Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 1,815
- 4,550
Wakati Serikali ikianza kushusha moto kwa halmashauri 85 zilizokusanya mapato chini ya malengo, huko Rorya wenyewe ni kama wameukwepa mtego huo, baada ya kukusanya mapato kwa asilimia 100.
Katika makusanyo ya mwaka wa fedha 2021/22, halmashauri ya Rorya imeivunja rekodi yake ya miaka 14 tangu mwaka wa fedha 2007/08, ambapo haikuwahi kufikia lengo la makusanyo.
Kuzibwa kwa mianya ya upotevu wa mapato na kusimamia ulipaji wa madeni kwa wafanyabiashara, ni miongoni mwa sababu zilizotajwa kufikiwa kwa hatua hiyo. Pia, mikakati ya Mkuu wa wilaya hiyo, Juma Chikoka maarufu Mchopanga, kuanzisha vyanzo vipya vya mapato vimechangia pakubwa.
Mwananchi limemtafuta Mchopanga kuzungumzia hatua hiyo ya kuvunja rekodi ya miaka 14 kwenye ukusanyaji mapato, ambapo amesema uwepo wa mapato ni jambo moja, lakini kuyakusanya ni jambo lingine.