Mchumba kanipiga mbata wapendwa

Mchumba kanipiga mbata wapendwa

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,966
Kwa wasioijua mbata, ni kofi zito la mkono uliokunjuliwa na vidole kunyooshwa huku mkono ukiwa umekazwa, mara ya mwisho kupigwa mbata ilikuwa kidato cha pili miaka zaidi ya 20 iliyopita.

Ilikuwa siku mwalimu wa kiswahili anafundisha mimi nikalala, nikashitukia tu mbata inashuka mgongoni, nikajikuta nasimama ghafla na usingizi kukata kabisa.

Nimejijengea tabia ya kutaniana na mchumba, jana nikatoa utani wa kweli kumbe umemuuma, ile nimemgeuzia kisogo nikasikia mbata inarindima mgongoni, nimebaki najiuliza kosa langu ni kuzoeana na huyu mchumba au? kwamba kanizoea kiasi cha kuingiza dharau au? hii inamaanisha wanawake hawahitaji kuwazoea maana ipo siku watakutia kidole jichoni au?

Maswali ni mengi, nipeni a way forward wakuu.
 
Mada zingine...naona malupe lupe kabisa .....hivi hii nayo ni thread hapa JF?
Mods mnaua bendi.
 
siku nyingine ukimuudhi ukimpa kisogo atakuchoma kisu
 
huyo mkeo hana kiasi, na kuna siku mtagombana chanzo kikiwa ni utani tu. Punguza kabisa utani naye
 
kwani wewe ni me au ke? just to start with maana hapo kuna different approaches. ila pole sana kwa kupigwa mbata
 
Kupigwa mbata hakumaanishi kudharauliwa mkuu.. Kunamaanisha umegusa a wrong button na kupata adhabu stahili (from huyo aliekupiga kibao's perspective).. Cha kujifunza hapo ni kwamba mchumba ulienae ni aggressive type.. So kama utakubaliana aina hiyo ya maisha (kula mbata kila ukimkwaza) basi endeleeni na maisha yenu.. Usimuambie hata rafiki yako maana watatangaza..

NB: Mwambie asiwe anakupiga mbata mbele za watu.. Atakuaibisha bure.. Hata ukimkosea hadharani akusubiri mkiwa wawili tu ndo akukong'ote mbata..
 
Anza kudhibiti hiyo tabia mapema, I mean tafuta dawa yake mapema sana kabla ya kupiga hatua ya pili mbele..huo ni uchumba tu je ukimuoa? c ndo atakukalia mdomoni?
 
Na wewe ungemuonjesha mbata lako ili ajue maumivu yake asingerudia siku nyengne
 
Kama ulijua utani utamuuma kwa nin umtanie asee mengine mnataka wenyewe na angekubamiza na kofi lingine la shavu
 
Back
Top Bottom