PakiJinja
JF-Expert Member
- Jan 16, 2012
- 11,766
- 26,156
Yanga ya sasa hivi hata uipeleke mkacheze kwenye mapango huko chini ya bahari, au ndani ya misitu ya Congo au Amazon itakufunga tu.Yanga atacheza na El Merreikh katika uwanja wa Kigali Pele ambao Zamani ulikuwa ukifahamika zaidi kama uwanja wa Nyamirambo.
Huu ni uwanja unaotumiwa zaidi na klabu ya Rayon na APR kwa nyakati kadhaa!
Awali klabu ya El Merreikh ilifikiria kuhamishia mechi yake Morocco ili kupata wafuasi na kukwepa nguvu ya Yanga kuwa na mashabiki wengi Rwanda.
Nikuambie tu... Kama kuna kitu Yanga wataenjoy kwa sasa ni kucheza nchini Rwanda na wana hakika ya kupata mashabiki wengi wa pale pale Rwanda na hata kusafiri na kuiunga mkono timu yao ni rahisi sana.
Mchezo huo utachezwa tarehe 16/09/2023
Kwanza wachezaji hawa huwa hata hawajui kama pale uwanjani huwa **** mashabiki.
Kambi ya Avic inawafundisha kutozingatia kama wanaungwa mkono au wanabezwa au wapo pekee