Mchumba mwizi wa nguo za watu

project planner

JF-Expert Member
Jul 8, 2019
1,166
1,532
Wakuu natuamaini hamjambo na mnaendelea vizuri kwenye ujenzi wa nchi niende moja kwa moja kwenye mada. Nina mchumba ambaye natarajia kumuoa mwezi wa kwanza na uchumba wetu unakaribia miezi mitatu sasa

Shida huyu binti niliye naye ana tabia ya kuiba nguo za watu haswa akienda kwa ndugu zake anaiba nguo za majirani wa hapo wakizianika na za ndugu zake na ukiangalia ana nguo nyingi sana tu na kila wikiendi nampa elfu hamsini ya kununulia mavazi ila bado ni mwizi wa nguo za watu.

Mnanishauri nifanyaje? Je atafaa kuoa huyu au ndio naingia mkenge? Msaada wenu mlio kwenye ndoa tafadhali maana ananipenda nami nampenda ila hii tabia ni kero kwangu
 
Anaiba halafu anavaa?
Maradhi ni mengi, kuvaa nguo ya mtu sio salama kwa afya.
Ongea nae kuhusu hiyo tabia ikishindikana piga chini.
 
Aisee wanasema ndege wafananao huruka pamoja, unahisi si kweli? Huwa anakusimulia kwamba anaiba hizo nguo?, ama wewe umejuaje kuhusu huo udokozi?

Yupo under 18yrs?acha kutembea na watoto mkuu
 
Aisee wanasema ndege wafananao huruka pamoja, unahisi si kweli? Huwa anakusimulia kwamba anaiba hizo nguo?, ama wewe umejuaje kuhusu huo udokozi?

Yupo under 18yrs?acha kutembea na watoto mkuu
Nimesimuliwa na mama zake wadogo na dada zake na si under 18 Ni binti wa miaka 20
 
Nimeishia hapo kuwa Kila wiki una mpa 50000 ya kununua nguo.
Ngoja nikakojoe nilale
Tangu nimejua hii tabia ya kuibia watu nguo nikadhani Wenda binti Hana nguo za kutosha nikaanza kumpa Kila wiki hamsini ili anunue nguo anazotaka Cha ajabu Tena Jana kaiba nguo za watu Tena
 
Kuna wakati hua najaribu kitafakari sana hizi mada ambazo kwangu naona kama hazina haja ya kuomba ushauri, na badalayake it's just the matter of your own decision...
 
Back
Top Bottom