Mchumba wangu ananishirikisha katika kila kitu cha maendeleo anachofanya

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,537
4,517
Mshaurini huyu jamani...

MCHUMBA WANGU ANANISHIRIKISHA KATIKA KILA KITU CHA MAENDELEO ANACHOFANYA!

Mimi ni binti wa miaka 28, sijaolewa ila nina mchumba ambaye yeye ana miaka 30, nampenda sana na yeye anaonyesha kunipenda kwakuwa kashanitambulisha mpaka kwao na kwetu pia nimeshamtambulisha. Tatizo ni kuwa mpenzi wangu huwa ni muwazi sana, ananishirikisha katika kila kitu chake cha maendeleo anachokifanya na mara nyingi anakuwa anataka mawazo yangu, akitaka kununua kiwanja, kujenga, akitaka kitu chochote hata kama ni mapazia anataka tufanye pamoja.

Mimi nafanya kazi na yeye pia anafanya kazi, haniombi pesa na wala hajawahi lakini tatizo ni kuwa kwakuwa ananishirikisha katika mambo yake basi nashindwa kumuomba pesa kubwa kubwa kwaajili ya kufanya mambo yangu kwani kila hela yake najua imeenda wapi? Kwa mfano labda nataka laki mbili, ninataka kununua kitu changu labda kutoka na marafiki, nikimuambia pesa ananiambia hana si tumenunulia kitu flani, ukiangalia kweli alinunua hicho kitui na alinishirikisha hivyo naona aibu hata kumkasirikia kwani kinakuwa cha maendeleo na najua pesa yake yote.

Naumia sana kwani mimi kama msichana nahitaji kudekezwa na kufanyiwa suprize za zawadi kama marafiki zangu ambao wanaweza kufanyiwa birthday na wapenzi wao, kutolewa out, kununuliwa nguo na zawadi. Mimi nikihitaji kitu inabidi nimuambie mapema kabla ya mshahara ili aniweke kwenye bajeti na sanasana atakupa elfu hamsini hata laki hakupi kwani anakuwa anafanya vitu vingi vya maendeleo ambavyo ananiomba ushauri na ukiangalia anakuwa kweli hana kwani hata yeye hafanyi hizo starehe

Kinachoniuma zaidi ni kuwa hawezi kufanya maamuzi yake mwenyewe kama mwanaume ni lazima aniambie na mara nyingi hupenda kufuata ushauri wangu na si wake. Kunipenda kweli ananipenda lakini nina wasiwasi je tukioana itakuaje kwani mara nyingi anasema tukioana itakua vizuri kama tukishirikiana kwenye mambo ya familia eti mshahara wangu nao tufanyie mambo ya maendeleo wakati yeye kama mwanaume anatakiwa kufanya kila kitu, niko njia panda nawaza je huyu ni mtu sahihi kwangu au nifanyeje?
 
Huyo sio mtu sahihi kwake! Ampige chini akatafute mwanaume anayejua kuspend, kumbebisha! Kumtoa out na kila aina ya starehe

Nasema hivyo kwasababu ndege wanaofanana huruka pamoja! Huyu jamaa akili zake ni za maendeleo wakati huyu dada yeye anataka starehe, outing, kuletewa zawadi! Kupewa hela wakati ana mshahara! Bora amuache huyo bro naamini atapata mtu wa type yake!
 
Hapo wadada ndo mnapofeli kumchagua mchumba sahihi, unapenda malimbukeni wakuchezee, wakupe suprise, wakutoe out na mengine. Hivi kwa umri wako bado unawaza suprise, umepata mtu anayeona mbele anakushirikisha kwa kila kitu wewe unaona sio sahihi duuuu, zingatia umri wako pia.

Kwa ushauri wangu huyu ni mwanaume sahihi kwako anayependa kukusiliza kwa ushauri na akatekeleza ila wewe sioni kama ni mke sahihi sana kama bado unadought action zake.
 
Hapo wadada ndo mnapofeli kumchagua mchumba sahihi, unapenda malimbukeni wakuchezee, wakupe suprise, wakutoe out,na mengine. Hivi kwa umri wako bado unawaza suprise, umepata mtu anayeona mbele anakushirikisha kwa kila kitu wewe unaona dio sahihi duuuu, zingatia umri wako pia.
Kwa ushauri wangu huyu ni mwanaume sahihi kwako anayependa kukusiliza kwa ushauri na akatekeleza ila wewe sioni kama ni mke sahihi sana kama bado unadought action zake.
Halafu utakuta wanawake wenzie wanamjaza ujinga
 
Mshaurini huyu jamani...

MCHUMBA WANGU ANANISHIRIKISHA KATIKA KILA KITU CHA MAENDELEO ANACHOFANYA!

Mimi ni binti wa miaka 28, sijaolewa ila nina mchumba ambaye yeye ana miaka 30, nampenda sana na yeye anaonyesha kunipenda kwakua kashanitambulisha mpaka kwao na kwetu pia nimeshamtambulisha. Tatizo nikua mpenzi wangu huwa ni muwazi sana, ananishirikisha katika kila kitu chake cha maendeleo anachokifanya na mara nyingi anakua anataka mawazo yangu, akitaka kununua kiwanja, kujenga, akitaka kitu chochote hata kama ni mapazia anataka tufanye pamoja.

Mimi nafanya kazi nayeye pia anafanya kazi, haniombi pesa na wala hajawahi lakini tatizo nikua kwakua ananishirikisha katika mambo yake basi nashindwa kumuomba pesa kubwa kubwa kwaajili ya kufanya mambo yangu kwani kila hela yake najua imeenda wapi? Kwa mfano labda nataka laki mbili ninataka kununua kitu changu labda kutoka na marafiki, nikimumba pesa ananiambia hana si tumenunulia kitu flani, ukiangalia kweli alinunua hicho kitui na alinishirikisha hivyo naona aibu hata kumkasirikia kwani kinakua cha maendeleo na najua pesa yake yote.

Naumia sana kwani mimi kama msichana nahitaji kudekezwa na kufanyiwa suprize za zawadi kama marafiki zangu ambao wanaweza kufanyiwa birthday na wapenzi wao, kutolewa out, kununuliwa nguo na zawadi. Mimi nikihitraji kitu inabidi nimuambie mapema kabla ya mshahaara ili aniweke kwenye bajeti na sanasana atakupa elfu hamsini hata laki hakupi kwani anakua anafanya vitu vingi vya maendeleo ambavyo ananiomba ushauri na ukiangalia anakua kweli hana kwani hata yeye hafanyi hizo starehe.

Kinachoniuma zaidi nikua hawezi kufanya maamuzi yake mwenyewe kama mwanaume ni lazima aniambie na mara nyingi hupenda kufuata ushauri wangu na si wake. Kunipenda kweli ananipenda lakini nina wasiwasi je tukiona itakuaje kwani mara nyingi anasema tukioana itakua vizuri kama tukishirikiana kwenye mambo ya familia eti mshahara wangu nao tufanyie mambo ya maendeleo wakati yeye kama mwanaume anatakiwa kufanya kila kitu, niko njia panda na waza je huyu ni mtu sahihi kwangu au nifanyeje?
Achana nae huyo, hana maajabu njoo kwenye ulimwengu mpya wa surprise
 
MIMI NILIVYOMUELEWA JAMAA...KAFUNGA MLANGO WA KUOMBWA OMBWA HELA BILA BUDGET...SIO KWAMBA ANAMSHIRIKISHA KILA KITU, HAPANA! NI ILE TU BIBIE AJISHTUKIE MWENYEWE KABLA HAJAOMBA HELA YOYOTE...AKIAMINI WAZI ANAJUA MATUMIZI YOTE YA PESA YA MCHUMBA WAKE...

AACHE TAMAA TU, YEYE SI ANAFANYA KAZI PIA ATUMIE HELA YAKE NA AMSAIDIE MUMEWE MAENDELEO...

JAMAA AMEFANIKIWA SANA KUZUIA VIZINGA...
 
Back
Top Bottom