Mchemsho wa Ndizi Kwa samaki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mchemsho wa Ndizi Kwa samaki

Discussion in 'JF Chef' started by Joyceline, Oct 13, 2011.

 1. J

  Joyceline JF-Expert Member

  #1
  Oct 13, 2011
  Joined: Jan 9, 2009
  Messages: 1,010
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Mchemsho wa Ndizi Kwa samaki

  Ndizi mshare au ndizi kimalindi au za mbea tano(5) inategemea na familia yako
  samaki nusu kilo wabichi sato itakuwa nzuri zaidi
  nyanya moja
  kitunguu kimoja
  karori moja
  pili pili hoho
  mafuta vijiko viwili vikubwa

  1. Osha samaki wako vizuri hakikisha wametakata mpaka maji ya kusuuza yawe meupe
  2.Bandika kikaango jikoni weka mafuta ya kutosha kukaanga samaki, mafuta yapate moto wa kutosha, baada ya hapo tumbukiza samaki wako na waache kwa dakika **** wasikauke wawe brown kidogo.
  3. Menya ndizi, bandika sufuria jikoni weka ndizi kidogo chini , then weka samaki halafu katia viungo vyote, vitunguu, pilipili hoho yote, karoti moja, na nyanya moja.
  4. Weka ndizi zilizo baki, weka chumvi kiasi , weka maji kidogo. Itakuwa vizuri kama utafunika na sifuria ili mvuke urudi ndani, usifunike na mfuniko, endelea kuweka maji kidogo mpaka uhakikishe zimeiva,
  5. Usigeuze na mwiko utafanya chakula kipondeke, hivyohivyo ulivyofunika zigeuze kwa kuzirusha mpaka zichanganyike, weka mchuzi kiasi unachotaka , ziache kwa dakika tano. tayari kwa kuliwa.
   
 2. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #2
  Oct 13, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  kwenye mabano hilo neno karori au karoti..

  kingine poa pishi safii:)
   
Loading...