Mchumba wa kukodi

ugaibuni

Member
Jan 5, 2012
15
9
Mwaka mpya wa kichina ndio huo umekaribia, katika jamii ya Wachina kila mchina kwa kadri awezavyo anatakiwa kurudi nyumbani kwake. Katika jamii hii ya Wachina wazazi hujisikia sifa na kumkweza mtoto wao pindi anaporudi nyumbani akiwa na mchumba yake haswaa kama anavutia, ana hela nk.
Kitu ambacho ni nadra kwa jamii yetu ya Tanzania, leo katika pitapita zangu mitandaoni nikakutana na matangazo(haswaa kwenye mitandao ya Groupon) yanayotoa punguzo na offer kwa kukodi mchumba wa kurudi naye nyumbani.


Katika jamii ya Wachina, kukodisha mchumba si jambo la hatari kwakuwa wengi wao wanaendeshwa kwa kuuza sura(jinsi watu wanavyokudhani). Nimewahi kuuona mkataba wa uchumba wa kukodi, mkataba huo humtaka muhusika kuzuga kadri awezavyo ili wazazi au marafiki wasijue kinachoendelea, ila hawaruhusiwi kuwa na mahusiano yoyote ya kimapenzi, pia wakiwa ndani ya mkataba mkodiwa anatakiwa kufuata amri za bosi wake, kinyume chake kitapeleka kutolipwa mafao.

Je unalionaje hili suala la kukodisha boyfriend au Girlfriend ili kukupa company kwa mtazamo wa kikwetukwetu, pia nyumbani huduma hii inapatikana?

Souce: Ughaibuni.com
 
Inaonekana umeipenda sana hii eeh?? mbona hata Tanzania wapo?? nenda pale kona bar, Q bar, Chole street wapo kila siku kuanzia saa moja..kule nako ni kukodi na dalili njema za ujasiriamali..
 
Sio China tu, hata mimi niliwahi kuifanya hapo Bongo. Nilikuwa natafuta nyumba ya kupanga, Baba mwenye nyumba akasema anataka mtu mwenye mume/mke. Nikawasimulia vijana wa mujini, wakasema hiyo sio issue, nitakafutiwa mwenza wa kukodi na nyumba nikapata kwa muda wa miezi sita niliyokuwa katika majukumu eneo hilo, ila aliishia kuwa wa kukodi kwa shughuli hiyo maana baada ya kupata nyumba kila mmoja alibaki na hamsini zake na Ba' Mwenye nyumba hakufuatilia kuniulizia kuhusu mwenza.
 
Back
Top Bottom