Mchango wa kuwafutarisha na kuwapa Iddi watoto mayatima Zanzibar!

Ngida1

JF-Expert Member
Aug 25, 2009
586
206
watoto wafutari.jpg

Baadhi ya watoto mayatima wakifutarishwa katika Ramadhani ya mwaka jana huko Zanzibar!


Ndugu Wapendwa,

Sote tunaifahamu hali ya maisha duni wanayopambana nayo baadhi ya watoto mayatima kule Zanzibar. Hatuwezi kuibadilisha hali yao hio, lakini tunaweza angalau siku moja kuwafutarisha vizuri katika hii Ramadhani ijayo na kuwapa mkono wa Eid siku ya Sikukuu.

Kwahivyo, ZANZIBAR-CANADIAN DIASPORA ASSOCIATION (ZACADIA) ya Toronto, Canada, inatoa wito kwa wote wanaoishi nje kuungana pamoja ili kuwafutarisha watoto hao mayatima na kuwapa mkono wa Eid siku ya Sikukuu.

Kama unaguswa na hali ya mayatima kule Zanzibar basi changia chochote unachokiweza ili watoto hao mayatima wafutari vizuri angalau hio siku moja katika Ramadhani ijayo na siku ya Sikukuu wapate mkono wa Idi.

Tafadhali changia and Allah will reward you, Inshaa Allah!

Hii kampeni itamalizika Ramadhani ya 10, ili kabla Ramadhani haijesha tupate muda wa matayarisho ya shughuli ya kufutarisha hao mayatima kule Zanzibar na pia kupata muda wa kuwanunulia nguo za Sikukuu, kwani hali zao kama mnavyoona pichani hapa juu ni taabani

Tuma mchango wako kwa muwakilishi ambae yupo karibu na wewe:


CANADA:

Hassan Othman @+1.647.404.8618 (Toronto)

Bi Shahida Hamad @+1.289.696.3089 (Toronto)

U. S. A

Mohammed Masoud @1.330.880.9524 (Ohio)

UNITED KINGDOM:

Miss Fauzia Karama @+44.7847.024.456 (Manchester)

Abdalla Juma (Dulla Ndende) @ +44.7909.225.287 (Milton Keynes)

CONTINENTAL EUROPE:

Dr. Muhammed Mwinyi Khami @ +46.70.426.9707 (Scandinavia / Sweden)

Nabil Salum (Nasser) / NASMO @ +32.487.28.39.96 (Belgium)

MIDDLE EAST:

Mohamed Omar @ +971.50.424.6878 (Dubai, U.A.E)

Ali Said Ali @+968.9.509.7454 (Muscat, Oman)

FAR EAST:

Suleiman Ali Al Rawahy @+81.80.4027.3510 (Japan)


Source: zacadia.com
 
Inshaallah
Ila kwa ninavyojua mie Hao wana Ofisi Zanzibar na Muwakilishi wao Zanzibar
Halafu unaposema Nje,kwa Nchi hizo chache ni kutenga baadhi ya watu kwenye Nchi nyingine.
Maana hata Bara huko Tanganyika ni Nchi nyingine na hata watanzania sie kwa sie tunauwezo wa kufanya hivyo na kuongeza Nguvu kwa ZANZIBAR-CANADIAN DIASPORA ASSOCIATION (ZACADIA).
Sadaka haingalii upo wapi,sasa nahisi wangeweka pia nafasi kwa watu wote tu kuchangia bila kujua unaishi nje au la then hilo la hizo Nchi likawa pia kama ziada hapo juu.
Na ukizingatia hao ZACADIA wana Ofisi Zanzibar na muwakilishi wao hapa Zanzibar,sasa ingekuwa busara pia kuweka Number zao,maana sio kila mtu aliepo huko akachangia hukuhuko ili kukwepa Gharama za kutuma pesa mara mbili.Kwakuwa mwisho wa siku pesa zote zitatakiwa kufika Zanzibar.Maana baadhi ya wanaoishi Nje wapo Zanzibar kwa mapumziko na kutumia mwezi wa ramadhani wakiwa hapa
Ni Ushauri tu
Pia nawapongeza ZACADIA kwa kuchangia vifaa miezi kadhaa iliyopita,na pia kwa michango yao miiingia mbayo wamekuwa wakichangia kwa Zanzibar
 
Back
Top Bottom