Mchungaji ataka kujiua baada ya ndoa yake kucheleweshwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchungaji ataka kujiua baada ya ndoa yake kucheleweshwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Nov 18, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,657
  Trophy Points: 280
  MWINJILISTI wa Kanisa la Evangelism Assemblies of God Tanzania (EAGT) lililopo Majengo mkoani Arusha, Fanuely Sanaki (27) anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada kutaka kujiua kwa kutumia kamba.

  Tukio hilo lilitokea saa chache baada ya Mchungaji huyo kufunga ndoa na baada hapo alidai kuwa Mchungaji mwenzake aliyepaswa kufungisha ndoa hiyo, alichelewa kufika kanisani kumsababishia usumbufu kwa wageni waalikwa pamoja na msichana liyekuwa afunge nae ndoa.

  Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Leonard Paulo, alisema ndoa hiyo ilipangwa kufanyika Jumamosi iliyopita saa nne asubuhi na kwamba ilichelewa kufungwa na badala yake ikafanyika saa saba mchana; kitu ambacho hakikumpendeza bwana harusi huyo.

  Kamanda alisema Mchungaji aliyepaswa kufungisha ndoa hiyo, Marko Haule (27), alichelewa kufika na alimkuta bwana harusi ambaye ni Mwinjilisti akiwa hana raha na alikubali kufungishwa ndoa hiyo kwa ‘shingo upande.’

  Baada ya ndoa hiyo kufungwa, kesho yake Mchungaji Marko alifika nyumbani kwa bwana harusi huyo ili kumuomba radhi kwa kumchelewa, lakini kulitokea kutokuelewana kiasi cha kujibizana kwa maneno yasiyofaa.

  Kamanda alisema baada ya hapo, Mchungaji ambaye ni bwana harusi alichukua kamba ya manila na kutaka kujiua kwa kujitundika chumbani kwake na ndipo raia wema walifika na kumwokoa.

  Alipohojiwa na waandishi wa habari ni kwa nini alifikia uamuzi wa kutaka kufupisha maisha yake, Mchungaji Sanaki alisema alipitiwa na shetani ambaye anapaswa kukemewa.
   
 2. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #2
  Nov 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,358
  Likes Received: 5,657
  Trophy Points: 280
  Alipohojiwa na waandishi wa habari ni kwa nini alifikia uamuzi wa kutaka kufupisha maisha yake, Mchungaji Sanaki alisema alipitiwa na shetani ambaye anapaswa kukemewa

  haya mambo ya kusingizia mapepo kila siku yafe jamani;toka lini pepo anakuletea watu kuja kukuokoa...pepo angekuokoa ukiwa ushaninginia...weee mchungaji unatufundisha nini kwa hili;kwanza napendekeza huyo unamsimamisha kabisa uchungaji akajinyonge akiwa muumini wa kawaida...sasa mkeo kuceheleshwa ndoa unajiua,,hujui kuna kuachika si ndio ungejichoma kisu;pole weye...mapenzi kitovu cha uzembe
   
Loading...