Mchele unapogeuka pumba................

Kapendana na nani mbona sioni chembe ya mahaba hapa? au mie ndio sielewi?

Hakuna mapenzi ndugu humu JF kuna ID za kike lakini wahusika ni wanaume hahahahaha mie nilileta tu shairi na sikujua kama litawafanya watu watafishike............lol
 
soma shairi hilo gaga, sijui nani nani anamfanyaje. Mnmh, ngoja aje mwenyewe atuambie vizuri.

Ushairi si lazima uzungumzie yanayokusiwe wewe unaweza kutunga ukawakilisha jamii pana, mie nimekaa nikafikiria nikaleta shairi nilitegemea manguli wa kughani kwa tenzi na nahau wangeniuliza kwa kutumia ushairi tukajibizana ili kukuza lugha lakini kwa bahati mbaya hatukufikia lengo............
 
Hapo nnakiri
Tabora ni wazuri
Wanyenyekevu kwa ari
hata bila ya hiyari
Angalia wakivinjari
pata shika ya hatari
Utaombea kaburi
Utumbukie kwa hiyari.

Hapo nnakiri Tabora ni wazuri

Wanyamwezi ni wazuri wamejaaliwa na manani
Uvmilivu wamebobea wanakula hata majani
Nsansa watakuungia ukajisikia burudani
Wanaladha ya boribo wamanyema hawaoni ndani
Itanibidi niende Tabora mwanyamwezi niweke ndani

Kwa maumbo wametulia na sifa pia tabia
Si wahuni wenye tamaa ya ofa za bia
Majimshindo ndo mana hukuwaharibia
Nitawaalika wapendwa harusi ikikaribia
 
Shossi,

heshima juu kabisa mkuu. huwa nasoma tu hapa kwenye hili jukwaa mara nyingi kuliko kuchangia. Nimeisoma hii thread yako weeeee nikavumilia weeeee lakini sasa nikaona hapana ngoja angalau niseme lililo moyoni likikuudhi natanguliza kuomba radhi kaka.

wakati ule ulipoaga halafu ukarudi nilikuambia unadeka unataka ubembelezwe na wadada. Ukaniambia nilikuelewa vibaya na mimi nikaamini hivyo.

Ukweli sioni ni kwa nini utake mtu akujibu vizuri kwenye kila post yako hata kama huyo ni rafiki yako. Mimi nina watu wachache hapa marafiki zangu lakini wakinitolea macho naona ni sawa as long as they have a point, wananisaidia. The important thing siyo mtu akutukane bali akusaidie kufikiri. Binafsi namwelewa Michelle, amekuwa akinisaidia kufikiri kwa changamoto zake kwa watu wengine kwa sababu huwa hana kawaida ya kuchangia post zangu. watu wengine pia wamekuwa wakikiri hilo.

Lakini pia nimeshutushwa na pale unapohusisha tofauti za kidini katika fikra za mtu.

Shossi, you are a good man, you are civilized, please take it easy. Avoid taking other people's opinion personal, especially when they are of a different religious denomination.

Be happy brother!

Kutunga shairi si ajabu, hilo kwanza eleweni,
Ushairi si dhambi, aliyanena Manani,
Msijenipa adhabu, kwa maswali ya kwa nini?

Modi mimi kughani, msiseme punguwani,
Ninaakili timamu wala sideki, hilo nawajulisheni,
Msinione ninadeka, mkanitenga jamani,
.
Malenga ni jina langu, naomba lizoeeni,
Barua zilizo zangu, Malenga niandikeni,
Mdumishe na huba na mapenzi kama zamani,

Kuna jambo la muhimu, bora niwajulisheni,
Kuna wazee muhimu, bora niwatajieni,
Gaijin ndo mwalimu, na Klorokwini sikieni,

Mkuu sinipe hila wakanitenga wenzangu
Hizo ni fikra zako niachie zakwangu
Ukiongea kaza maneno au umekula kungu
Usinisemee moyo wangu ukanitia machungu.

Gurudumu kama unahoja zilete kwa tungo
Tena zenye mishiko ukaze ni vivungo
Ziwe zenye vina uvitie na viungo
Usiviweke bayana vifunike na ungo
 
Hahahahaaaaaaaaa......Kudadadadaadeki.....kweli hapa kiswahili kimetulia sana.Kama anajitongozesha siinamaana kayakubali mashairi..hiyo kauli ya kusema Mpemba blabla ni kutaka mwanaume uendelee kukaza gidamu za viatu......hang over aliyonayo ni amarula kumbe...!!!Muache tu Binti jamaa mashairi yamemwingia.

Sikuanza malumbano, bali tungo na mashairi,
Ukwa ni mvutano, nusu nakugeuka shari,
Shosti kapewa kibano, na mabunda kaghairi,

Kuja kwenye beti, mimi nakapiga mia,
Michelle kajaribu sana,mbili hakufikia,
Mwishoni akala kona, Masanilo alipomjia,
 
Hakuna mapenzi ndugu humu JF kuna ID za kike lakini wahusika ni wanaume hahahahaha mie nilileta tu shairi na sikujua kama litawafanya watu watafishike............lol

Shossi sio kwamba umemlenga mtu kweli? ni shairi tu uliamua kulitoa? if yes basi punguza jazba ndugu yangu haya mambo ya jf yasikufanye uchukulie vitu serious kiasi hiki au sio mohd!
 
Ushairi si lazima uzungumzie yanayokusiwe wewe unaweza kutunga ukawakilisha jamii pana, mie nimekaa nikafikiria nikaleta shairi nilitegemea manguli wa kughani kwa tenzi na nahau wangeniuliza kwa kutumia ushairi tukajibizana ili kukuza lugha lakini kwa bahati mbaya hatukufikia lengo............

nifundishe na mimi.
 
Shossi sio kwamba umemlenga mtu kweli? ni shairi tu uliamua kulitoa? if yes basi punguza jazba ndugu yangu haya mambo ya jf yasikufanye uchukulie vitu serious kiasi hiki au sio mohd!

Wala hakuna aliekusudiwa hilo naweka bayana
Wadau walichangia wakadhani ni wao bwana
Mie nikataharuki kuona tunaanza kugombana
Michelle alinitia ari kunikejeli kinamna
Mie sikukubali kama noma ikawa noma
Gudumu hakutanabai na yeye akajitoma
Hata wewe hukuona ndo mana ukasema!
 
nifundishe na mimi.

Nitakufundisha kutunga hilo wala usijali
Utapangilia na vina vitamu kama asali
Utawachoma wabaya wasiwe na hali
Nitakufundisha na mngine ili uwe nguli
Ila sharti ugangamare uukaze na msuli
 
Kusema ukweli niliposoma kichwa cha hii thread na shairi lenyewe, ujumbe nilioupata nadhani ndo wenyewe na matokeoa yake yamekuwa yale yale!!! Ashukuriwe Klorokwini na Gaijin tu kuibadilisha direction.

Mi kuna kitu nakifikiria, ikiwa kweli Shoss hukumlenga mtu, ilikuwa ni shairi tu, naona jukwaa halikuwa sahihi, ungeiweka kule kwenye jukwaa la lugha. Nadhani kule lingekuwa na ladha zaidi. Kwa sababu sioni kama linavutia kuwa hapa kama una focus kwenye lugha ya ushairi. Lakini kwa jinsi lilivyo hapa na jinsi ulivyokuwa unamjibu Michelle kuna sehemu unaonesha ulikusudia na umemlenga mtu.

Nisamahe, ni akili yangu inawaza hivo. Lakini napenda mtu awe na furaha na amani, na heshima pia. Kwa hiyo jaribu kuilinda furaha yako kwa kutokorofishana na watu. Kama unalenga lugha ya ushairi peleka kule kwenye lugha........vinginevyo mmmmmh!!!!
 
Nduguzangu mshamjua yule nilomkusudia?
Ameshindwa jizuia ameidhihirshia dunia
Kaingia ukumbuni akanya kwenye zulia
Ukuulizwa kwanini si akaanza kulia?

@ Shosti umenifurahisha sana mpenzi wangu :wink2:

Najua zaidi kichagga kuliko kiswahili,
Lakini hii Shoss kaka angu, ni ushauri tuuuu!!!
Nisamehe sina mbaya, lakini tusifanye maisha magumu kiasi hiki!!!!!
Hii mipasho hii siyo kabisa kaka angu!!!
Narudia Nisamahe kama nimekukwaza lakini natamani uwe na furaha tu.
 
So mipasho hizi ni tenzi jaribu kusoma maudhui ya tungo/ushairi utaniambia nilichokifanya sahihi............ sikuweza kuliweka kule kwenye lugha kwakuwa shairi linabeba ujumbe wa kirafiki na mahusiano nilitaka watu washuke mashairi! keani leo ndio mara yangu kuweka hapa mashairi?
 
Kwani kule watu wasingeweza kujibu?Kubali tu kwamba ulikua unawapasha watu flani flani!
 
Kwani kule watu wasingeweza kujibu?Kubali tu kwamba ulikua unawapasha watu flani flani!

Ndio nilikukusudia saga chupa unywe, naona unataka kujiingiza na wewe hata kama nimekusudia basi hazidi mtu mmoja soma hilo shairi lakini naona na wewe unatafuta sehemu ya kujiingiza siwezi kuli edit kuafiki matakwa yako I am sorry..........................
 
Tafadhali kaka siwezi kujiingiza sehemu isiyo saizi yangu!Kutupiana madongo sikufunzwa wala sio sawa yangu sasa naona unanilazimisha uhusika!Kweli una lako jambo!Kila la kheri na kushushuana!I'm out!
 
Tafadhali kaka siwezi kujiingiza sehemu isiyo saizi yangu!Kutupiana madongo sikufunzwa wala sio sawa yangu sasa naona unanilazimisha uhusika!Kweli una lako jambo!Kila la kheri na kushushuana!I'm out!

Maneno yako "Kubali tu kwamba ulikua unawapasha watu flani flani!" wala sikukushushua samahani kama wewe unahisi nimekushushua mie nao nimekupa SURE..................
 
Maneno yako "Kubali tu kwamba ulikua unawapasha watu flani flani!" wala sikukushushua samahani kama wewe unahisi nimekushushua mie nao nimekupa SURE..................

Kwahiyo watu flani flani ni jina langu?Kweli wewe ni dada wa uswahilini haswa!Wakunipa shur utakua wewe?Tafuta unaolingana nao!
 
Back
Top Bottom