Kwa wasioijua mbata, ni kofi zito la mkono uliokunjuliwa na vidole kunyooshwa huku mkono ukiwa umekazwa, mara ya mwisho kupigwa mbata ilikuwa kidato cha pili miaka zaidi ya 20 iliyopita.
Ilikuwa siku mwalimu wa kiswahili anafundisha mimi nikalala, nikashitukia tu mbata inashuka mgongoni, nikajikuta nasimama ghafla na usingizi kukata kabisa.
Nimejijengea tabia ya kutaniana na mchumba, jana nikatoa utani wa kweli kumbe umemuuma, ile nimemgeuzia kisogo nikasikia mbata inarindima mgongoni, nimebaki najiuliza kosa langu ni kuzoeana na huyu mchumba au? kwamba kanizoea kiasi cha kuingiza dharau au? hii inamaanisha wanawake hawahitaji kuwazoea maana ipo siku watakutia kidole jichoni au?
Maswali ni mengi, nipeni a way forward wakuu.