Mchakato wa ufutaji hatimiliki za ardhi ambazo hazitumiki: Vigogo wadaiwa kutumia wanyonge ili wavitumie kwa maslahi yao

Mzee mende

Member
May 29, 2020
33
29
Mchakato wa ufutaji hatimiliki za ardhi ambazo hazitumiki unadaiwa kuingiliwa na baadhi ya matajiri wanaotumia wanyonge ili wavitumie viwanja kwa maslahi yao. JAMHURI lina taarifa kwamba katika orodha ya hatimiliki za ardhi zilizowekwa mezani kwa Rais John Magufuli kwa ajili ya kufutwa, zipo za watu ambao hadi sasa hata hawana habari kwamba umiliki wao wa ardhi unakaribia kufutwa. Na kwamba jambo pekee linalowaokoa ambao hawajafutiwa hadi sasa ni umakini wa Rais Magufuli, ambaye shughuli hii huifanya kwa uangalifu na umakini mkubwa.

“Hao ambao hatimiliki zao zinatakiwa kufutwa wanapaswa kumshukuru sana Dk. Magufuli, kwa sababu jambo hili halifanyii haraka. Anajipa muda na kuwasiliana na vyanzo vyake mbalimbali vya taarifa. “Angekuwa ni mtu wa kupokea tu taarifa na kusaini, watu wengi wangekuwa wamekwishaumia na wengine wengi wangeendelea kuumia kila mwaka. “Kwa sasa yeye ndiye tegemeo la wanyonge ambao wangeumizwa na tabia hii mpya ya matajiri kuingilia mchakato huo wa ardhi ili wayatumie maeneo ya watu wengine kwa faida binafsi,” anasema ofisa mmoja wa Manispaa ya Mpanda mkoani Katavi katika mahojiano na JAMHURI.

Ofisa huyo ametoa mifano ya mashamba kadhaa ndani ya Mkoa wa Katavi yanayodaiwa kuwa katika hatari ya kufutiwa umiliki, hati zake zikidaiwa ama kuandaliwa kuwekwa mezani kwa Rais, au tayari zinasubiri saini ya kiongozi huyo mkuu wa nchi. Mbali na Katavi, JAMHURI lina mfano wa kiwanja chenye hatimiliki namba 35871, kilicho katika kitalu namba 270, eneo la Viwanda, Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, ambacho tayari hati yake imewekwa mezani kwa Rais kwa ajili ya kufutwa matumizi, kwa maelezo kwamba hakijaendelezwa na aliyekuwa akikimiliki.

Hata hvyo, JAMHURI lilipotembelea eneo hilo limekuta shughuli kadhaa zikiendelea, yakiwapo makontena; ishara kuwa mmiliki halali wa sasa analitumia (au kuliendeleza) eneo ambalo umiliki wake umo katika hatihati ya kufutwa. Eneo hilo lenye huduma za maji na umeme, pia limezungushiwa uzio na mmoja kati ya wafanyakazi 10 waliopo hapo anasema makontena hayo yanatumika kuhifadhi vifaa mbalimbali, ingawa hakubainisha ni kwa matumizi gani.

Wasamaria wema ambao ni majirani wa eneo hilo wameliambia JAMHURI kuwa kuna mchezo mchafu unafanywa na mmoja wa matajiri walio na ardhi maeneo hayo (jina tunalihifadhi) anayetaka kulitwaa kwa manufaa yake. “Hapa sisi tunamjua mmiliki wa hili eneo. Huwa anakuja, na ni jirani yetu. Watumishi wa Wizara ya Ardhi wenye nia njema wametutonya kwamba Rais amepelekewa faili ili abatilishe umiliki halali wa kiwanja hiki. “Huyu jirani mwingine ambaye ni tajiri anapambana liwe ‘open space’ (eneo LYAMBA-LYA-MFI- ushawishi wao serikalini kufuta hati za NA JOE BEDA RUPIA la wazi); kwamba anapanga kufungua ‘supermarket’ lakini anadhani kutakuwa na shida ya maegesho ya magari ya wateja. Ndiyo maana hiyo open space anaitaka kwa ajili ya maegesho.

“Hatari tunayoiona mbele yetu ni kwamba akifanikiwa kuchukua eneo hilo, hata sisi hatutakuwa salama. Anaweza kutufanya anachotaka, kwa kuwa tabia mbaya huwa haina dawa,” anasema jirani mmoja na kuongeza kuwa hofu hiyo ndiyo imesababisha wao kulitaarifu JAMHURI, kwa kuwa ni kama tajiri huyo anamweka Rais mtegoni.

JAMHURI limeelezwa kuwa eneo hilo ni la mita za mraba 885 na taarifa kutoka Wizara ya Ardhi zinaonyesha kuwa lilinunuliwa mwaka 1989; likipewa umiliki wa miaka 99 kuanzia Julai 1, 1989. Hizi ni taarifa kutoka eneo moja tu la Tanzania, mbali na Katavi ambako gazeti hili halikuweza kuyatembelea maeneo husika, na tayari linazua maswali mengi kuhusu namna ‘zoezi’ zima la ufutaji wa hatimili za ardhi kwa watu; hasa wanyonge, linavyoendeshwa.

Iwapo eneo lililo barabarani kabisa ndani ya Jiji la Dar es Salaam linaweza kubadilishwa matumizi na kufutwa, itakuwaje kwa maeneo yaliyo mikoani ambako pia wapo matajiri wenye tamaa ya ardhi za wanyonge? Ni bahati mbaya kwamba majirani hao wamekuwa na hofu ya kuandikwa majina yao gazetini wakidai kuwa huenda tajiri mhusika ana marafiki ambao ni ‘wakubwa’ serikalini, hivyo anaweza kuhamishia hasira zake kwao Simu: 0653 336 490.

“Watendaji wanaomsaidia Rais katika masuala ya ardhi wanapaswa kuwa makini. Watu wanaonewa sana. Wanaporwa ardhi kwa hila.
“Rais Magufuli ni mtetezi mzuri wa wanyonge, lakini hawezi kujua kila kitu! Ni kweli kwamba kuna maeneo mengi nchini ambayo watu wameyanunua lakini hayatumiki na ni vizuri kuyagawa kwa watu wengine wenye uwezo wa kuyaendeleza. “Lakini kwa hapa kwetu mtu anamiliki eneo halali, analiendeleza na analipa kodi zote kwa serikali kila mwaka kama inavyotakiwa; leo serikali kufuta hatimili na kukifanya kuwa eneo la kuegesha magari, si kwamba itapoteza kodi inayopata kila mwaka, lakini itakuwa pia imemfukarisha mmiliki. “Huu ni uonevu. Sisi tunaumia kwa sababu tabia hii ni mbaya na haifai itasababisha chuki za bure kwa Rais.

Bahati mbaya ni kwamba haya mambo yako mezani kwake (Ikulu), lakini kwa kuwa bado Rais anafanya mapitio na hajaanza kufuta, upo uwezekano wa kumsaidia jirani huyu. “Jambo baya ni kwamba mwenye kiwanja hajapewa taarifa rasmi kwa maandishi; walau kuambiwa tu kuwa; ‘jiandae, kuna hili huenda likatokea’. Ni kama vile anaviziwa. Sasa na sisi majirani tuna wasiwasi nini kitafuata,” anasema jirani huyo.

JAMHURI linafahamu kuwa sheria au taratibu zilizopo haziruhusu ujenzi wa maduka eneo la viwanda na sasa linamtafuta ‘tajiri’ huyo kufahamu ukweli wa mambo.

Shughuli zikiendelea kat
 
Tajiri ‘ambipu' JPM

Na Mwandishi Wetu

MCHAKATO wa ufutaji wa vibali vya ardhi ambazo hazitumiki unadaiwa kuingiliwa na baadhi ya matajiri ambao hutumia ushawishi wao serikalini kufuta vya wanyonge ili wavitumie kwa matumizi yao.

JAMHURI lina taarifa kwamba katika orodha ya vibali vya ardhi vilivyowekwa mezani kwa Rais John Magufuli kwa ajili ya kufutwa, vipo vya watu ambao hadi sasa hata hawajui kwamba umiliki wao wa ardhi unakwenda kufutwa.

Gazeti hili linafahamu kwamba jambo pekee linalowaokoa wale ambao hawajafutiwa vibali vyao hadi sasa ni umakini wa Rais Magufuli ambaye zoezi hili hulifanya kwa uangalifu.

"Hao wanaotakwa kuvuliwa vibali vyao wanatakiwa kumshukuru sana Ras John Magufuli kwa sababu halifanyi jambo hili kwa haraka. Anajipa muda na ana vyanzo vyake vya taarifa.

Angekuwa ni mtu wa kupokea tu taarifa na kusaini, watu wengi wangekuwa wanaumia kila mwaka. Yeye sasa ndiye tegemeo la wanyonge wengi ambao wangeumizwa na tabia hii mpya ya matajiri kungilia mchakato huo wa ardhi ili watumie maeneo ya watu wengine kwa faida yao.

JAMHURI lina mfano wa kiwanja chenye hati namba 35871, kilicho katika kitalu namba 270 kilichopo eneo la viwanda la Mbez Beach jijin Dar es Salaam ambacho sasa kimewekwa mezani kwa Rais kwa ajili ya kufutwa matumizi kwa maelezo kwamba hakijaendelezwa na aliyekuwa akikimiliki.

Hata hvyo, JAMHURI limefanya ziara katika eneo kiliko kiwanja hicho na kukuta kuna shughuli zinaendelea, kuna makontena yamewekwa kwa ajili ya shughuli za baadaye za mmiliki halali wa kiwanja hicho lakini ndiyo tayari umiliki wake uko hatarini kufutwa.

Wasamara wema ambao wanaishi katika eneo hilo ndiyo waliotoa taarfa kwa gazeti hili kwamba kuna mchezo mchafu unataka kufanywa na mmoja wa matajiri walio na ardhi katika eneo hilo kutwaa eneo la mwenzake ili kujinufaisha mwenyewe.

“ Sisi tunamjua mmiliki wa hili eneo. Huwa anakuja hapa na ni jirani yetu. Sasa tumetonywa na watumishi wasafi wa Wizara ya Ardhi kwamba umiliki wa hicho kiwanja unaweza kubadilishwa wakati wowote na Mhe Rais na kwamba faili liko mezani kwake Ikulu.

“ Kuna tajiri anapambana hili eneo la mwenzake liwe open space (eneo la waz). Yeye tumeambwa anataka kufungua Super Market hapa na lengo lake anataka hiyo open space itumike kama eneo la kuegeshea magari ya watu watakaokuwa wakija kununua vitu kwake.

“ Kinachotutisha ni kwamba huyu bwana leo kaanza na mwenzetu hapa. Akifanikiwa, hatujui atafanya nini kwa sisi majirani zake wenzake. Unajua taba mbaya haina dawa na ndiyo sababu tumeamua kukuita ndugu mwandishi ili muandike na hatmaye Mhe Ras ajue kwamba kuna watu wanamtegeshea mabomu, alisema mmoja wa majirani hao.

Eneo hilo ambalo JAMHURI lilifanikiwa kuliona lina ukubwa wa mita za mraba 885 na taarifa kutoka Wzara ya Ardhi zinaonyesha lilinunuliwa mwaka 1989 kwa kibali cha miaka 99 kuanzia Julai Mosi, 1989.

Taarifa hizi kutoka katika eneo moja tu la Tanzania, linazua maswali mengi kuhusu namna zoezi zima la ufutaji wa vibali vya umiliki wa ardhi kwa watu; hasa wale wanyonge linavyoendeshwa.

Kama eneo lililo barabarani kabisa jijiji Dar es Salaam linaweza kubadilishwa matumizi na kufutwa, itakuaje kwa maeneo yaliyo mbali na Dar es Salaam na kwingine ambako kuna matajiri wenye tamaa ya ardhi za wanyonge.

Majirani waliozungumza na JAMHURI kwa masharti ya kutotajwa majina yao kwa maelezo kwamba inaonekana tajiri anayetaka eneo la mwenzake ana marafiki katka ngazi za juu na anaweza kuhamishia hasira zake kwao, wameeleza kwamba Rais na watendaj wake wanatakiwa kuwa makini kwenye kufuta vibali vya umiliki ardhi vya wananchi.

“ Ras wetu anatetea sana wanyonge lakini hawezi kujua kila kitu. Ni kweli kwamba kuna maeneo mengi hapa nchini ambayo watu wameyanunua lakini hayatumiki na ni vizuri kugawa kwa watu wengine wenye uwezo wa kuendeleza.

“Lakini, kwa hapa kwetu, mtu anamiliki eneo halali, analiendeleza na amelipa kod zote kwa serikali kila mwaka kama anavyotakiwa na serikali inapokea kodi. Leo serikali kufuta kibali na kukifanya kuwa eneo la kuegesha magari, si kwamba itapoteza kodi inayopata kila mwaka, lakini itakuwa pia imemfukarisha mtu aliyenunua eneo.

“ Huu ni uonevu. Sisi tunaumia kwa sababu tabia hii ni mbaya na haifai. Watu watakuwa wanamchuka Rais wao pasipo sababu wakati kosa ni la watu wengne kabisa. Kwanza tuna bahati kwamba haya mambo yako mezani kwake Dodoma lakini bado Rais anafanya mapitio na hajaanza kufuta bado.

“ Jambo baya ni kwamba mwenye kiwanja hajapewa taarifa rasmi kwa maandishi kwamba eneo lake litafutwa na kubadilishwa matumizi hadi sasa. Barua tu hajapewa. Ile kuambiwa tu bwana wewe kuna hili linakuja. Ni kama vile anaviziwa. Sasa na sisi majirani tuna wasiwasi nini kitafuata, alisema mmoja wa majirani wa eneo lenye mgogoro.

Jambo lingine ambalo gazeti hili limeambiwa na wasamaria wema hao ni kwamba eneo lao hilo ni la viwanda na kwamba ujenzi wa kitu kama maduka ni tofaut na matumizi sahihi kwa sababu duka si kiwanda.

Gazet hili linaendelea na uchunguzi wake kuhusu jambo hili kwa kuzungumza na wahusika wote na kuona nakala halisi za vibali lakini kwa sababu ya ukweli kwamba Rais anaweza kubatilisha vibali vya sasa wakati wowote, limeona umuhmu wa kutoa taarifa hii mapema.

Mwisho
 
Watu aina hii ya huyu mfanya biashara anayetaka kudhulumu wenzake haki ya kumiliki ardhi ndio waliokuwa wakitamba miaka ya nyuma, sasa hizo nafasi hazipo tena lazima walalamike.
 
Hilo gazeti linafanya habari za kichunguzi, sawa.

Ila lilishindwa kufanya habari ya kichunguzi dhidi ya mauaji ya muandishi wa habari Azory Gwanda, Mwanaharakati Ben Saanane na watu waliopotea katika mazingira ya kutatanisha na kuogofya katika utawala wa Serikali ya Magufuli.
 
Back
Top Bottom