mchango wenu wa mawazo jamani.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

mchango wenu wa mawazo jamani....

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Jestina, Jun 28, 2012.

 1. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #1
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  wakuu nina milioni kumi,najiuliza nifungue biashara sijui biashara gani hapa mtaniadvise au niweke msingi kny kiwanja changu kule kibaha tatizo nikiweka msingi sijui nitamaliza lini kujenga as sina uhakika/regular income na b, nikianza biashara ni biashara gani itakayonirudishia hela yangu ili niweze kujenga? msaada kny tutazzz.....:israel:
   
 2. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #2
  Jun 28, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  Hizi thread ni nyingi sana humu, Tatizo letu ni wavivu wa kusoma, pitia humu janvini ziko nyingi sana
   
 3. sweetlady

  sweetlady JF-Expert Member

  #3
  Jun 28, 2012
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 16,982
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  :sleepy: :sleepy: :sleepy:
   
 4. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #4
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  sweetlady utakuwa umeshiba sana,unasinzia tu lol
   
 5. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #5
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  leta mawazo mapya,sio wote tugombee kufanya wakala wa m-pesa...maana ndio biashara mnayoadvise kila siku....:wacko:
   
 6. Root

  Root JF-Expert Member

  #6
  Jun 28, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,267
  Likes Received: 12,986
  Trophy Points: 280
  Tanzania biashara bado nyingi sana so ni wewe tu.
  waweza kuwa muuzaji wa bidhaa kwa retail.
  Hapa itategemea sasa na biashara waweza anzisha duka la retail hasa pale kkoo na ukawa unanunua vitu kwa wafanyabiashara wakubwa unauza kwa retail ukiwa mvumilivu utakula mbivu
   
 7. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #7
  Jun 28, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Hiyo pesa yako iweke kwanza mpaka utakapopata au utakapojua nini majibu ya haya maswali:
  1. Biashara gani ambayo una uwezo wa kuifanya (hapa tunamaanisha capacity)
  2. Eneo gani unataka kuifanyia hiyo biashara-je wateja wanapatikana sehemu hiyo? na banda la kufanyia biashara, gharama ya banda?
  3. Soko la hiyo bidhaa ikoje? nina maana ya je ina soko mwaka mzima au kwa kipindi fulani tu.
  4. Bidhaa utakazouza zitapatikanaje?
  5. Je mzunguko wa pesa katika eneo hilo ukoje?
  6. Je wateja wako ni kundi gani au ni watu wa aina gani?
  7. Mtaji wa biashara huo ni kiasi gani?
  8. Je unataka kufanya biashara mwenyewe au kuna mtu au watu utawaajiri ili wakusaidie, kama ndivyo je ni watu wa aina gani na nini gharama zao?
  9. Je hiyo biashara itahitaji kiasi gani, na unategemea kuuza kiasi gani kwa siku au kwa mwezi? na je unategmea baada ya muda gani mtaji wako ulioweka kwenye biashara iweze kurudi?
  10. N.K

  Kama hauwezi kujibu hayo maswali au 80 asilimia ya hayo maswali vizuri, basi hiyo pesa yako nakushauri ukatafute kiwanja eneo zuri ukanunue na mara utakapokuwa tayari unajua biashara gani ya kufanya, ndipo ukauze hicho kiwanja ili hiyo pesa utumie kwenye hiyo biashara. Kiwanja ununue sehemu ambayo ni potential ili utakapohitaji kuuza usipate shida.

  Onyo.
  Kamwe usipoteze pesa zako kwa kutafuta akuandalie business plan kabla hujajua bado ni aina gani ya biashara una uwezo wa kuufanya. Kama unahitaji sehemu ya kwenda kujenga capacity kwanza ili ukimaliza uweze kujua nini biashara gani unaweza kufanya. Na naamini baada ya muda mfupi sana,tena masaa 3 kwa siku ya jmosi na jpili tu na ndani ya miezi 3 tayari utakuwa na uwezo wa kujua ni biashara gani una uwezo wa kufanya. Usihofu gharama, kwani katika kipindi hicho gharama haizidi 300,000(laki tatu tu).

  unaweza uni pm au tuwasiliane kwa lindinachingwea@gmail.com
   
 8. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #8
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280
  Wewe kweli ni punguwani, hizo thread zote zina zungumzia M-PESA TU? Kwani huwezi kuwa na mawazo yako mwenyewe? Hizi hudumu Nchi nyingine ni pesa, tusipende vya bure sana,

  Huko uliko kuna kampuni za Consultancy wafuate na uwape pesa wakushauri nini cha kufanya, Na by the way hutapata michango yoyote ya maana make watu walisha choka na marudio rudio ya vitu vile vile,
   
 9. CHASHA FARMING

  CHASHA FARMING Verified User

  #9
  Jun 29, 2012
  Joined: Jun 4, 2011
  Messages: 6,133
  Likes Received: 2,118
  Trophy Points: 280

  Mkuu unahangaika kushauri Mtu Asiye kuwa siriasi,
   
 10. Mgombezi

  Mgombezi JF-Expert Member

  #10
  Jun 29, 2012
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 630
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  FURSA YA BIASHARA NI NINI?

  Watu wengi wamekuwa wakijiuliza biashara za kuanza kufanya, wakati mwingine kumekuwa na baadhi ya watu ambao huwa na kianzio cha biashara (mtaji), lakini hawafahamu ni biashara gani wataweza kufanya.

  Fursa ya Biashara (Business Oppurtunity) hutokana na mahitaji ya watu katika eneo husika; kwahiyo katika kutengeneza wazo la biashara (Business idea) huanza kwanza kwa kuchunuguza fursa zilizopo katika eneo husika. Baada ya hapo hufuata mpango wa biashara (Business Plan).

  Kwa hiyo unapofikiria ni biashara gani ya kufanya ni vyema kuchunguza mahitaji yaliyopo katika eneo husika (inaweza kuwa mtaani kwako, katika mji au hitaji la Taifa). Kwa kweli nchi yetu bado kuna mahitaji mengi ambayo yanaweza kutumika kama fursa ya biashara; hebu jiulize toka unapoamka ni mahitaji au shida kiasi gani umekutana nazo, naomba kuorodhesha baadhi ya maeneo ambayo tunaweza kuchunguza mahitaji:

  1. Unapotaka kwenda kuoga asubuhi nyumbani kwako, unapata maji kwa urahisi?
  2. Je unapotaka kupata kifungua kinywa, unapata kitafunio kwa urahisi?
  3. Je unapotaka kwenda kazini au kwenye shughuli zozote, usafiri kutoka eneo lako uko vipi?
  4. Unapofika katika eneo lako la kazi au shughuli yeyote kuna vitendea kazi vya kutosha?
  5. Vitu gani vinakufanya kushindwa kutekeleza majukumu yako ya kazi au shughuli za kila siku?
  6. Unapotaka kupata chakula cha mchana, je unapata katika mazingira gani?
  7. .............................
  8. .............................

  Wengine wanaweza kuendeleza, mambo ambayo tunaweza kuchunguza kutokana na mazingira husika.

  Jambo lolote ambalo utaliona ni hitaji kwa watu basi hiyo ndio fursa ya biashara, kwa hiyo unapaswa kutengeza wazo la biashara. Tuache kuyachukulia mazingira yanayotuzunguka na mambo yanayoendelea katika jamii kuwa ni kawaida, kwa mfano unaweza kuwa unakwenda kupanda daladala kila siku kwa kugombania na ukachukulia hiyo ndio hali ya kawaida, lakini tunaweza kutumia hiyo hali kama fursa ya biashara na kutengeneza wazo la biashara.

  Tunapoaangalia mahitaji ya watu na kugeuza kama fursa ya biashara, basi hapo tutakuwa tunafanya biashara lakini vile vile tutakuwa tumekutana na mahitaji ya jamii inayotuzunguka na taifa kwa ujumla, kwa kweli jamii yetu bado ina mahitaji mengi; itashangaza kusikia kwamba hatujui nini cha kufanya na jamii inayotuzunguka. Hebu tuige mfano wa Mjasiriamali Bakhresa na kampuni yake ya AZAM, kwamba amekuwa akichunguza mahitaji ya jamii na kuleta bidhaa ambayo itakutana na hitaji hilo, mfano; CHAPATI, MIKATE, TUI LA NAZI na nyinginezo.

  Vile vile tujifunze kutofautisha fursa za biashara katika nchi zilizoendelea na nchi zinazoendelea kama ya kwetu; kwani upatikanaji wa fursa za biashara ndani ya Marekani ni tofauti na Tanzania; ndio maana katika nchi zilizoendelea wamekuwa na biashara za mitandao na biashara nyinginezo ambazo zisikiri kama zinaweza kuwa na ufanisi mkubwa zaidi kutokana na mazingira yetu; kwani nimeshawahi kuona baadhi ya link zikielekeza jinsi ya kutengeza fedha ka jinsi ya mtandao n.k. Nafikiri bado jamii yetu ina mahitaji mengi ambayo yanahitaji mtu wa kuyatatua.

  Nawatakia kila la kheri wajasiriamali wenzangu, katika kukutana na mahitaji ya jamii inayotuzunguka na kupunguza hili wimbi kubwa la kutegemea bidhaa kutoka nje; yaani tumeshindwa hata vijiti vya kusafisha meno, miti ya kuchoma mishikaki n.k, vimekuwa vikitoka China; hawa watu wamekuwa wakitoka mbali na wakifika hapa wanabaini fursa za biashara na kurudi kwao kutendea kazi.
   
 11. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #11
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  ngoja nikupotezee kabla hujachafua mada yangu na ***** wako.
   
 12. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #12
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Thanks wakuu Telo,Mgombezi and Andybird kwa mawazo yenu mazuri,nitayafanyia kazi....
   
 13. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #13
  Jun 29, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  MISSION IMPOSSIBLE IDEA:

  1 - Tafuta frem moja ya biashara kisha lipia na uikarabati katika muonekano wa kiofisi ya kisasa.(weka mlango wa alluminium, air condition, meza, kiti, viti 2 vya wageni, kompyuta, printer, shelf / kabati nk ila usiweke tangazo lolote)
  2 - Watangazie watu waaminifu unaowafahamu (ambao wana uwezo wa kuingiza hela kila siku na walio na shughuli nzuri na kubwa zinazowaingizia kipato, mfano wafanyabiashara na wafanyakazi wenye mishahara mizuri) watangazie kuwa unatoa mikopo ya marejesho ya mwezi mmoja kwa riba ya 30%, kuanzia Tsh 100,000 hadi milioni moja.
  3- Weka lending policy and procedures ambazo zipo secured na sustainable katika utoaji wa huduma hiyo.
  4 -Anza kutoa mikopo kwa mtaji wa kiasi utakachokuwa nacho baada ya process hapo juu. Amini kuwa kama utakuwa serious na kufuatilia ipasavyo, basi baada ya miezi 12 (mwaka 1) tangu ufungue hiyo kijiofisi chako utaweza kupata return nzuri kama ifuatavyo: mfano ukaanza na mtaji wa milioni kumi (working capital)

  [TABLE="width: 500"]
  [TR]
  [TD]MWEZI
  [/TD]
  [TD]MTAJI (TSH)
  [/TD]
  [TD]RETURN (TSH)
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]January
  [/TD]
  [TD]10,000,000
  [/TD]
  [TD]13,000,000
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]February
  [/TD]
  [TD]13,000,000
  [/TD]
  [TD]16,900,000
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]March
  [/TD]
  [TD]16,900,000
  [/TD]
  [TD]21,970,000
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]April
  [/TD]
  [TD]21,970,000
  [/TD]
  [TD]28,561,000
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]May
  [/TD]
  [TD]28,561,000
  [/TD]
  [TD]37,129,300
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]June
  [/TD]
  [TD]37,129,300
  [/TD]
  [TD]48,268,090
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]July
  [/TD]
  [TD]48,268,090
  [/TD]
  [TD]62,748,517
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]August
  [/TD]
  [TD]62,748,517
  [/TD]
  [TD]81,573,072
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]September
  [/TD]
  [TD]81,573,072
  [/TD]
  [TD]106,044,994
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]October
  [/TD]
  [TD]106,044,994
  [/TD]
  [TD]137,858,492
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]November
  [/TD]
  [TD]137,858,492
  [/TD]
  [TD]179,216,040
  [/TD]
  [/TR]
  [TR]
  [TD]December
  [/TD]
  [TD]179,216,040
  [/TD]
  [TD]232,980,851
  [/TD]
  [/TR]
  [/TABLE]

  Hivyo baada ya miezi 12, unaweza kuisajiri biashara yako na kuwa kampuni na kuifanya kuwa ofisi kubwa. Najua kutakuwa na matumizi mfano, kulipa mshahara kama kuna mtu utakuwa umemwajiri, umeme nk. ila gharama zake hazitakuwa kubwa za kuweza kukushinda kulipia kwa kutafuta fedha mbadala kutoka katika vyanzo vingine ili mtaji ubaki vile vile.

  Ni wazo tu.
   
 14. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #14
  Jun 29, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Asante kwa hili wazo mkuu,ubarikiwe...nimelipenda..will definately work on it....
   
 15. Laigwanan76

  Laigwanan76 JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: Nov 21, 2010
  Messages: 540
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35

  Hao ndio wabomgo na utajiri wa harakaharaka........kaazi kwelikweli
   
 16. Jestina

  Jestina JF-Expert Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 4,806
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  wacha tujaribu bana....:spy::nerd:
   
 17. T

  Tuliwonda Senior Member

  #17
  Jul 1, 2012
  Joined: Jun 29, 2012
  Messages: 121
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Ukishapata biashara ya kufanya, nakushauri usitumbukize hela yote huko. Weka pembeni angalau mil 3 itakusaidia kwenye + or -.
   
 18. e

  exzavery New Member

  #18
  Jul 5, 2012
  Joined: Jul 4, 2012
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hello Tanzania!
   
 19. neggirl

  neggirl JF-Expert Member

  #19
  Jul 6, 2012
  Joined: Jul 30, 2009
  Messages: 4,830
  Likes Received: 81
  Trophy Points: 145
  wazo zuri.. but changamoto kubwa iko ktk kufuatilia waliokopa walipe.. na wakati mwingine wengine hushindwa kulipa
   
 20. m

  mwajiri Member

  #20
  Jul 6, 2012
  Joined: Feb 17, 2012
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  1. Kila jambo lenye mafanikio lina changamoto, hivyo ni muhimu kufahamu kwa mapana kitu unachokifanya, ukipende, utafute ujuzi, upate uzoefu kwa wengine wanaofanya au waliofanya. Nothing comes easy.
  2. Kila mkopo unapaswa kurejeshwa ama kulipwa kwa wakati na kama ilivyokubaliwa. Mkopeshaji na mkopaji wanapaswa wafahamu dhumuni la mkopo, umuhimu wa mkopo, athari zinazoweza kupatikana mkopo usiporejeshwa kwa wakati, usalama wa mkopo uliotolewa na yote muhimu yanayohusu mkopo ikiwemo kupanga namna za kuweza kufanya mikopo iliyotolewa kurejeshwa. Unaweza kupata msaada kwa hili kwa wanasheria, maafisa wa serikali za mitaa, maafisa watendaji wa kata, wajumbe wa nyumba kumikumi, wamiliki wa taasisi na asasi za kifedha na wafanyakazi wa mabenki ambao wanaweza kukusaidia kwa ushauri juu ya taratibu nzuri za kutumia katika biashara hii.
  3. Kabla ya kuanza biashara hii, mkopeshaji anapaswa kujua sababu zote zinazopelekea wateja kushindwa kulipa mikopo, kisha afanyie uchunguzi na kuweka mipango ya kuweza kukabiliana na changamoto hizo.
  4. Nimelipenda wazo hili, kama mtu akiwa serious anaweza kufanikiwa. Hasara na Faida ni sehemu ya biashara na hakuna biashara isyo na hasara ila kinachotakiwa ni hasara isiwe kubwa.
   
Loading...