Mchezo huu utaisha lini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchezo huu utaisha lini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by chama, Aug 22, 2010.

 1. c

  chama JF-Expert Member

  #1
  Aug 22, 2010
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hii michezo ya kuigiza itakwisha lini?

  Watanzania tumechoshwa na michezo ya kuigiza, vyama vya upinzani vikuwa ni vichekesho vitupu, sisemi kwamba watanzania hatuna uchungu na nchi yetu au tunafurahia vitendo vy a kifisadi vinavyofanywa na CCM bali kinachotia uchungu ni vyama vya upinzani kukosa dira ya ushindi na kujaza mamluki wa CCM ndani ya vyama. Mfano kitendo cha kuiachia CCM kupitisha wagombea zaidi 10 bila kupingwa kama si usaliti kwa watanzania ni kitu gani? CCM inatumia kila mbinu kudhoofisha upinzani ; ukweli uliopo hivi vyama havikubaliki kila sehemu je wapinzani wamekosa busara kuungaisha nguvu ili kupambana na CCM? Lingekuwa jambo rahisi pale inapokubalika Chadema wapinzani waiunge mkono Chadema, pale inapokubalika CUF waiunge mkono CUF hata uraisi ilipidi wakubaliane asimame mgombea mmoja tu, viongozi wa upinzani wanalijua jambo hili lakini kwa kuwa hawapo kwa maslahi ya watanzania hawawezi hata siku moja wakakubaliana, kimsingi hii michezo ya kuigiza itaendelea siku hadi siku jana ilikuwa Mrema, akaja Mbowe leo hii Dr. Slaa hakuna kitachofanikiwa hadi watakapo tokea viongozi wa kweli kama akina LECH WALESA alipoongoza mapinduzi ya Poland; mapinduzi si lazima damu imwagike; tukipata viongozi wa kweli CCM itaondoka madarakani kwa nderemo na vifijo. Watanzania vyama vyama vya kweli tunavyo bali hatujajua namna ya kivitumia. Vyama vya wafanyakazi na wakulima vikisimama kidedea kutetea maslahi ya watanzania ndio pekee watakaoing`oa CCM madarakani. CCM wameshajifunza kilichotokea Kenya haitakuwa rahisi kuitoa madarakani watatumia kila mbinu chafu wanayoijua kutetea maslahi yao. WATANZANIA AMKENI !!!!!!!!!!
   
 2. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #2
  Aug 22, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Unafiki wa kipimo cha kwanza.

  Kwa nini wewe usianzishe hicho chama cha wakulima na wafanyakazi ili kipambane na ccm? Hata marekani kwenyewe kuna chaguzi huwa vyama vikubwa hivi havina kabisa wagombea (na hata vikiwa nao, havifanyi kabisa kampeni kwenye baadhi ya majimbo).

  Katika siasa hili ni jambo la kawaida kabisa. Vyama vya upinzani vinashindana na chama chenye dola na pesa zote zilitumika kujenga ccm kwa kodi za watanzania wote kipindi kile cha chama chashika hatamu. Itachukua muda kwa vyama vya upinzani kuwa strong Tanzania nzima.

  Na hata huo muda ukifika, kuna wakati chama fulani kitakuwa na nguvu sehemu fulani ya nchi (au kwenye tabaka fulani la wananchi) na sio nchi nzima ya Tanzania.
   
 3. S

  Solomon David JF-Expert Member

  #3
  Aug 22, 2010
  Joined: Mar 1, 2009
  Messages: 1,148
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Karibu sana chama

   
 4. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #4
  Aug 22, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  bange!
   
 5. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #5
  Aug 22, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,656
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  Yaani we acha tu....

  Hii August nadhani imevunja rekodi kwa wanachama wapya
   
 6. Abdulhalim

  Abdulhalim JF-Expert Member

  #6
  Aug 22, 2010
  Joined: Jul 20, 2007
  Messages: 16,472
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu usiumize kichwa chako, wewe kula ugali wako kwa maharagwe malizia na kangara siku ipite..waTz ukitaka kuwaamulia mustakabali wao watakukera tu.
   
 7. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #7
  Aug 22, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Chama, wewe unasapoti chama gani???
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Aug 22, 2010
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,475
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Wengine wanakuja kupiga kampeni humu!
   
 9. c

  chama JF-Expert Member

  #9
  Aug 22, 2010
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Ndugu Solomon, nadhani upeo wako wa kuelewa ni mdogo ama unaongea kama kada wa ccm, hoja yako haina msingi wowote. Unafiki hauna kipimo, si lazima tukubaliane kwenye kila hoja kinachotakiwa ni kujibu kwa hoja ya nguvu ama nguvu za hoja. Inaeleweka wazi kipindi hiki cha uchaguzi ni kipindi cha kuganga njaa bila kujali athari za baadaye na hicho ndicho kinachotuponza watanzania, suala la kuanzisha chama nadhani hukuelewa nilichokisema hapo ndipo ninapohoji upeo wako; sidhani kama unafuatilia mabadiliko ya kisiasa yanayotokea sehemu mbalimbali duniani, mapinduzi mengi yametokana na nguvu za wafanyakazi pale wanapochoshwa na dhuluma; hasa pale uwiano wa kipato na hali ya maisha vinapokuwa havioni huku watu wachache wakiwafurahia maisha hilo lipo njiani kutokea Tanzania, ukweli njaa huvuruga amani kuliko udini na ukabila, fuatilia mapinduzi yaliyomuondoa Bokasa, Marcias Nguema na Mobutu, umegusia siasa za marekani bahati huzijui. Marekani kuna vyama viwili Republican na Democrat vipo vyama vidogo kama Green party hivi vyama vidogo havina athari yoyote kwenye chaguzi za Marekani vishiriki ama visishiriki ni sawa tu. Kimsingi pale Republican inapoona haikubaliki hutumia pesa nyingi kwenye kampeni zake ili kushinda, Democrat hutumia mbinu hizo hizo kuuza sera zake, kuhusu kukishinda chama chenye dola fuatilia kilichoindoa KANU madarakani; siku nyingine usirukie mada kama ulieamkia mlango wa fisi.
   
 10. c

  chama JF-Expert Member

  #10
  Aug 22, 2010
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Acid mimi sisapoti chama chochote ila nasapoti mabadiliko ya kisiasa Tanzania, vyama vya upinzani vilivyopo Tanzania vilianzishwa ili kuleta demokrasia ya kweli; bahati mbaya sana vimeingia kwenye mtego wa ccm badala ya kulenga kwenye kuleta mabadiliko vimekimbilia kwenye kupigania ruzuku.
   
 11. A

  Audax JF-Expert Member

  #11
  Aug 22, 2010
  Joined: Mar 4, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  vyama vya siasa vyote vina uchu wa madaraka.Havina dhamira ya kweli ya kuleta mabadiliko. CCM OYEE?
   
 12. Ng'azagala

  Ng'azagala JF-Expert Member

  #12
  Aug 22, 2010
  Joined: Jun 7, 2008
  Messages: 1,276
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  ni sahihi, hasa hili la vyama vya upinzani kutoshirikiana ndiyo linaleta kinyaa zaidi. haiwezekani wagombea wa upinzani 8 against 1 wa chama tawala. wangekubaliana kumwacha mmoja vs CCM hapo tungeona kuwa nia ya vyama pinzani ni kuleta mabadiliko otherwise mtazamo unabaki kwamba watu wanatafuta tu maisha (rejea Songs of Ocol & Lawino kwa wale walikisoma)
   
 13. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #13
  Aug 22, 2010
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Huu ndo ukweli na huenda ikawa ni kweli kuwa Lipumba na Hamad wako mfukoni mwa Rostam Aziz. Mrema yeye anajulikana ni CCM damudamu na kapelekwa huko kuwavuruga wapinzani.
   
Loading...