Wont be the same
JF-Expert Member
- Aug 15, 2024
- 1,564
- 2,483
Mwenyekiti wa Kituo cha Wanahabari Watetezi wa Rasilimali na Taarifa (MECIRA) na Mkurugenzi wa Jamvi Media Group, Habibu Mchange, amepongeza juhudi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) katika kudhibiti vitendo vya rushwa, hasa kuelekea uchaguzi mkuu.
Akizungumza na gazeti la Jamvi la Habari, Mchange ambaye pia ni kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) amesema kuwa hatua zinazochukuliwa na TAKUKURU ni muhimu katika kuhakikisha taifa linapata viongozi waadilifu wasiopata madaraka kwa kutumia pesa kwani baadhi wamekuwa wakidaiwa ‘kujipitishapitisha’ kabla ya wakati wa kampeni na uchaguzi.
"Kitendo cha TAKUKURU Kigamboni kutilia mashaka mtu, watu au kikundi cha watu ni haki na wajibu wao. Na kufanya hivyo kutasaidia kuliondoa taifa kwenye hatari ya kupata viongozi wanaoamini katika matumizi ya pesa kupata uongozi," amesema.
Kauli hiyo ya Mchange inakuja siku chache baada ya kudaiwa kushikiliwa na TAKUKURU Kigamboni kwa saa kadhaa. Inaripotiwa kuwa aliitwa Ijumaa saa tatu asubuhi, baada ya siku ya Alhamisi kukaa ofisini kwa taasisi hiyo hadi saa saba usiku. Tukio hilo lilitokea muda mfupi baada ya magazeti yake kuripoti kuwa TAKUKURU iliwafungia ofisini viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) kata ya Tungi, wilayani Kigamboni.
Pamoja na hali hiyo, Mchange amesisitiza kuwa anaunga mkono juhudi za vyombo vya dola katika kukabiliana na vitendo vinavyoweza kuhatarisha upatikanaji wa viongozi bora.
"Ninawaomba waongeze kasi na wasiangalie mtu usoni. Ni jambo la kupongeza kuona vyombo vya dola vinakemea michezo inayoweza kupelekea kukosekana kwa viongozi bora, nawaunga mkono na nipo tayari kuwapa kila aina ya ushirikiano kuhakikisha malengo yao yanafikiwa," ameongeza.
Aidha, ameeleza kuwa mafanikio ya TAKUKURU ni mafanikio ya taifa katika kujenga jamii inayopinga na kukataa rushwa.
"Kufanikiwa kwa malengo yao ndiyo kufanikiwa kwa taifa kupata jamii inayokataa, kuchukia na kukemea rushwa na viashiria vyake. Kwa hili nawapa kongole," amesema Mchange, akisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana na taasisi hiyo katika kupambana na rushwa.