Mchumba hauguzwi

Mchumba hauguzwi

Kwani ni wanaume wangapi wanafanyiwa fadhila nyingi na wanawake zao kwenye mahusiano na bado hao wanaume wanawaacha hao wanawake mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu haya mambo wakifanyiwa wanawake mnaona ni kawaida ila mkifanyiwa wanaume mnaona ni uonevu
Mzee wa counterargument za utetezi ningeshangaa sana kama usingetokea kwenye huu Uzi.
 
Umesahau kitu kingine kwenye kile kikao chetu mkuu!,ni marufuku kulipa mahari zaidi ya Laki 4 narudia tena Laki 4,hata Kama ukiambiwa utoe milioni 10
Kama tulivyokubaliana kwenye kikao chetu, kuwa ni maeufuku kumsomesha mchumba wako. Hili tulishalifunga na atakae tuletea malalamiko tutampiga kwenzi kuu, ndio tunampa ushauri.

Sambamba na hilo, niongezee kuwa ni marufuku kumuuguza mchumba wako. Hapa nazungumzia matatizo makubwa ynayoghalimu muda na Pesa za kutosha.

Baadhi ya magonjwa hayo ni, kisukari, kifafa, ugumba, miscarriage za Mara kwa Mara, moyo, figo na matatizo mengine sawa na hayo. Mwanamke ukimsaidia na kupona, dharau huwa kubwa sana na hata ndugu wanaweza kukuuliza, "unataka urudishiwe kiasi gani ili uachane nae".

Muuguze yule tu unayeishi nae kama hujamuoa achana nae.

*********** ushuhuda *********

Kuna jamaa anaitwa Steve, huyu bwana alikutana na demu mkali (Beth). Tatizo la huyo demu alikuwa na matatizo ya kukamaa mfano wa kifafa. Ndugu walihangaika wakachemka, wakakata tamaa.

Baada ya muda jamaa akajitosa. Akaanza kumhangaikia na demu akaenda kuponea kilolo ndani ndani huko. Jamaa ilimghalimu kama kilo 9 hivi, baada ya demu kupona ndugu wakampa ruhusa ya kuishi nae.

Mwaka mmoja mbele (mwaka huu), binti akawa hakamatiki. Madoni ya mji yaliyomdharau yakaanza kumfukuzia by hook and crook. Demu akaanza dharau, pia kutokana na jamaa kuunga unga tu life ikabidi asalimu amri.

Nilikaa nae muda mrefu na kumpa ushauri uliomsaidia sana. Maana jamaa alishaanza kupiga hesabu tu ya namna ya kuacha kuvuta oxygen. Lakini demu kuonesha kuwa hamtaki jamaa alikunywa mpaka sumu kuwaahinikiza ndugu zake wamtoe kwa jamaa.

Niishie tu hapo lakini, ole wake atakae muuguza mchumba!!!!!!!!!!.
 
MTOA UZI CHUKUA BALIMI ntalipa.. PITIA HAPA KIGAMBONI..
 
Mimi sikubaliani na wewe mleta mada! Hicho kikao ulikaa mwenyewe! Usitegemee fadhila baada ya kumsaidia MTU. Kama ni wako, wako tu.

Hata kama hukumsadia ipo siku atakuwacha kama sio wako. Upendo haubagui
 
Mimi sikubaliani na wewe mleta mada! Hicho kikao ulikaa mwenyewe! Usitegemee fadhila baada ya kumsaidia MTU. Kama ni wako, wako tu.

Hata kama hukumsadia ipo siku atakuwacha kama sio wako. Upendo haubagui
UKIKUA UTAMUELEWA MLETA UZI..
OVER
 
Kwahiyo wewe unataka afe? Ili upate faida gani kwani akipona mkaachana shida iko wapi wewe unajua atakayekufaa?
 
Kwani ni wanaume wangapi wanafanyiwa fadhila nyingi na wanawake zao kwenye mahusiano na bado hao wanaume wanawaacha hao wanawake mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu haya mambo wakifanyiwa wanawake mnaona ni kawaida ila mkifanyiwa wanaume mnaona ni uonevu
Watanyooka tu na magu anavyokaza kila kitu kitakaa kwenye mstari lazima mkuki ugeuki nyuma
 
Back
Top Bottom