Mchumba wangu kaanza katabia cha ajabu

Tehe tehe mshukuru Mungu hujaoa bado. Fikiria ungekuwa ushaoa halafu ndo unafanyiwa hivyo. Mwambie unasitisha huo mpango wa kuoa atanyooka tu
 

Atakuwa amewaza mengi uliyomfanyia, akafikia point ya kusema una mdharau sasa anarudisha heshima yake. Umeshiriki nae kutoa hizo mimba 3, watoto wake watatu wamekufa mikononi mwako ukijua kabisa. Bado makosa unayofanya hutambui kama makosa unamhamishia yeye. Unamuona mjinga na poyoyo mwenzio, analiona hilo. Unadhani ulipokuwa unamgeuzia kesi alikuwa hajui? Alijinyenyekeza ili matatizo yaishe lkn unaonekana kwa akili yako ya kitoto uliamini unashindana eti ukashinda.
Tulia nae sehemu na umuulize na umuombe msamaha, anaweza kuwa alikuwa haongei lkn ana mengi moyoni mwake hasa uliyomuumiza nayo.
Tengenezeni wenyewe na mtengeneze na Mungu ili muwe na ndoa ya furaha.
Mwanamke huwa hacharuki bila sababu hasa kwa tabia uliyomuelezea huyo mpenzi wako.
 
Ngoja nkuambie rafiki yangu.ulivoenda kuposa akapata confidence ya umilikia halali (japo suo kwa ndoa).hiyo ikamdhihirishia kuwa uko serious....that means aka-create ownership...yani ukawa wake haswaaa.so wala si mabadiliko ila analinda kilichochake......pole ila jitahidi kumfahamu mwenzako vizuri.
 
Miaka 9 duh si mshamaliza styles zote?!

Wakifunga ndoa na hanemuni wataenda!!

mzaramo mahusiano sio kushindana ni vyema kutumia busara zaidi kuliko hivyo unavyofanya. mambo ya kuwa kwenye Kabila lenu eti wanaume ndio mko hivyo.., hayo yanepitwa na wakati! Ni vyema kuendeleza yake yenye faida ktk mahusiano na kuyaweka pembene yake yanayomkandamiza mwanamke!!

Ila pole kwa kushindwa kwa mara 3 mfululizo!
 
Last edited by a moderator:
Tehe tehe mshukuru Mungu hujaoa bado. Fikiria ungekuwa ushaoa halafu ndo unafanyiwa hivyo. Mwambie unasitisha huo mpango wa kuoa atanyooka tu

aiseee kama angefanya hivi nikiwa nishamlipia hela kwao nisingekubali na muda huu ndugu na jamaa wangekuwa busy kuja kuniwekea dhamana police
 

mkuu nimejitaidi mno kujishusha kwake hasa kwa kipindi hiki ili mambo ya mahari yapite maana kwa uhusiano wetu ulivyo kwa sasa kupeleka barua mahari kwao bila kusawazisha itakuwa sio sawa...ila nachukua ushauri wako mkuu ngoja nimuombe msamaha tu ili yaishe maana yakishindikana itakuwa aibu kubwa kwangu
 

aiseee kumbe wasichana wapo namna hiyo daaah...huyu bibie amejua kuninyoosha haswa
 

Nashukuru mkuu ila unadhani nitaweza kuwa namshinda tena kama zamani kweli?!
 
Last edited by a moderator:
napata picha mtu aniandae halafu atoweke gafla kisa simu duu mi ningekushika huondoki,

una mke mvumilivu sana
 

Fanya hivyo mkuu, utaona anabadilika. Wanawake hasa wasio ongea sana wanaweka mambo moyoni sasa ikifika mahali yanamuumiza akiyawaza anatolea hasira hata kwa mambo madogo na ya kufikirika. Inawezekana uliposema umemshinda alikuwa na ushahidi ili akaacha tu, jishushe kweli maana amekuvumilia sana huyo.
 
Kama hana kushinda inamaanisha huwa anakukamata kwenye ukweli siunajua ukweli upunguza nguvu muongo
 
ukiachana nae na kumalizana nae jmwa kila kitu tuwasiliane nikupe dawa ya stress
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…