Azathioprine
JF-Expert Member
- Sep 16, 2013
- 588
- 371
Zinaweza kupungua kama kanuni hizi zitapita!
1. Posho zitolewe baada ya kikao/shughuli za bunge kwa siku husika kuisha
2. Mbunge akitolewa nje kwa kuzomea, kupiga kelele au kukaidi amri ya Spika hatoruhusiwa
kukaa/kusogelea maeneo ya bunge (yale yale ya mita 200)
3. Mbunge atakayetolewa nje hatalipwa posho ya kikao husika
4. Mbunge akitolewa nje azuiwe kuhudhuria kikao kinachofuatia (Nani akose posho mara x2)!
5. Ikifanyika hivyo mara 3 kwa mbunge kwa mkutano mmoja wa bunge, Mbunge atazuiwa kuhudhuria vikao
vyote vilivyo salia vya mkutano husika!
6 Mbunge atakaye zuiwa kuhudhuria vikao vilivyo salia atatangwa bungeni ili asipooneka Jimboni
kwake, wananchi wajue huyo kabaki Chako ni Chako anatafuna filigisi!
Hizo kanuni nazo sio rafiki kwa watanzania maskini.
Hakuna sababu ya kumlipa mbunge Posho ya kikao Wakati yupo pale kutumiza majukumu yake aliyopewa na wananchi. Mshahara wa mwisho wa mwezi ndio stairi yake Kama mtumishi wa Umma.