MCHAMBO WA LEO:MAJI YA BAHARI HAYAPIKIWI CHAI

Kanungila Karim

Verified Member
Apr 29, 2016
16,603
2,000
HALOOOO eeeehhh! Unajifanya barafu umesahau kama unayeyuka! Wee ringia sura siye tunaringia ngozi! Shoga nashanga unalamika oooh mambo yako hayaendi si uende wewe! Heee eheeeiyaaaaa! Kama ulikuwa hujui mchawi mtu paka katu-mwa tu, upo? Wanakwambia usilaze sukari chumba cha watoto na hausigeli hafui nguo za baba, akifua basi ujue mke mwenza huyo! Shoga tangu lini muuza mkaa akaoga mchana? Weee haya tu maana nakuona unasha-ngaa dagaa kuanikwa juani unasahau hata nguo nazo zaanikwa!


Tenaaaa! Shoga usinione leo nipo hivi ukadhani Anti Naa amechangamka, atapunguza kuchamba! Unitue bibi weee! Leo nipo na nyie kinamama mnaofuga kucha ndefu kama mnaenda vitani.


Utakuta limama limefuga kucha kama linaenda kwenye mashindano unabaki unajiuliza hivi huyu hata kufua nguo anaweza, kupika je? Haya basi na akiwa na babaa usiku si anaweza kugeuka zombi amparue, wareeee reeee! Shoga siku zote nikiongea huwa namaanisha ati! Wengine wanalia kuachika kumbe wamejitakia wenyewe, wewe unafuga mikucha kazi zote umemrundikia hausigeli kuanzia kufua nguo za mumeo za ndani na nje hadi kuwapikia chakula unadhani kwa nini asichepuke?


Ngoja nikung’ate sikio shoga yangu! Mwanamke siyo kama hatakiwi kufuga wala kubandika kucha ila unaangalia na majukumu mengine utafanyaje? Mfano miye shoga nimefuga lakini siyo kooote na tena siyo ndefu! Najua jinsi ya kukabiliana na shemeji yako kuanzia juu hadi chini, upo nyonyo?Kuna wengi wanabandika tu wao huwezi kukuta wanafuga tu ilimradi wawepo kwenye kundi la wasichana wenye kucha lakini ukiwakuta kwenye kumi na nane zao, mboooooonaaaa! Shoga kati ya vitu unavyotakiwa kutofanya ni kumpa nafasi hausigeli wako amfulie nguo babaaa, mbaya zaidi unampa ruhusa anaingia hadi chumbani kwako kufanya usafi wakati wewe upo na unaweza kufanya vyote hivyo!


Mahausigeli wa siku hizi siyo wa zamani! Ndiyo maana nikasema maji ya bahari hayapikiwi chai! Huwezi kumpa asilimia zote mwisho wa siku ukaja kunililia kuwa amekusaliti, ukija kuchunguza unakuta sababu ni ndogo kama hii ya kuwa na mikucha mirefu unamuachia kazi za kufua nguo za baba!
 

Nyange

JF-Expert Member
Mar 25, 2010
3,455
2,000
We utakuwa wa msoga, make kucmba kama unakodishwa vile shoga
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom