YphNet
Member
- Sep 3, 2022
- 62
- 103
Wapendwa, najua mchezo huu vijana wengi sasa hawaufahamu, hivyo katika private project yangu ya AI (Artificial Intelligence) nimeamua kuchagua mchezo wa bao kutengeneza simple game ambalo mchezaji atacheza vs AI. Kwa sasa linapatikana kwenye Android pekee.
Nimechagua mchezo huu ili kuufanya uwe kidigitali zaidi na watu wengi waweze kujifunza. Ndani yake nimeweka aina tatu za bao: Bao kubwa, bao dogo na bao toto. Bao kubwa ndio maarafu zaidi lakini ndo linakera katika kujifunza kwakuwa linasheria nyingi na vipengele vingi. Bao dogo ni sawa na bao kubwa isipokuwa kipengele cha "kunamua" hakipo.
Bao toto, ni rahisi zaidi kujifunza kwakuwa halina sheria nyingi, hata hivyo linamahesabu mengi tofauti na inavyodhaniwa. Kwa mtu ambaye hajui kabisa bao na mshauri ajifunze bao toto kwanza, na ndo aina ambayo hata mimi mtengenezaji naicheza zaidi. Kwa ambao hawajui bao toto, maelezo yafuatayo machache tu utaweza kulicheza:
JINSI YA KUCHEZA BAO TOTO:
Game hili ni la Android, lipo Playstore, search "baotz" kisha install (free). Ni file dogo tu chini ya 250 KB.
Linahitaji Android 4.1 so kwa sasa karibu kila simu itakubali. Pia unaweza weka kwenye tablet, dashboard ya gari yenye Android (Android player) pia Android TV (nb: sijatest).
NB: Kwa sasa lina level 3. Bado AI haina ubora sana lakini ukiset level 3 (L3) kama unamawazo litakuchapa, pia AI engine ya Bao Toto type inauwezo mkubwa zaidi. Maboresho mengi yanahitajika ili liweze kuwa bora. Kwa sasa linatumia simple evaluation functions. Tofauti na nilivyolichukulia ni project tough kinamna yake, linahitaji permutations na evaluations za kutosha ikiwezekana baadaye na machine-learning ili licheze vizuri katika levels za kibingwa.
Anyway, enjoy level hizo hizo chache kwanza.
Playstore link: BaoTz - Apps on Google Play
Naambatanisha hiki kitabu kidogo (PDF eBook) cha Kiswahili chenye maelezo jinsi ya kutumia BaoTz app katika kucheza game la bao katika simu yako.
UPDATE: version 2.2.0
Kwa sasa huruhusiwi kula jumba wakati wa kutakata. Haya ni mabadiliko ya sheria ya bao kubwa. Update sasa ili uweze kutumia sheria hii ambayo inatumika na wengi.

- Lazima ucheze kuanzia chumba (shimo) chochote chenye kete mbili au zaidi
- Mwelekeo wa kusambaza kete haubadiliki mpaka zamu yako ya kucheza iishe
- Mshindi ni yule ambaye atahakikisha vyumba vya mstari wa ndani wa mpinzani
- Unapokula kete za mpinzani unazoa pamoja na kete zako ili kuendelea kusambaza
- Bao toto halizingatii sheria za matumizi ya "jumba" wala "vichwa au kimbi"