Mchinjita: Wananchi wawe wa kwanza kulinda haki zao sio viongozi

Mchinjita: Wananchi wawe wa kwanza kulinda haki zao sio viongozi

Bawabu wa pili

Senior Member
Joined
Nov 14, 2025
Posts
147
Reaction score
432
Makamu Mwenyekiti wa Chama cha ACT Wazalendo bara, Isihaka Mchinjita, ametoa wito kwa Watanzania kutokubali kukata tamaa kufuatia matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025, akisisitiza kuwa silaha kubwa ya "mkandamizaji" ni kuuvunja moyo na mtazamo wa wanaokandamizwa.

Akizungumza jana, Januari 13, 2026, katika mkutano wa ndani na viongozi pamoja na wajumbe wa Jimbo la Ubungo, Mchinjita alitumia nukuu ya mpigania haki wa Marekani, Malcolm X, kuelezea umuhimu wa raia kulinda haki zao wenyewe badala ya kusubiri msaada kutoka nje au kwa viongozi pekee.

Soma pia: Mchinjita: Kilichotokea Oktoba 29 kimedhihirisha CCM imekosa ushawishi



“Wajibu wetu wa kiuongozi ni kuwaambia ukweli kwamba lazima sisi ndio tukalinde haki zetu, sio maneno ya viongozi. Tujenge hoja tukikaa mezani lakini nguvu ya umma ndio itakayoweza kuleta mabadiliko kwa sababu hoja zimeshajaa mezani", amesisitiza Makamu Mwenyekiti huyo mbele ya wafuasi wa chama hicho waliojitokeza kueleza dukuduku lao kuhusu uchaguzi uliopita.
 
Ikawaje wao ACT wakashindwa kulinda kura zao?
 
Ni kweli kabisa. Wananchi tunatakiwa kuandamana hadi haki ipatikane. Nguvu ya umma ikiamua hakuna wa kuizuia. Samia must go.
 
Back
Top Bottom