Mchengerwa: Rufiji Mbioni Kuwa Mkoa

Mchengerwa: Rufiji Mbioni Kuwa Mkoa

Baada ya harakati za kugawa majimbo ya Uchaguzi kushika Kasi suala la kuunda Mikoa mipya nalo limeanza kujitokeza ambapo Waziri wa Tamisemi bwana Mchengerwa amesema huenda Rufiji ikawa Mkoa Mpya.Pia soma Ushauri. Ni muda sahihi Bagamoyo ipewe hadhi ya mkoa

Waziri huyo na Mbunge wa Rufiji amesema jambo Hilo litategemea ikiwa Wilaya za Mkoa jirani wa Lindi ya Kilwa kama itakubali Ili kufanikisha Vigezo.

Ikumbukwe Mikoa mingine iliyoomba kugawanywa na kuwa Mkoa Mpya ni

-Chato (itachukua Wilaya za Kagera,Mwanza,Kigoma),

-Mkoa wa Manonga( kutoka Tabora),

-Mkoa wa Handeni( kutoka Tanga),

-Mkoa wa Kilombero (kutoka Morogoro) na

-Mkoa wa Rufiji (kutoka Pwani & Lindi).

​

My Take
Kuongeza Mikoa mipya bila kubadili mfumo wa Usimamizi wake haiwezi kusaidia lolote kwenye maendeleo sana sana itaongeza mzigo Kwa walipakodi.


View: https://www.instagram.com/reel/DMz8-ORoT37/?igsh=NzhtMWd6Nmdjc25l
 
1.Kuondoa ma DC na kuwapa Nguvu Serikali za Mitaa kuamua mambo Yao badala ya Sasa kuwa mawakala wa Serikali kuu.

2.Kuwa na Kanuni maalumu za mgawanyo wa Rasilimali za Serikali Kuu kama ilivyo Nchi nyingi hasa USA badala ya Sasa kutegemea uchawa(viongozi wanaotoka kwenu).

3.Kukusanya na kupanga matumizi ya Fedha wenyewe badala ya Kila chanzo kuingia Serikali Kuu harafu ndio mnasubiria huruma za walioko Dom/Dar.
Dah,
Nakazia ✍️
Hakika wewe ni CHAWA pekee mwenye maarifa baadhi ya wakati. Big up
 
Back
Top Bottom