Isihaka Mchinjita, Makamu Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo Bara, amesema kuwa wakati wa kampeni za ndani ya CHADEMA za kumtafuta Mwenyekiti, taswira ya chama iliharibika sana kutokana na makundi ya ndani kushambuliana vikali.
Ameeleza kuwa moja ya mambo yaliyoumiza zaidi ni namna kundi la Mbowe lilivyokuwa likimzungumzia Tundu Lissu, hadi kufikia hatua ya kumchukulia kama "mtu ambaye hafai hata kuwa mwenyekiti wa kijiji."
View attachment 3445940
Kundi la Freeman Mbowe akiwemo Mbowe mwenyewe actually lilimdhalilisha na kumtukana sana Tundu Lissu mpaka kushambulia utu wake, heshima yake. Halafu hawa hawa leo wanasema Tundu Lissu alimtukana sana Mbowe. Uongo mtupu..!
Freeman Mbowe alifikia hatua ya kuutetea uenyekiti wake kwa majigambo ya kuwa yeye ni tajiri, ana pesa nyingi na amekisaidia sana chama na kumsaidia sana Tundu Lissu. After all pesa zenyewe anazodai anazo kumbe huwa ni mapesa machafu ya deal toka CCM na serikalini kwa gharama ya maisha na damu za wenzake ndani ya chama...🤔🤔!!!
Freeman Mbowe alifikia hatua ya kukufuru kusema kuwa, eti hata Tundu Lissu alipopigwa risasi mwaka 2017, basi asingekuwa yeye (Mbowe), Tundu Lissu angekufa. Kufuru hii, hakumpa utukufu Mungu wa mbinguni, akajitukuza yeye. Na atubu, hii dhambi ni mbaya sana...!
Yaani alijisahau kabisa kuwa, yeye ndiye alikuwa kiongozi mkuu wa chama na hilo lilikuwa jukumu lake mojawapo la msingi kulifanya akisaidiana na wengine kwa wakati huo kwa msaada mkuu wa Mungu wa mbinguni ktk kuokoa maisha ya Lissu, mtumishi wa Mungu kwa wakati huo...
Zile kauli za matwezo, majigambo na ufirauni mwingine uliofanywa na Team Mbowe wakiongozwa na
Yericko Nyerere ilikuwa ni intimidation kumfanya Lissu ajione hafai, mdogo asiyeweza lolote. Bahati mbaya ni kuwa hawakujua wana deal na mtu wa namna gani...!!
Pole zao wote hao. Mungu wa mbinguni awarehemu kwa kuwa hawajui watendalo...