Mchumba hauguzwi

Mchumba hauguzwi

Vitalis Msungwite

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2014
Posts
3,313
Reaction score
7,962
Kama tulivyokubaliana kwenye kikao chetu, kuwa ni maeufuku kumsomesha mchumba wako. Hili tulishalifunga na atakae tuletea malalamiko tutampiga kwenzi kuu, ndio tunampa ushauri.

Sambamba na hilo, niongezee kuwa ni marufuku kumuuguza mchumba wako. Hapa nazungumzia matatizo makubwa ynayoghalimu muda na Pesa za kutosha.

Baadhi ya magonjwa hayo ni, kisukari, kifafa, ugumba, miscarriage za Mara kwa Mara, moyo, figo na matatizo mengine sawa na hayo. Mwanamke ukimsaidia na kupona, dharau huwa kubwa sana na hata ndugu wanaweza kukuuliza, "unataka urudishiwe kiasi gani ili uachane nae".

Muuguze yule tu unayeishi nae kama hujamuoa achana nae.

*********** ushuhuda *********

Kuna jamaa anaitwa Steve, huyu bwana alikutana na demu mkali (Beth). Tatizo la huyo demu alikuwa na matatizo ya kukamaa mfano wa kifafa. Ndugu walihangaika wakachemka, wakakata tamaa.

Baada ya muda jamaa akajitosa. Akaanza kumhangaikia na demu akaenda kuponea kilolo ndani ndani huko. Jamaa ilimghalimu kama kilo 9 hivi, baada ya demu kupona ndugu wakampa ruhusa ya kuishi nae.

Mwaka mmoja mbele (mwaka huu), binti akawa hakamatiki. Madoni ya mji yaliyomdharau yakaanza kumfukuzia by hook and crook. Demu akaanza dharau, pia kutokana na jamaa kuunga unga tu life ikabidi asalimu amri.

Nilikaa nae muda mrefu na kumpa ushauri uliomsaidia sana. Maana jamaa alishaanza kupiga hesabu tu ya namna ya kuacha kuvuta oxygen. Lakini demu kuonesha kuwa hamtaki jamaa alikunywa mpaka sumu kuwaahinikiza ndugu zake wamtoe kwa jamaa.

Niishie tu hapo lakini, ole wake atakae muuguza mchumba!!!!!!!!!!.
 
Acha kuwafundisha wenzako roho mbaya..sio ubinadamu huo...nyie wenye kusaidia wagonjwa wasaidieni mana ndio mtamuona muumba..na hyo ndio dini nzuri....kikao cha wanawake kimeazimia watenda mazuri wote watauona uso wa bwna..lakin zaidi watakula mema ya nchi..
 
Hayo sio maisha mkuu Kikubwa ni kuangalia tu uelekeo wa huyo mwanamke wako toka mwanzo na ufanye maamuzi mapema kwamba umeona atakufaa kwenye shida na raha au haeleweki mwanamke huwa hawezi kujificha tabia yake
 
Hamna cha roho mbaya Jamaa anasema kweli haha. .mchumba hauguzwi
Acha kuwafundisha wenzako roho mbaya..sio ubinadamu huo...nyie wenye kusaidia wagonjwa wasaidieni mana ndio mtamuona muumba..na hyo ndio dini nzuri....kikao cha wanawake kimeazimia watenda mazuri wote watauona uso wa bwna..lakin zaidi watakula mema ya nchi..
 
Wenzio huwa wanachukulia advantage hiyo hiyo 'Ambayo wewe u-nahisi kuwa ni roho mbaya. ..

Mind you --mwenye huruma hana Bahati
Duu ukisikia dilema ndo hizi. Kama una point vile lakini pia kwa upande mwingine kama ni roho mbaya vile!!?
 
tenda wema nenda zako usingoje shukrani,kwani hiyo shukrani anayo mwenyezi mungu,utalipwa hapa kama sio hapa basi huko kuzimu
 
Kwa sisi ambao hatuitaji kuoa tena,huwa tunapiga mashine kisawasawa ndipo uweze kutumia garama zetu,hata ukiniacha inakuwa haina maumivu.
 
Kwani ni wanaume wangapi wanafanyiwa fadhila nyingi na wanawake zao kwenye mahusiano na bado hao wanaume wanawaacha hao wanawake mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu haya mambo wakifanyiwa wanawake mnaona ni kawaida ila mkifanyiwa wanaume mnaona ni uonevu
 
Back
Top Bottom