Mchoraji wa nembo ya Taifa ahamishiwa Hospitali ya Muhimbili

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,266
DAqzjgXWsAAzpFC.jpg
Mzee Francis Maige maarufu Ngosha, aliyechora nembo ya Taifa ya Bwana na Bibi amehamishiwa Hospitali ya Muhimbili (MNH) akitokea Hospitali ya Amana alikokuwa amelazwa tangu jana (Jumatano)

Ngosha amehamishiwa hospitalini hapo baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamisi Kigwangalla kumtembelea leo asubuhi kumjulia hali.

Katika mazungumzo, Ngosha amesema alichora nembo hiyo akiwa na mwenzake Ali Pangani ambaye amefariki dunia.

"Nimetumwa nije kumuona mzee wetu aliyechora nembo ambayo ni utambulisho wa Mtanzania, tumemhamisha hapa na kumpeleka Muhimbili kwa matibabu zaidi", alisema Dk. Kigwangalla

Chanzo: Mwananchi
 
kwani huyu hakulipwa mafao yake ,nadhani apewe matibabu kama sera yetu ya afya kwa wazee na watoto (AFYA BURE) inavoelekeza . wazee wa umri wake ambao hawkufanya lolote wanatibiwaje . Hizi ni cheap popularity on social media politics. Sera iko wazi na ifuattwe

Unaweza kuongea hivyo ka kuwa huyu mzee sio mzazi wako na hii nembo ni rahisi sana kwako au mtu mwingine kutengeneza. Kumbuka wakati anaitengeneza hakulipwa hata senti moja kwa kuwa alijitolea.

Alianza na ya Tanganyika

upload_2017-5-25_11-17-9.jpeg

Wengine wakaiboresha iwe ya Tanzania

2000px-Coat_of_arms_of_Tanzania.svg.png
 
kwani huyu hakulipwa mafao yake ,nadhani apewe matibabu kama sera yetu ya afya kwa wazee na watoto (AFYA BURE) inavoelekeza . wazee wa umri wake ambao hawkufanya lolote wanatibiwaje . Hizi ni cheap popularity on social media politics. Sera iko wazi na ifuattwe
Kulipwa tu haitoshi.
 
Hii ndio picha halisi ya wazeee wangi walioitumikia nchi hii wanavyoishi kwa shida. Kwa kweli wazee wamesahaulika, hata sie tutasahaulika hivyo hivyo
 
Huyu mzee nikionana naye nitamuuliza kuhusu hili la kuweka mwanaume aliyevaa sketi kwenye nembo ya taifa na maana yake ni nini hasa.
Nakumbuka nikiwa primary ilinipa shida sana kutofautisha na pia kuniacha na maswali mengi

Hilo ni vazi la Lubega.. Nenda Dodoma, Kaskazini Na Kanda ya Ziwa ni vazi la asili.
 
Huyu mzee nikionana naye nitamuuliza kuhusu hili la kuweka mwanaume aliyevaa sketi kwenye nembo ya taifa na maana yake ni nini hasa.
Nakumbuka nikiwa primary ilinipa shida sana kutofautisha na pia kuniacha na maswali mengi

Hili suala hata mimi linanichanganya, kwani wanaume wa Tanzania tunavaa sketi? Au hiyo miaka ya uhuru walikuwa wanavaa magauni? Mbona Nyerere picha zake zote yupo smart na suruali yake amechomekea vizuri na shati limenyooka pasi..? Ngoja apone aje ajibu hizi lawama!
 
Back
Top Bottom