Mchumba wangu kaniambukiza kisonono

Mchumba wangu kaniambukiza kisonono

kvelia

JF-Expert Member
Joined
Jun 24, 2009
Posts
246
Reaction score
45
Jamani wadau nisaidieni ushauri mpenzi wangu(wife to be) ameniambukiza gonorrhea(kisonono). nifanyeje na dalili zake zimeshaonekana kabisa.
Naomba ushauri wa tiba na kama ni sahihi kama nikimwacha.
 
Nenda kapime na HIV status yako, magonjwa ya zinaa huenda sana na maambukizo ya UKIMWI. Pata ushauri wa Dr ila strong antibiotics hutibu vizuri tu Gono mfano Ofloxacin, Cefixine, ama Ceftriaxine
 
Jamani wadau nisaidieni ushauri mpenzi wangu(wife to be) ameniambukiza gonorrhea(kisonono). nifanyeje na dalili zake zimeshaonekana kabisa.
Naomba ushauri wa tiba na kama ni sahihi kama nikimwacha.
Huyo your wife to be ameshakuambukiza gono na bado unajiuliza kumwacha du, ndo hapo atakapokuambiza ngoma sijui utasemaje pole mshikaji.
 
Ni sahihi kabisa ukimwacha. Kwanza nakushangaa unakuja kuomba ushauri hapa kama umwache au ubaki naye. Wala usijiulize mara mbili mbili, wewe mwache tu huyo mwanamke. Ni mchafu, kaoza, anatia kinyaa, na juu ya yote kadhihirisha utovu wa uaminifu wake kwako. Sasa ndugu unataka ubaki naye kwa minajili ipi?

Kama kakuletea gono (kisonono) sasa hivi unadhani safari ijayo atashindwa kukuletea kaswende au ukimwi? Ndugu, anza haraka iwezekanavyo.

Halafu unamwita eti mpenzi wako. Mtu akupendaye hawezi kukuletea gonjwa la zinaa. Mtu akupendaye hawezi kukudhuru kwa namna yoyote ile. Mtu akupendaye atakuheshimu na hawezi kutangatanga kwingine na kukuletea magonjwa. Huyo mwanamke hakupendi.
 
Nenda kapime na HIV status yako, magonjwa ya zinaa huenda sana na maambukizo ya UKIMWI. Pata ushauri wa Dr ila strong antibiotics hutibu vizuri tu Gono mfano Ofloxacin, Cefixine, ama Ceftriaxine

TUTAKESHA lakini TUTALALA ,kwa mana hiyo unataka kutwambiakuwa ikiwa hatutokuwa tunamuona mtowa mada hii humu javini ndio atakuwa amelikwa DOLE lake GUMBA kwenye KISIKI cha Muwaridi.
 
Jamani wadau nisaidieni ushauri mpenzi wangu(wife to be) ameniambukiza gonorrhea(kisonono). nifanyeje na dalili zake zimeshaonekana kabisa.
Naomba ushauri wa tiba na kama ni sahihi kama nikimwacha.

...nendeni pamoja mkapatiwe tiba na ushauri nasaha. Ajali kazini tu hiyo mjomba, msamehe.
 
Duuu sio mchezo...Alfu mtoa hii topic anaonekana kama mtoto hivi....Hivi mtu mzima na akili zako huwezi kuja hapa ukauliza swali kama hilo wewe unaona mpenzi wako kakuambukiza hilo gonjwa alafu bado unauliza kama umuache au vipi lol........wewe mpige chini wanawake wengi sana wala usikate tamaa mkuu!!!

Then nenda kwa doctor maa moja akakusaidie!!
 
Buraza umevuna ulichopanda..kila siku mnaimbiwa msijamiiane kabla ya ndoa na kabla ya ndoa mpime afya zenu, mnaziba pamba masikioni. Sasa hapo ulipo angalia umeshafulia, wahi mapema ukajikabidhi kwa watabibu wakucheki barometer zinasemaje kuhusu ngwengwe, maana duh, ina maana wadau wamekusaidia bila kiatu kwenye uwanja wenye mbigiri.

NB: Pole mdau ndo maisha hayo.
 
Pole sna ni vizuri kumpeleka kwa daktari akatibiwe na nasikia kwa sie wanawake inachukua muda sna kupona hivyo hakikisha anatibiwa vizuri na mshauri anywe maji mengi na kupima kizazi km kimeathirika.....!

By the way inaelekea ni mchafu fulani hivi pole kaka!
 
...nendeni pamoja mkapatiwe tiba na ushauri nasaha. Ajali kazini tu hiyo mjomba, msamehe.

Mkuu Mbu, Mapenzi yasiyokuwa na uaminifu kati ya wapendanao siku zote hayadumu. Badala ya huyu kijana kupoteza muda wake na huyu binti ambaye si mwaminifu na anaweza tena kurudia alichokifanya ni bora tu aingie mitini na kuanza kutatafuta upya.
 
Inawezekana ameshikwa sana ndo maana anjiuliza mara mbili mbili kuwa amuache au la, by the way WE ARE hiaTO ADVICE BUT YOUR THE one WHO CAN MAKE DECISION
 
Mkuu Mbu, Mapenzi yasiyokuwa na uaminifu kati ya wapendanao siku zote hayadumu. Badala ya huyu kijana kupoteza muda wake na huyu binti ambaye si mwaminifu na anaweza tena kurudia alichokifanya ni bora tu aingie mitini na kuanza kutatafuta upya.

Naomba kutofautiana na wachangiaji wengine waliotangulia. Kwa vile huyu jamaa kaja kuomba ushauri, ina maana bado anampenda mpenzi wake. Ingawa hajasema mengi, lakini inawezekana huyo dada aliambukizwa kabla hawajawa marafiki. Kwa maana hiyo siyo sahihi kusema kuwa huyo msichana ni mhuni. Labda alikutana na ex-wake mara moja akaambukizwa. Let's give her a benefit of doubt.

Nashauri jamaa ampeleke mpenzi wake kwa dokta wapime vizuri, wapate maibabu sahihi ili waendelee kufaidi penzi lao. Kumpiga chini siyo suluhu. Anaweza kukumbia miiba akaangukia kwenye upupu. Ila kama atauchukua ushauri wangu basi ajipe muda zaidi kabla ya kwenda kwa pilato kujitia kitanzi, kwani inawezekana mbia wake kweli hajatulia! Ukiwa mtumba na ukanunua mtumba basi ukubali harufu yake hata kama haipendezi!!!
 
Tupo ukurasa mmoja kabisa Dark City!

Kwanza hapa huyu jamaa hajaeleza kabisa kama kabla ya kuwa na huyu demu yeye mwenyewe alikuwa na uhusiano na mtu mwingine au la! kama alikuwa na uhusiano na mtu mwingine kuna uwezekano mkubwa kwamba hiyo kitu yeye ndo originator na demu anamsingizia tu, kwani ni kitu gani kinamdhibitishia kuwa demu wake kamuambukiza in case yeye mwenyewe alishakuwa na kicheche kingine before?

Pili, kama ulivosema DC, inawezakana huyo demu kaambukizwa kabla ya kuwa na uhusiano na huyu mshikaji.....so wan't be fair to just damp her kwa sababu kaleta Kisonono......jiulize na wewe mwenyewe, ungekuwa wewe ndo mleta Kisonono huko kny mahusiano yenu na demu unampenda ungejisikia na demu akikupiga chini? Kwanza in this case wote mna makosa, mlianzaje kuibanjua amri ya sita kavu kavu bila check up ya miili yenu?

Third, cha muhimu now nenda kacheki vizuri miili yenu kama inamaabukzo mengine as well, then wote pateni tiba ya hiyo kitu.....then sahauni yaliyopita na anzeni life jipya mkiahidiana kuwa waaminifu!
 
Cha kufanya mchukue mwende naye kama upo Dar mpeleke pale Makao makuu ya Polisi Central kwa pembeni kuna dispensary pale wanatibu magonjwa ya zinaa.
Mkisha jitibia muulize kalitoa wapi hili gonjwa?
 
Jamani wadau nisaidieni ushauri mpenzi wangu(wife to be) ameniambukiza gonorrhea(kisonono). nifanyeje na dalili zake zimeshaonekana kabisa.
Naomba ushauri wa tiba na kama ni sahihi kama nikimwacha.

Nenda pale infectious diseases testing centre pale mjini(DSM) watawapa matibabu bila shida. Tena mngepima na ngoma kabisa. Mkiwa mpo fit fanyeni mikakati ya pamoja ya kuwa waaminifu ktk mahusiano yenu. Endeleeni na maisha kwa amani!
 
mzee demu kama huyo hafai,kama vipi we mpige kibuti then tulia utafakari kabla ya kutafuta mamsapu mwingine
 
Wewe mwenyewe hujatulia, mtu unabadilisha wanawake kama nguo; una uhakika gani kwamba huyu ndiye aliyekuambukiza? Kabla hujamtaka mwenzio kuwa mwaminifu kwako anza wewe. Kama una uhakika 100% kuwa hujakukuruka kwingine, basi msahau huyu wala huhitaji kuomba ushauri.
 
Cha kufanya mchukue mwende naye kama upo Dar mpeleke pale Makao makuu ya Polisi Central kwa pembeni kuna dispensary pale wanatibu magonjwa ya zinaa.
Mkisha jitibia muulize kalitoa wapi hili gonjwa?

Kwa nini amuulize demu kalitoa wapi badala ya kujiuliza mwenyewe kalitoa wapi? Inawezekana dada wa watu anakuwa muhanga wa unyanyapaa wa kijinsia. Yeyote anaweza kuwa ni chanzo cha huo ugonjwa. Kama wanadhani biashara yao bado ni imara watibu majeraha na kusonga mbele. Yeyote kati yao akisema lilikotoka itakuwaje?
 
Back
Top Bottom