Amavubi
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 30,156
- 13,249
Mchoraji vibonzo wa Kenya Godfrey Mwapembwa ,aka Gado ameiambia BBC kwamba atalishtaki gazeti la The daily Nation nchini Kenya kuhusu kile alichokitaja kuwa kusimamishwa kwa kandarasi yake kinyume cha sheria.
Mwaka uliopita alienda likizo kufuatia kile alichosema ni kuingiliwa kwa kazi yake.
Alikuwa amechora kibonzo katika gazeti jingine kuhusu aliyekuwa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ambacho anasema hakikumuangazia vizuri.
Mhariri wake katika gazeti hilo alipendekeza kwamba apumzike kwa kuwa sio mfanyikazi kamili wa gazeti hilo lakini amepewa kandarasi ya kuchora vibonzo hadi mwezi Julai 2016.
Hata hivyo mwezi uliopita alipewa barua ya kumsimamisha kazi.
Gazeti hilo limesisitiza kuwa uamuzi huo wa kuachana uliafikiwa na pande zote mbili,lakini mchoraji huyo anaamini kwamba kufutwa kwake kulitokana na shinikizo za kisiasa akiongezea kuwa anaamini kwamba serikali ya Uhuru Kenyatta imekuwa haipendezwi na kazi.
Mwapembwa ni mchora vibonzo maarufu nchini Kenya ambaye huwachekesha wasomaji wengi kwa uchoroji wake.
Mtandao wake unaomtaja kuwa mchoraji vibonzo hodari wa kisiasa katika eneo la Mashariki na Afrika ya kati,anasema kuwa vibonzo vyake huangazia kila suala kutoka ugaidi,ukataji miti,ukimwi na ufisadi na vibonzo vyake vimekuwa vikizua mjadala mkubwa.