Mchango wa WanaJF Kuelekea Uchaguzi wa Kidemokrasia 2020

Sophist

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
4,220
2,000
Ndugu wana JF,

Ninawasilisha ombi kwenu kujitolea kuchangia nchi yetu iweze kufanikisha uchaguzi wa kidemokrasia (2020) kwa lengo la kuimarisha utawala bora katika taifa letu.

Pengine tuanze kutoa ushauri wa kitaalam kwa vyama vya siasa na wagombea kila mara wawe wanakuja hapa kuchota maarifa na ujuzi utakachangia kuimarisha kampeini za uchaguzi kwa ajili ya vyama na na wagombea wenyewe.

Ninadhani kuwa ni kwa njia hii JF itakuwa imetoa mchango wa kutosha kwa maendeleo ya demokrasia hapa nchini.

Kwanza: Maudhui ya Manifesto ya Upinzani

Namba Moja

Serikali mpya itakayoundwa Novemba 2020 kuondoa (Undo) sheria zote zilizopitishwa na serikali hii ambazo zinakandamiza uhuru wa raia kujieleza na kujumuika (vyombo vya habari, vyama vya siasa, mawasiliano/matumizi ya mitandao ya kijamii, NGOs/jamii ya kiraia, wakulima, biashara ya fedha za kigeni na kadhalika) ili kujenga jamii huru na inayowajibika kimaadili kwa hiari badala ya kushurtishwa.

Namba Mbili
Kuandaa mpango mkuu (comprehensive) wa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu wa kitaifa wa kukabiliana na janga au madhara ya janga la virusi vya corona (COVID 19) kukwamua taifa kiafya (afya ya jamii), kijamii na kiuchumi. Hadi sasa serikali ya CCM haijafanya chochote wakati wananchi wanakufa kimya kimya, uchumi unakufa kimya kimya na jamii inaathirika kimya kimya bila mwitikio wowote wa Kisera.

Namba Tatu
...
 

tindo

JF-Expert Member
Sep 28, 2011
33,825
2,000
Wengi wa wanasiasa tuko nao hapa jf, ila wanatumia fake I'd, labda useme waje na verified I'd. Hilo pendekezo lako namba moja usitegemee mabadiliko yoyote chini ya rais huyu, ila tegemea kuwa mbaya zaidi ya sasa. Yeye anaamini demokrasia ni kikwazo cha maendeleo. Kutokana na katiba yetu ilivyo, kitakachotekelezwa Ni kile anachokitaka na kukiamini.

Kwenye pendekezo lako namba mbili, utawala huu hautaki kusikia habari za Corona. Hivyo hakuna lolote litakalotekelezwa kwenye mapendekezo yako. Kwanza ni hatari hata kusema kuna huo ugonjwa hapa nchini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom