi maalum, kama walemavu na kadhalika

Lengo hili la kimkakati lililenga kufikia 25% ya vijana kuhusu elimu juu ya kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi na mambo mengine ya kimtambuka.

Chanzo: National Strategy for Youth Involvement in Agriculture (NSYIA) 2016-2021

Fahami Matsawili Juma.

View attachment 1816848
View attachment 1816851
View attachment 1816852
View attachment 1816854
View attachment 1816855
View attachment 1816856

View attachment 1816853
 
Hapana kilimo chochote mimi nimechagua mpunga wewe umechagua kilimo gani???

Anaongea na vijana au anawahutubia vijana? Unajua maana ya kuongea? Dhalimu alinajisi chaguzi zote za nchi hii ili wanaccm tu ndio watangazwe washindi kwa shuruti, as a result sasa hivi viongozi wa ngazi zote nchini ni waccm, ni kipi wawakilishi wote hao wameshindwa kumfikishia changamoto za vijana, mpaka yeye awasikilize mwenyewe? Achani utapeli usio na kichwa wala miguu.
 
Back
Top Bottom