1. Juu ya Msamaha wa dhambi
Unahitaji kujua na kuwa na uhakika siku ile uliyotubu kumpokea Yesu Kristo kama Bwana na Mwokozi wako, dhambi zako ZILISAMEHEWA, ZILIFUTWA, WALA MUNGU HAZIKUMBUKI TENA.
Ndiyo Mungu hazikumbuki tena! Ndivyo neno lake linavyosema. Hebu tafakari mistari ifuatayo:
Haya, njooni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu (Isaya 1:18).
Tena Mungu alisema hivi katika Isaya 43:25;
Mimi, naam, mimi, ndimi niyafutaye makosa yako kwa ajili yangu mwenyewe; wala sitazikumbuka dhambi zako.
Mungu anasema hatazikumbuka tena dhambi zako! Sasa wewe kwa nini dhambi ulizokwisha kuzitubu bado zinakusumbua rohoni? Inakuwa kama vile Mungu hajakusamehe!
Lakini nakwambia ya kuwa ikiwa ulitubu katika roho na kweli umesamehewa dhambi zako wala Mungu hazikumbuki tena! Kwa hiyo na wewe usizikumbuke tena! Hata kama mawazo yako yanakuzomea hata kama wenzio wanakuzomea Mungu amekusamehe, wala hazikumbuki dhambi zako tena.
Unaweza ukasema, lakini ndugu Mwakasege, hiyo mistari iko katika agano la kale, Je! tuna mistari kama hiyo katika Agano Jipya?
Hiyo mistari ipo mingi tu lakini fahamu pia ya kuwa hiyo mistari ingawa iliandikwa wakati wa agano la kale ilikuwa inazungumza na watu walio katika agano jipya. Hii ni kwa sababu katika agano la Kale pamoja na sadaka zilizokuwa zinatolewa, Mungu alikuwa anazikumbuka dhambi zao. Soma Waebrania sura ya 8,9, na ya 10.
Katika agano jipya, yaana wakati huu, mtu anapookoka, damu ya Yesu Kristo iliyo mbele ya kiti cha enzi kwa ajili yetu inafuta hati zote zilizopelekwa na kuandikwa mbele za Mungu ambazo zilikuwa zimejaa dhambi zetu.
Ndiyo maana imeandikwa;
Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye; akiisha kutusamehe makosa yote; akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu, akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani (Wakolosai 2:13,14).
Tafsiri ya Kiswahili cha kisasa inasema hivi katika mistari hii ya Wakolosai 2:13,14;
Wakati mmoja nanyi mlikuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kwa sababu ninyi mlikuwa watu wa mataifa mengine. Lakini Mungu amewapa ninyi uzima pamoja na Kristo. Mungu ametusamehe dhambi zetu zote; alifutilia mbali ile hati ya deni iliyokuwa inatukabili na masharti yake, na kuifuta kabisa kwa kupigilia Msalabani.
Soma pia Waebrania 9:23 hati iliyotumwa mbinguni na shetani kukushitaki imefutwa! Shetani anapojaribu kukukumbusha juu ya dhambi za zamani ulizozifanya kabla ya kuokoka, ujue ameshika nakala tu ya hati, lakini hati yenyewe ilikwishafutwa kwa damu ya Yesu.
Mbele ya Mungu unaonekana huna kosa, kwa sababu hujasimama mwenyewe mbele zake lakini Yesu aliyekuokoa yuko pamoja na wewe kwa kuwa uhai wetu, umefichwa pamoja na Kristo katika Mungu (Wakolosai 3:3)
Hebu zidi kutiwa moyo na maneno yafuatayo yaliyomo katika Warumi 8:31-39 yanayosema: Basi, tuseme nini juu ya hayo? Mungu akiwapo upande wetu, ni nani aliye juu yetu?Yeye asiyemwachilia Mwana wake mwenyewe, bali alimtoa kwa ajili yetu sisi sote atakosaje kutukirimia na mambo yote pamoja naye? Ni nani atakayewashitaki wateule wa Mungu? Mungu ndiye mwenye kuwahesabia haki. Ni nani atakayewahukumia adhabu? Kristo Yesu ndiye aliyekufa; naam, na zaidi ya hayo, amefufuka katika wafu, naye yuko mkono wa kuume wa Mungu; tena ndiye anayetuombea.
Ni nani atakayetutenga na upendo wa Kristo?
. lakini katika mambo hayo yote tunashinda, na zaidi ya kushinda, kwa yeye aliyetupenda. Kwa maana nimekwisha kujua hakika ya kwamba, wala mauti, wala uzima, wala malaika, wala wenye mamlaka, wala yaliyopo, wala yatakayokuwapo, wala wenye uwezo, wala yaliyo juu, wala yaliyo chini, wala kiumbe kinginecho chote hakitaweza kututenga na upendo wa Mungu ulio katika Kristo Yesu Bwana wetu.
Nashukuru kwa hili. Ni changamoto kweetu sote. Kwani mara nyingi we are tempted to see the negative in us. Shetani anatuletea yale mabaya tuliyoyafanya na kutufanya tusahau kwamba dhambi zetu zilishasamehewa.
Hayo maneno yaliyopo kwenye kitabu cha Isaya yamenburudisha hadi mimi. Sijui kwa nini sikuwa nimeyakumbuka.
Nashukuruni kwa mchango wenu.
Ohh, shida nyingine wapendwa ni kuwa some of the men(actually to be precise wawili) bado wanamsumbua. na ameshawaambia hataki mahusiano nao. And imagine they are married guys!!!! Ni jambo gani anaweza kufanya ili waone yupo serious kweli? Mimi hili jambo ni very new kwangu na sijui nimsaidieje.