Mchiriku: Hisani Musical Club (Gari Kubwa)

TAARIFA!!! Aliekuwa mpiga kinanda wa Hisani Gari kubwa na baadae Tumaini Jabali aitwae Muddy Kadogo amefariki dunia. Kwenye album za Hisani Gari kubwa kuanzia ya kwanza hadi ya nne huyu mwamba ndio aliepiga kinanda.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
 
Alifariki lini tena huyu maana,miaka niliyomfahamu huyu jamaa tulihamia manzese kwa mfuga mbwa kutokea sinza,Hisani walikuwa wanapiga mziki wao Pale ccm uzuri na kiingilio,kipindi hicho tulikuwa tunavizia fungulia mbwa ndio tuingie
 
Naskia kuna wanamuziki wa mnanda vibaka ambao walikuwa wanalala barabarani magari yakisimama wanayapora siku hiyo huko Kibada Kigamboni dereva alisimamishwa lakini hakusimama akawagonga wote wakafa,jamaa akawaimbia huo wimbo wa Ajali ya Kibada

Hawakuwa wanamuziki bali walikuwa masela wa tandika Soweto ambao walikuwa ni marafiki sababu maskani ni zile zile ..hivyo vifo vyao vilishtua na kuacha majonzi
 
wanyamwezi family pande za tegeta. mpiga kinanda kamongo manjarino, alikuwa anapiga kinanda hata bendi ya jaguar. sasa hivi ni teja choka mbaya. anapiga debe stendi ya tgt kariakoo. muimbaji chipukizi dogo mau, naye ni teja na pia ni pusha pande za tgt. sheshi junior a k a kapita naye ni hivyo hivyo. fido au mafidonga a k a kola, naye aliingia kwenye ngada lakini kwa sasa ametoka. yupo smart. mpiga taiming wao anaitwa issa, au baba roja yupo smart sana, yeye ni kinyozi. mpiga misondo dogo hassani, sijui yuko wapi? mara ya mwisho nilimuona machimbo ya mawe boko magereza. mpiga misondo msaidizi babu idi, marehemu naye alikuwa mjangwa. muimbaji wao mansuri mtoto wa tgt kibaoni, sijui yuko wapi? aliyebakia kwny ramani ya muziki mpk sasa ni muimbaji wao nguli machupa. ingawa haimbi mnanda. bendi imekufa ingawa sometime wanajaribu jaribu kuirudisha kwenye ramani ya muziki. wanafanyaga show pande za tgt, mbweni, bunju, na haswa bagamoyo. kwa sasa bendi ipo chini ya usimamizi wa ramso wa malaga na wadau wawili watatu. kilichoua muziki huu ni usela mavi. mnanda na uhalifu ni kulwa na doto. ukumbi wa silent inn pale mwenge ni shahidi mzuri kwa hili. usiku ikipiga show bendi ya mnanda, kesho asubuhi wahudumu walikuwa na kibarua kigumu kuokota vipisi ya bangi na vinailoni vya unga. achilia mbali chupa na mabaki ya gongo. huko mitaani kukatiwa nyavu za madirisha ni jambo la kawyda. ugomvi wizi na biashara ya mihadarati kwny show ya mchiriku, ndiyo mahala pake. wale majambazi sugu, kwenye mnanda ndiyo chimbo lao. zile sura za hatari ukienda kwny mnanda utaziona. kuvamiwa na mamwela, kukamatwa wahusika na vifaa vyao, ni kawyda. mnacheza huku macho bara. kama haitoshi, ukienda club 'disco' usiku mnene zitapigwa ngoma za mamtoni miksa bongo flavour, saa 9 mtakatishwa miuno na maboringo, saa 10 mtachezeshwa rege, 11 mpk kuchwe mtamalizia na mnanda.
 
Kama hutojali kuna what group la Mchiriku humo kuna wakongwe na wadau wanaoujua historia za muziki huu na wasanii wa sasa pia wapo humo. Kwa vile unataka kuandaa Documentary nakushauri ujiunge huko uchukue baadhi ya "madini" ambayo yatakusaidia kwenye Documentary yako. Ukitaka kujiunga nitumie namba yako ya WhatsApp PM.

Sent from my SM-A105F using JamiiForums mobile app
Kama ni group la Mchiriku 4 Life mimi mdau muhimu sana humo,natambulika kwa utambulisho wa Mbega au Makaratas.Labda kama kuna group lingine sio mbaya mkuu.
 
Dah...kumbe walianza mwaka 1981 na Ali Hassan Mwinyi umeimbwa 1986
Kwenye hiyo interview waliyofanyiwa wasanii wa band ya Hisani Gari kubwa,kuna makosa mengi ya utunzaji wa kumbukumbu yamefanyika (Director wa interview ni Muddy Mwanaharakati).

Huo wimbo wa #Ally Mwinyi ulifyatuliwa kwenye albam no.1 (Vol.1) ya Hisani Gari kubwa iliyotoka mwaka 94.Na hata hivyo kwa kumbukumbu zilizo sahihi kabisa,hao Hisani Gari kubwa wimbo huo si wao bali ni mali ya band ya Night Star ya akina Haidary Kessy na Halfan Wamizoga chini ya umiliki wa Afande Mkama Sharp.

Historia sahihi ya mziki wa Mchiriku (mnanda)iko hivi:

Band ya kwanza kabisa iliyoanza kuingia studio na kufyatua albam ilikuwa ni band ya Dar Nyota ya akina Seleman Msasa mnamo mwaka 93.
Kwa wakati huo kulikuwa na band kubwa kuliko hii kama vile Night Star,Red Star, Zipolari,na zingine pia zilizokuwa zinapiga Mchiriku (mnanda) kwa kuchanganya na Magita.Tena zilikuwa maarufu kuliko Dar Nyota na hata hao Hisani Gari kubwa walikuwa bado kutambulika kwenye ramani ya mchiriku ipasavyo.

Dar Nyota wakiwa katika makumu yao (Band ya CCM mkoa wa Dar es Salaam) walipata mwaliko Dodoma kwenye shuguli za mambo ya chama,walipokuwa huko wakapata bahati ya kuingia studio ili kufyatua albam (RTD Dodoma),ndio wakatumia nafasi hiyo kufyatua albam ya kwanza ya miondoko ya Mchiriku mnamo mwaka 93 na kuiingiza sokoni.

Baada ya hapo band zingine nazo zikaanza kupata muamko wa kufyatua albam na hatimaye Mchiriku ukaanza kuwa maarufu.
Hisani Gari kubwa wao waliingia studio na kufyatua albam yao ya kwanza mwaka 94,na kwakuwa nyakati hizo hapakuwa na sheria za hati miliki (Copy Right) Hisani waliiba nyimbo nyingi za Night Star na kuzirecord.

Sasa basi,kilichowafanya Hisani Gari kubwa kukubalika kwa haraka na tapes zao (kanda) kuuza sana sokoni,ni kwa sababu wao wiliibuka na midundo tofauti kidogo na zile zilizokuwa zinajiita band kubwa kama vile Night Star ya Kariakoo na Zipolari ya Mtoni Kichangani kwa kuondoa mfumo wa magitaa na kupiga miondoko ya kisela na ya kuchezeka.

Kuanzia hapo ikawa ni mfululizo wa kuanzishwa band na kuingia studio chini ya makampuni ya usambazaji ya kihindi kama vile FK Mitha,Mamu Store na Mwananchi Store.Na hatimaye mziki unapata umaarufu na kushika kasi jijini Dar es Salaam na viunga vyake.

Kwahiyo kwa ujumla band ya Hisani Gari kubwa itabaki kuwa ni miongoni mwa band kongwe tu za mziki wa mchiriku nchini Tanzania lakini katu sio waasisi
 
Ahsante sana kiongozi kwa darasa unalonipa,basi ndio maana kuna wimbo ameimba dogo jack unaitwa maisha popote,kumbe katokea morogoro kuja dar
Mfululizo wa waimbaji wa Jagwa uko kama ifuatavyo:

(1)Dulla Seli muimbaji muasisi,kaimba Vol.1&2 (peke yake)
(2)Jumanne #Baba J,kaimba Vol.3,4 na 5
(3)Aigosh Mkwavi,kaimba kuanzia Vol.6
(4) Ally Fankulla,kaimba kuanzia Vol.7
(5)Dogo Jack Simela,kaimba kuanzia Vol.9
(6)Dogo Mwinyi (Mtoto wa Mlandizi),kaimba kuanzia Vol.10
(7)Machupa, kuanzia Vol.16 hadi sasa.
 
Kuanzia Vol 10 na kuendellea zinappatikana wapi?
 
Asante mkuu Kwa historia hii...
 
Mfululizo wa waimbaji wa Jagwa uko kama ifuatavyo:

(1)Dulla Seli muimbaji muasisi,kaimba Vol.1&2 (peke yake)
(2)Jumanne #Baba J,kaimba Vol.3,4 na 5
(3)Aigosh Mkwavi,kaimba kuanzia Vol.6
(4) Ally Fankulla,kaimba kuanzia Vol.7
(5)Dogo Jack Simela,kaimba kuanzia Vol.9
(6)Dogo Mwinyi (Mtoto wa Mlandizi),kaimba kuanzia Vol.10
(7)Machupa, kuanzia Vol.16 hadi sasa.
Asande sana Mkuu kwa ufafanuzi mulua,ila huyu Baba J na Dogo Jack Simela walikuwa moto sana kwa sauti zao.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Mfululizo wa waimbaji wa Jagwa uko kama ifuatavyo:

(1)Dulla Seli muimbaji muasisi,kaimba Vol.1&2 (peke yake)
(2)Jumanne #Baba J,kaimba Vol.3,4 na 5
(3)Aigosh Mkwavi,kaimba kuanzia Vol.6
(4) Ally Fankulla,kaimba kuanzia Vol.7
(5)Dogo Jack Simela,kaimba kuanzia Vol.9
(6)Dogo Mwinyi (Mtoto wa Mlandizi),kaimba kuanzia Vol.10
(7)Machupa, kuanzia Vol.16 hadi sasa.
Na kuna bendi fulani walimuimba Dogo Jack kuwa anamchezo wa kurudi kinyume nyume,sema nimesahau jina la wimbo,ila kuna kipande kinasema unajiita Simela Simela gani.

Sent from my SM-A305F using JamiiForums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom