Mchezo wa draft

Nchi nyingi wanacheza draft la kwenda mbele na nyuma, lakini kwa Tanzania yapo ya aina mbili, kuna hilo la mbele na nyuma na kuna la mbele tu

We ni mtaalamu wa lipi?
la mbele na nyuma lipo kwenye computer dah
 
Kama ukitaka kujua draft lazima ukae na mtu anayejua draft, akufundishe michezo /format (wanaziita copy) na uzikariri baada ya kuzikariri na kucheza sana hapo ndio utaweza kujiongeza na kuzimodify hizo copy. Kuna watu wawili wazuri kwenye draft nawafahamu, ukimfunga anaenda kumuuliza mwalimu wake umemfungaje. Anamuonyesha draft zima lilivyoenda kwamba nilicheza hapa akacheza hapa, nikaenda hivi akaenda hivi yaani kete ya kwanza hadi ya mwisho. Halafu mwalimu anamwambia umekosea hapa akicheza hivi unatakiwa uende hivi. Yaani kiufupi mabingwa wengi wanaanza kwa kukariri
 
We ata jina tu hujui kuliandika ndio utajua kama kweli lina formula? Draft lina formula na lina husisha akili ndio ila siri ya draft ni kujua aina ya michezo mingi na kuikariri basi, hapo utakuwa unafungwa na mtu ambae anacheza mchezo mpya kwako au uwe unacheza na mtu unaelingana nae kiwango so mnaoteana au kama yule bwana hapo nyuma aliesema alikutana na mchezo unaitwa ebola na kwake mpya lazima apigwe sana hadi atakapouzoea, draft ni kama bao tu anaejua michezo mingi ndio bingwa

Huwezi kufananisha mpira na draft ata siku moja, mpira unaweza kubadili matokeo uwanjani ata first half umepigwa 2 unaenda second half unashinda 3, draft haliko hivo ukishakosea tu kusukuma kete moja kwa mpinzani anaelijua we hapo ata aitwe nani huponi lazima ufungwe tu
 
unatakiwa ucheze game mbili....yani unacheza draft lako at the same time unacheza na la mwenzio...kila anapocheza mwenzio inatakiwa ujue ana lengo gani...kukupiga tutusa au kukuwahi kingi...then hakikisha kete yako moja ina uwezo wa kuzuia kete mbili au tatu za mwenzio....bila kusahau hakikisha unampunja kete mpinzani wako....
 
nilijua ni mfuatiliaji, kwamba ukiona neno jipya utajaribu kujiuliza limetoka wapi basi ulifuatilie, basi ni vyema kukuacha na misimamo yako.

however, lengo la post yangu sio kubishana na mtu nilikuwa na changia tu mawazo yangu..!
Hatubishani mkuu tulikuwa tunaeleweshana tu. Anyway sorry kama nimekukwaza
 
Na concentration, kuna wakati nilikuwa napiga watu mpaka naona raha. Nilipouacha na kurudi tena, nikawa nashinda kwa 40% ya game zote nnazocheza.
 
unapeleka kete tatu za mstari mkuu (ikweta)...then unarudia mbili mkono wa kulia .....ukimaliza kabla hajaanza mashambulizi unaweza ukaanza wewe na kete mbele kati ya tatu za ikweta .....enjoy ....
 
Hakikisha hupotezi kete yoyote bure...yaani kama kula Kate angalau kwa kila kete upate faida..japo sio kila kete utakayokula italeta faida..wakati mwingine ni kuujenga mashambulizi..ili kushinda lazima uwe na kete nyingi kumshinda mpinzani
Hamna kitu hapa.
 
Kabla hujacheza kete yeyote lazima use umeangalia michezo yako mitatu ijayo pamoja na upande wake, kifupi in mchezo unaohitaji kufikilia vizuri?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…