Mchina aliyepata "A" tisa NECTA

dah wacha wachina waitwa wachina, akuna namna wageni wanajuwa
 
100% nakuunga mkono, pia hizo hizo IQ za weusi walio wengi waliandama london eti kupinga yaliyotokea zanzibar na wengine wanadai eti wanaenda fungua kesi ulaya kwa kunyimwa haki zao za uchaguzi wa haki, hizi IQ wazungu wanaendelea kupima na kujiridhisha zaidi kuwa tafiti zao ziko sahihi, tena inawezekana walipendelea maana hizi IQ ziko sub zero kabisa!
Tatizo unalodai kuwepo kwako unaenda kwa watu kutaka wakusaidie kulitatua ilhari wee ni mtu mzima mwenye 'akili' timamu, Hovyo kabisa! Unazira kisha unadai unanyimwa haki, hizi ni akili kweli?
Mleta mada umeumganisha vizuri point zako kuanzia kwa mchina mpaka kwenye uhalisia.
 
Wa Africa bado tunasafari ndefu mno. Na tatizo kubwa lipo kwenye Elimu yetu.

We angalia nchi masikini duniani.
Nchi karibu zote za Africa zimeandamana
Chini. Ni chache sana ambazo wamejitoa .
Na walio jitoa kuna Wazungu kibao wanaishi
Kwenye hiyo nchi.

Kwa kweli saa nyingine unaweza na kufiri labda
Kuna kitu kimekosekana Akilini mwetu. Kuna shoti fulani hivi au ni ujinga na uvivu wa kufikiria.

Sijui kwa kweli . Nabaki na maswali yangu tu.
 
Ninadhani mada yako ingekuwa ya kuhusu sukari tu, hoja ya IQ umeipoteza kabisa maana yake!! Unaleta dhana kuwa ukiwa na IQ kubwa basi unapaswa kukubaliana na hoja na ukiipinga unakuwa na IQ ndogo.

Mkuu, 1+8 = 9, 3x3 = 9, 14-5=9, 18/2=9. Namba zote hapo hazifanani, na hata aljebra pia - lakini jibu ni 9! Maana ya hii ni kwamba kuna njia nyingi tofauti za kufanya mambo na matokeo yakawa ya aina moja. IQ kubwa inasaidia kujenga uwezo wa kutambua njia hizo, sio kukubali kila unachoambiwa!! IQ ndogo inaleta upofu - sio kukataa jambo.

Tuache tabia ya kuona fikra tofauti ya kufanya mambo ni kosa. Tunajifunza katika tofauti hizo!!
 
Theory yako italeta maana zaidi kama ukiweza kuthibitisha kuwa huyu mchina amehamia hapa (miaka michache iliyopita) akiwa hajui kiswahili...Ila kama huyu "mchina" amezaliwa hapa mjini na amelelewa hapa mjini, tofauti yake na watanzania wengine itakuwa ni rangi tu...
 
Je hili la Mchina kuwa wa Pili kwenye mtihani wa kidato cha nne TanZania nzima inasema nini?
Amepata B ya Kiswahili, lugha ambayo siyo yake na wala sia ajabu haiongei nyumbani amewapita watoto wengi sana wa Kiswahili


Nashauri huyo mtoto wa kichina kama si raia wa Tanzania apewe uraia haraka sana.Anajali nchi yetu na lugha yetu,Elimu yetu na mitihani yetu.Ni wageni wachache sana wanaoweza jipambanua hivyo.Wageni wengi ungekuta wanapenda kufanya mitihani ya cambridge nk Huyu wetu aliyefanya mitihani ya NACTE kweli tumpe uraia yeye na wazazi wake kama wanataka.Ila yeye nashauri kabisa apewe.
 
Wewe una matatizo gani? huyo si mchina bali Mtanzania mambae ana asili ya china na hiyo Bell curve ilikuwa na drawback nyingi sana ambazo kama vile haiku consider vp minority wanakuwa disadvantage na kitu chengine kuhusu asia ni kweli walikuwa wanafanikiwa darasani sana na kwenye mitihani na hiyo imechukuliwa Zaidi kwenye overbearing parents na ndiyo maana kuna discussion kubwa sana hasa marekani why watu wamarekani wenye Asian origin wanakuwa na vyeti vizuri lakini wakifika kazini na once inapotakiwa creativity wanakuwa sawa na watu wengine au wanakuwa wana struggle sana.
Hivi unajua wewe ya kuwa kuna Watanzania wenye asili ya china wengi sana na wapo Tanzania for than 200 yrs kama unataka ushahidi huo nenda Zanzibar na kawaulizie wachina tambi( kwa sababu Biashara ya ni kuuza tambi) na wanakijua Kiswahili swa na watu wengine kwani ni sawa na watoto wa Kiswahili wengine na huko china wengi wao hawajawi kufika.Sasa huyo mchina aliyepata one form 4 unajua background yake? kwanza A ni mtanzania wa kuzaliwa kwa hivyo kufikia conclusion yako kwa sababu amepata B ya Kiswahili naona hapo umechemka
 
Mkuu umeugusa moyo wangu nachangia hiyo sehemu ya mwisho, hasa hasa hawa wanaopinga harakati za rais, mimi huwa siwaelewi wanahitaji mtu wa aina gani. Mimi nina imani ndani ya miaka 5 kwa speed hii ya serikali ya 5 kuna mafanikio makubwa tuyategemee, haingii akilini mf DG wa HESLB kutoa mikopo hewa kwa wanafunzi 19,000 ilhali kuna vijana wanasoma hawana mikopo eti pesa haitoshi, halafu hatua zinachukuliwa kuwafukuza kazi watu wanalaumu, na wanaolaumu ukufuatilia kwa undani utakuta na wao vijana wao hawajapata mikopo, kweli IQ ni shida kwetu
 


Hapana haujanielewa, Sukari ni mfano tu wa mambo mengi tunayoyafanya hapa nyumbani ambao kwa nchi za jamii nyingine hawawezi kuelewa!
Huu mfano wa sukari ni mfano hai kabisa lkn ziko nyingi, Raisi ameeleza sababu za kwa nini ameamua kufanya hivyo na amesema ataruhusu pala kutakapo kuwa na sababu ya kufanya hivyo na amekwenda mbali aksema sukari nyingi inayoingizwa hapa nchini huwa imebakiza mwezi iexpire huko ilikotoka lkn bado watu wanapinga uamuzi kama huu, sasa naomba unisadie sitaki kutoka kwenye mada kwani kuna mada ya sukari tayari inaendelea kupamba moto huko!
 
Barbarosa

Hamna colleration yote kufaulu Kiswahili na u taifa wa mtu.
Mimi O Level Kiswahili nilipata D na English A

CCM imeua shule zetu za Vipaji Maalum ambazo zilijijengea heshima Kubwa sana

SHULE ZETU ZA VIPAJI MAALUMU TUNAZOZIAMINI ZIKISHIKA NAFASI ZIFUATAZO

Ilboru- 53
Kibaha- 69
Mzumbe-71
Tabora boys-124
Kilakala-94
Tabora girls-123
Msalato-148

TAFAKARI PELEKA MTOTO PRIVATE
 


Ukinisoma vizuri utaona kwamba nimeliezea hilo najinukuu ,, najua kwamba data hazitoshi kuweza kuhitimisha chochote lkn labda kuna ukweli ndani yake kwamba watu wa Asia wana IQ kubwa klk wote Duniani kwa maana sijawahi kusikia Mwafrika diaspora akiongoza kwa kwenye mitihani huko aliko kama yuko naomba nisahihishwe"!
 
Andiko lako lipo sahihi na linaonyesha jinsi na wewe IQ yako ilivyo make ujui umesimamia lipi na unaongelea kipi, kichwa cha article Mchina aongoza mtihani, maelezo magufuli na sukari wapi na wapi.
 
...umefikiria ukaandika vizuri sana,jamaa anadai mchina kapata B ya kiswahili,mbona kuna watoto wengi tu wa kichina wamezaliwa Tz,na kama alipelekwa shule bora ambazo zinafahamika kwa matokeo yao kila mwaka,sioni sababu kwa nini asiwe wa pili.Ningemkubali huyo mchina kama angekuwa kamaliza shule ya kata.
Naona watu wamekurupuka,wanataka kuukana u afrika wao bila kufikiria nje ya box,naamini hata huko marekani wapo wachina wanaopata alama nzuri tu,na kuwashinda wazungu.!!
 
Andiko lako lipo sahihi na linaonyesha jinsi na wewe IQ yako ilivyo make ujui umesimamia lipi na unaongelea kipi, kichwa cha article Mchina aongoza mtihani, maelezo magufuli na sukari wapi na wapi.


Ukisoma vizuri utaona kwamba nimetumia hoja ya sukari kama mfano kuelezea uwezo wetu wa kufikiri!
 
Mhh!!! Siamini matokeo yake yaani hata kiswahili kapata B lakini cha ajabu hats kuongea kiswahili no shida kuongea..... Msikilizeni yupo live leotena @cloudsfm
 

Msaada wangu ni kuwa swala la IQ halikuwekwa mahala pake. Huyu mchina labda si mgeni wa kwanza kufanya mitihani hii. Kwani hatuna watu wa asili nyingine waliwahi kufanya mitihani hii? Hatuna waasia wanaofanya mitihani yetu?? Je kama IQ itapimwa kwa mchina kupata point 7, unasema nini kuhusu watahaniwa wa kiafrika waliowahi kupata point 7 na wakiwa na A ya Kiswahili??

Ungejikita kwenye kukubaliana na mpango wa Rais kuhusu sukari. Usichanganye kukubaliana au kutokukubaliana na Rais kama ni jambo la IQ kubwa ama ndogo!! That's my point.
 
Huyo mchina amesoma shule moja na watoto Wa jk na rais wako. We watoto wanasoma wapi!?
 
Kwa mtazamo wangu umeaminishwa kuwa ni hivyo na wewe ukaamini kwamba IQ yako ni ndogo.Hakuna kitu kama hicho. unawaelezea vipi watanzania wanaokwenda kusoma nchi ambazo mfumo wao wa elimu unaendeshwa kwa lugha za kihispania,kichina,kirusi,kifaransa,kireno,kidachi,kibelgiji,kijerumani nk na bado wakachanganywa na wazawa na wakafaulu mitihani yote na kuhitimu ktk vyuo vikuu vyao na hata kuwa wanafunzi bora.Na unapozungumzia wamarekani weusi si swala la IQ bali ni swala la mazingira ,umasikini,kuathirika kisaikolojia na fursa duni vilivyokidhiri ktk jamii husika ndiyo vinavyochangia kuwa na uelewa mdogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…