Mwenyezi Mungu ametuumba Wanadamu kwa Mfano wake, lakini ametupa haiba tofauti. Mfano; haiba ya Wazungu ni tofauti na Yetu Waafrika na ya Warabu ni tofauti na ya Wahindi, Wachina na kadhalika.
Katika kuonesha Utukufu wake, Mungu ametupa Utajiri wa Asili(Natural Resources) lakini ili Mwanadamu anufaike na Utajiri huu wa Asili inambidi atumie akili ya ziada.
Wenzetu Wazungu, Wachina, Wahindi, Waarabu walishaanza kunufaika na utajiri wa Asili walio pewa na Muumba Mbingu na Ardhi, Waafrika bado hatujaanza kunufaika na Utajiri huu. Tatizo kubwa likiwa ni lack of good learship, Leo nataka nieleze Mchango wa Mh. Ngeleja katika Sekta ya Madini.
Madini ni chanzo kubwa ya kuinua Uchumi wa Nchi, kuna mifano ya Nchi nyingi ambazo zimefanikiwa kukuza Uchumi wao kupitia Madini, Tanzania tuna Madini ya aina nyingi Mfano; gold, iron ore, nickel, copper, cobalt, silver, diamond, tanzanite, ruby, garnet, limestone, soda ash, gypsum, salt, phosphate, coal, uranium, gravel, sand and dimension stones n.k.
Nchi yetu ina ardhi ambayo imejaliwa utajiri mkubwa, Mfano; Tanzanite inapatikana Tanzania tu, je tanzania imesaidia nini kukuza GDP ya taifa letu? Vile vile tuna dhahabu nyingi sana na katika Africa nzima sisi ni wa 4 kwa kuzalisha tani zaidi ya 40 kwa mwaka. Copper kwa mwaka tunazalisha zaidi ya tani 2980, silver more tha10 tonnes per year. Etc.
Tanzania tulianza kijiingiza katika uchimbaji wa Madini kwenye miaka ya 90s, lakini bado hatukupata matunda ya Madini, Utajiri huu umeguuka laana kwa wazawa na kuwanufaisha wachache (Wawekezaji na washirika wao).
Ila kwa kuwa watanzania hatuna tabia ya kusoma na kufanya utafiti hatujui watu walio tukomboa katika sekta mbali mbali, ukimtajia Mtanzania wa kawaida jina la Ngeleja kitu cha kwanza ni kufikiria maneno machafu ya wanasiasa chwara ambao wanapenda kuwa chafua wenzao. Ukweli ulio wazi Mh. William Ngeleja ni Mkombozi katika sekta ya Madini katika kipindi chake cha miaka 5 kama Waziri wa Nishati na Madini alifanya Mapinduzi makubwa kwa maslahi ya Watanzania Wanyonge.
Kulingana na utafiti tulioifanaya kama Wanafunzi wa Chuo Cha Madini Dodoma, tumebaini Mkombozi wa nchi hii katika sekta ya Madini ni Mh. William Mganga Ngeleja, love him or hate him this is a matter of fact. ule usemi wa Nabi hakubaliki kwao umepitwa na wakati, huu ni wakati wa kuwa kubali na kuwaunga mkono viongozi wetu Wazalendo kama Ngeleja, kashfa za kutengenezwa zisitunyime viongozi wenye maono.
Mwaka 2008 sekta hii ya Madini ilipata Mkombozi kijana kutoka kanda ya ziwa, alifanya mapinduzi makubwa kwa maslahi ya wanyonge na Taifa kwa ujumla. Mh. Ngeleja alifanya mambo makubwa na bado sekta hii ina muhitaji sana.
} Mh. Ngeleja alifanikisha mchakati wa kupata Sera mpya ya Madini mwaka 2009.
} Mh. Ngeleja alifanikisha mchakato wa kupata Sheria mpya ya mwaka 2010.
Baadhi ya mambo mapya na muhimu yalioingizwa katika Sera na Sheria mpya ya madini ni pamoja na;-
a\ Sharti la Serikali kumiliki hisa za bure katika migodi(free carried interest), mfano migodi wa Buckreef Geita, Serikali inamiliki hisa za bure 45℅ kupiti STAMICO, Mchuchuma/ Liganga(NDC 20%) Na ngaka (NDC 30%).
b/ Migodi yote inatakiwa kununua Huduma na bidhaa mbalimbali nchini badala ya kuagiza kutoka nje kama ilivyokuwa awali.
c/ Kipindi cha leseni za wachimbaji wadogo kimeongezwa kutoka 5-7.
d/ Viwango vya mrabaha vimeongezeka, kwa mfano, dhahabu kwa sasa ni 4% badala ya 3%(migodi ilianza kulipa mrabaha mpya Mei 1, 2012).
} Mh. Ngeleja alisimamia kuifufua STAMICO mwaka 2008, awali ilikuwa imeorodheshwa kufutwa kabisa.
} Mh. Ngeleja alisimamia kumpata mwekezaji katika mgidi wa Makaa ya Mawe na Chuma wa Mchuchuma/Liganga kwa kushirikiana na NDC mwaka 2007-2011.
} Mh. Ngeleja alisimamia kuurudisha mgodi wa kiwira mikononi mwa serikali kupitia STAMICO Mwaka 2009/11.
} Mh. Ngeleja alisimamia kampuni za madini kuanza kulipa kodi ya mapato (30℅) mfano, resolute (Nzega), Geita Gold Mine (Geita), Tulawaka (Biharamulo) na TanzaniaOne (Mererani).
} Mh. Ngeleja alihakikisha maeneo zaidi kwa ajili ya wachimbaji wadogo yanatengwa na serikali.
} Mh. Ngeleja aliasisi utaratibu wa Mfuko Maalum wa kusaidia wachimbaji wadogo nchini.
} Mh. Ngeleja alipiga marufuku usafirishaji nje ya nchi wa madini ghafi ya Tanzanite yenye ukubwa unaozidi gramu 1, mwaka 2010 April.
} Mh. Ngeleja ni Muasisi wa utaratibu wa kutoa hati ya uasili( Certificate of Origin) kwa wanaouza madini ya Tanzanite.
} Mh. Ngeleja alisimamia uanzishwaji wa wakala wa ukaguzi wa Migodi, Tanzania Mineral Audit Agency (TMAA). Mwaka 2009. Nb; manufaa ya wakala huu yanajulikana.
} Mh. Ngeleja alisimamia mchakato wa Tanzania kujiunga na tasnia ya uziduaji duniani (EITI) kuanzia mwaka 2009.
} Mh. Ngeleja alisimamia kuhamishwa kwa kitengo cha kukata almasi (TRASORT) kutoka Uingereza na kuhamia nchini mwezi agosti mwaka 2010.
Huyu ndiye Mh. William Mganga Ngeleja nimjuaye Mimi, kijana mwenye good track record katika utendaji wake serikalini, kauli mbiu ya Hapa Kazi tu inawafaa Viongozi wenye haiba/hulka ya William Ngeleja.
Kwa wale tuliopo kwenye field ya Nishati tunaweza kuona gap ya Ngeleja, imeshindwa kuzibika ni wazi Prof. Muhongo AMEfail, kazi kubwa anayoifanya ni propaganda tu, watanzania wanapenda viongozi wa propaganda na sio wa chapa kazi kama Ngeleja, ila naamini Mh. Rais atapata maono huko mbele and sekta ya Madini itarudi kama enzi za Ngeleja.
Naomba Kuwasilisha, kama Wasomi tujadiliane kwa hoja, hakika Ngeleja ni shujaa, Mkombozi wa Tanzania katika Sekta ya Madini.