Nyenyere
JF-Expert Member
- Sep 9, 2010
- 14,770
- 10,650
Gazeti la majira la leo limeripoti habari hizi. Anaitwa mchungaji Kennedy Mwasomola wa kanisa la mitume wapya kusanyiko la Tukuyu mjini. Ameoteshwa na Mungu mti na majani yake yanayotibu magonjwa sugu baada ya kuchemsha na kunywa kikombe. Aliota yuko kwenye foleni ya babu Loliondo. Alipokaribia kufika kupata kikombe akagundua kuwa hana hela (500). Akatoka kwenye foleni na kusimama pembeni. Ndipo akaona umbo mithili ya malaika. Akamponya uvimbe mkononi. Akamchukua mpaka kwenye mti uitwao mpandapanda. Akamwambia, " kwa kuwa wewe ni mwenyeji mwombe mzee mwenye mti huo uitwao mpandapanda ili ukatwe kwa ajili ya dawa." Mzee huyo akakubali kutoa mti bila kinyongo. Ndipo mchungaji akaamka. Akautafuta mti huo na ameshaanza kugawa dozi ya kikombe. Zaidi ya watu 2000 tayari wamekunywa. Anasema ameonyeshwa kuwa ni tawi la babu wa Loliondo.
Mwingine ni John Agunda mkazi wa Ruvu Darajani. Kaoteshwa na malaika. Ameshatoa tiba kwa zaidi ya watu 100. Hatozi hata senti moja. Haulizi mtu anaumwa nini. Ukienda kwa imani tu utapona.
Mwingine ni John Agunda mkazi wa Ruvu Darajani. Kaoteshwa na malaika. Ameshatoa tiba kwa zaidi ya watu 100. Hatozi hata senti moja. Haulizi mtu anaumwa nini. Ukienda kwa imani tu utapona.