Mukulu wa Bakulu
JF-Expert Member
- Aug 12, 2014
- 4,050
- 12,966
Hongera, hicho ni kipaji,una uwezo mkubwa wa kufanya mambo mawili kwa wakati mmoja, ujenzi tumboni kwa mtu na ujenzi wa nyumba, hongera sana.
Nani alikwambia ukioa hauwezi kujenga? Wengi tumeoa hatuna hata viwanja lakini pamoja na wake zetu tumelea watoto, tumesomesha na tumejenga vile vile.
Nakwasababu umesema unataka ujenge inaonyesha una kipato fulani. Hivyo nakushauri upange nyumba, uoe na mlee mtoto. Mambo mengine yatakuja tu kwa juhudi na mipango yenu wote wawili.
Khaa!!! Nimesoma mara 100 sijaona hiyo changamoto unayoisema. kwani milikuwa mnakutana wapi? Au na yeye anakusaidia kuchimba msingi hivyo una wasiwasi akiwa na mimba nguvukazi inapungua? Nauliza tu :glasses-nerdy:Habari zenu wadau,
Mimi ni kijana mwenye umri wa miaka 24,ninamchumba wangu ana miaka 20 tunapendana sana lakini hivi majuzi ananiambia hajidikii vizuri na hajaona siku zake ambazo hua zinawahi lakini Leo ndio alitakiwa apate hedhi.
Anadai ana mimba yangu lakini changamoto inakuja kwamba Mimi naishi na wazazi na ndio nimeanza kuchimba msingi nijenge na nilimwambia asubiri nijenge niende kwao lakini sasa majukumu yamekua mawili nashindwa nifanyeje, nimwambie aende kwao ili nimalize ujenzi au nipange chumba nimuoe kabla mimba haijawa kubwa ujenzi usubiri.
Daah yaani hapa maana yake ni nini?
Kwamba jamaa huwa anagonga Tigoo?
Au mbegu zake hazizalishi:
Bomoa huo msingi mlee mimba kwanza
kumbukumbu LA torati 22:28
Nonsense!!!
Zile sheria zilikuja kabla ya kristo.kitambo sanawalipewa israelites!sasa nenda kwenye agano jipya unipe kifungu kinachohalalisha we kufanya mapenzi kabla ya ndoa..amri kumi alizotupa mungu mojawapo ni usizini!kua kijana!

hahahaaa!!! mambo mengine inabidi kucheka utadhani mazuri. Sasa ulimwambia asubiri lakini utamu mnapeana... ahahahaaa!!! kazi kweli kweli... komaa tu, jenga na ulezi pamoja...
Hayo ni matokeo baada ya kupanda, endelea kuvuna. Mbona hukushirikisha kama umelala nae bila kinga, tena mwezi mmoja tu uliopita. Hebu endelezeni familia, umeongeza idadi ya wababa Tanzania. Kapange mchukue kaeni pamoja, utajishangaa hata nyumba utaimaliza mapema maana huyo kakuletea Baraka!. Hongera sana Kijana!
Ha ha haa. . . .We kiboko asee
Habari zenu wadau,