Kwa sasa hatuishi wote maana tuko kwenye michakato ya ndoa lakini mara kadhaa anakuja na kukaa siku mbili tatu.
Kusema ukweli mimi nafanya almost vitu vyote, kwa mfano nina uhakika hajawahi kuosha vyombo!! Tukishakula(hata kama ni chips) ataacha sahani chafu mezani na kukaa sebuleni moviez. Either mimi nitoe na kupeleka kwenye sink au na mimi niache.
Mara nyingi napenda kukaa zangu chumbani au kwenye computer tu maana ananikera.
Mwambia ukweli vitu vinavyokukera kabla hamjaingia kwenye ndoa
Ili ajue kama yuko tayari
Naomba ushauri wenu. Nina mchumba wangu tumekaa muda mrefu kama miaka 5 hivi. Sasa tumeona ni muda muafaka wa kuoana. Kipindi kirefu cha uhusiano wetu hatukuwa tunaishi pamoja as yeye alikuwa anasoma mkoa mwingine nami mwingine. Lakini hii haikupunguza mapenzi yetu maana tulikuwa tunawasiliana na kutembeleana mara kwa mara.
Sasa alimaliza chuo na kuanza kazi, na mimi pia nina kwangu. Tukawa tuko close zaidi na siku moja moja tunakaa pamoja nyumbani. Hili kufanya mambo yaende kwa heshima, tukafikia hatua ya kutambulishana kwa wazazi rasmi na kuanza kujipanga kwa ajili ya mahari na ndoa
Kuna tabia ambazo nimezigundua zinanikera na ninaomba ushauri.
1. Huyu binti ni mvivu
Anapenda kukaa kuangalia moviez tu. Moviez, kuchat thats it. Nyumba chafu nasafisha mwenyewe. Kila kitu kipo ndani(jiko, chakula), hataki kupika eti mpaka awe kwenye mood kwahiyo tunaishia kula chips. Nguo zangu chafu(hata za kwake) kufua ugomvi.
2. Kisirani
Mtu wa visirani, kujibu, kununa.
Sasa tunaelekea kwenye mahari lakini kichwa changu kinawaka moto. Hivi tu kwenye ndoa bado, tukiwa ndani ya ndoa si itakuwa balaa?
Mimi pia nina mapungufu yangu kama vile ni mkali sana, pia nina maneno ya kukejeli(wengine wanasema dharau), but mara nyingi nakuwa open sana sio mtu wa kuficha ficha.
Je nifanyeje? Binti nampenda, napenda niishi nae ila kwa style hii nyumba si itawaka moto?!
Ushauri
Nitamwambia(na anafahamu maana nilishamwambia). Akionekana kutobadilika itabidi nifanye maamuzi magumu
kaa naye mwambie mwanzo hadi mwisho ajue wajibu wake ikiwezekana wasiliana na mama yake amkalishe chini amwonye au amfunde asijekuwa mzigo kwa baadaye ndo hawa ambao huwaachia wasichana wa kazi kufua hadi nguo za ndani pole kaka yangu mi na ushahidi wa watu ambao mpaka anaingia chuo hajui kupika wengine wako rafu wavivu hadi nashangaa nasema wanaume wa na kazi kwa kuchagua wa chumba ndo hivyo usione ua lachanua kwa nje tu hasa wakina dada wa leo tena wale waliosoma ndo balaa wavivu hakuna. jamani wadada hawa wanakera tena sana
ndio hizi nyumba unaingia unashindwa hata kuomba maji ya kunywa. Yaani ukiomba glass inatolewa kwenye kabati bila kufutwa wala nini, alafu ukute haikuoshwa vizuri, glass ukiisogeza kinywani inatoa harufu ya mayai mabichi.....mbona kiu itakuishia au utatapika kabisa.
mleta mada, nakushauri umuepuke huyo binti, especially unaonekana unakerwa sana na uchafu na uvivu. sasa ivi unaweza mvumilia sababu mapenzi bado motomoto, but trust me, marriage is more than that
Nakula bia sasa hapa nikitafakari ushauri ila am pissed off
Badili Tabia huyo mdada anachojua ni kufanyiwa ukaguzi tu
Badili Tabia huyo mdada anachojua ni kufanyiwa ukaguzi tu