Mch. Rwakatare avunjiwa nyumba

Soma post yako niliyorespond kwake. Naona unaandika vitu halafu unasahau.


 

Mkuu sema mwizi wa umeme kavunjiwa nyumba zake, mheshimiwa mwenye uchungu na nchi yake huwa anafanya mambo yake kiuadilifu na kufuata sheria na taratibu zote za nchi. Hilo gume gume rwakatare lilihonga wanawake chain za dhahabu ili apate viti maalum apate kufanya dhulma anazozifanya. Shame on her!


Sent from my iPad using JamiiForums
 

Wewe ungekuwa ni mpembuzi ungeitafuta kwanza hii sheria usome. Sasa hapa unataka kuleta ubishi wakati hujasoma hichi kipengele kimeandikwaje. Sheria sio novel, inaandikwa kwa misingi ya natural justice. Lazima sheria inamtaka apewe notice, then aondoe au avunje kwa ridhaa yake akikaidi commissioner kapewa mamlaka ya kuondoa. Ndugu huwezi kuwa na facts kama hutosoma. Hakuna hata sehemu moja nimesema commissioner yupo juu ya sheria, nakushangaa unavyonilisha maneno. Narudia tena, nakushangaa unavyomtetea huyu mama ambaye yeye ndo alikiuka amri ya baraza la ardhi. Na sijui hiyo court order unayosema ilitolewa imeitoa wapi, maana gazeti hilo unalolisema wameandika kesi ipo mahakamani.
 

Sikubaliani na non sensw yako!!! Kwahiyo wewe unaenda safari, nakuja nawatoa vijana wako ndani mwako. Nasema hii nyumba ni yangu. Then unakuja unakuta ulinzi mkali. Unaenda mahakamani. Then wanasema nyumba ni yako kisheria. So, i mean time mimi nikaongeza ongeza hapo. Je utanilipa? Nikuachie nyumba yako? Hakuna laws au such mitigating tacts za aina hii hata siku moja. Haki ni haki yake !


The King.
 
Hiv vitu vickie tu,halaf pita kimya mtu akuvunjie mjengo kama hizo picha,unaweza ukapiga mtu risasi au ukamroga kabisa,au ikishindikana ukatafuta wauaji wa kukodi,watu wanashabikia kama vile sheria iliyovunjwa ni hiyo tu mbona ziko nyingi imagine ni ww halaf ukoment,mtu hata kibanda cha njiwa hujawah kujenga unajifanya bush lawyer,hiv sehem kiasi gan ya tz imepimwa ili tusijenge ovyo ovyo,cku zote akili ya watu weusi ni kurudishana nyuma ili wote tukose,mtu anayebomoa anajua cost ya hiyo decra.
 
[h=2]Mch. Rwakatare avunjiwa nyumba[/h]
Rungu la Sheria limetua kwa Mch.Gertrude Rwakatare,Mchungaji Kiongozi wa 'Mlima wa Moto'.Ni nyumba yake iliyokuwa Mbezi Beach. Alijenga katika eneo la mjane alilolivamia. Hatimaye sheria imechukua mkondo wake. Mjane alilia kwa furaha. Nyumba hiyo ilisajiliwa kwa jina la mtoto wa Mch.Rwakatare. Uboboaji huo ulifanywa chini ya ulinzi mkali wa askari waliokuwa wamesheheni silaha za moto.

Wakati wa ubomoaji,alijitokeza mtu mmoja aliyedai kuwa ni Wakili wa mwenye nyumba akiwa na nyaraka za kimahakama zinazodaiwa kuweka zuio la kubobolewa kwa nyumba hiyo.Hatahivyo,alipuuzwa na ubomoaji kuendelea kama ulivyopangwa. Kweli sheria ni msumeno!

Chanzo: ITV


Serikali yabomoa nyumba za mamilioni Mbezi Beach




Katapila likibomoa moja ya nyumba nne za Tibe John katika eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam jana.
Picha na Beatrice Moses.
​

Na Beatrice Moses na Ally Nguba, Mwananchi


Kwa ufupi

Nyumba hizo zilizokuwa katika Kitalu namba 314 chenye mgogoro wa umiliki, zilikuwa zinajengwa na John kwa kasi bila kujali kuwa kulikuwa na amri ya Baraza la Ardhi ya kuzuia ujenzi huo hadi mgogoro uliohusu eneo hilo utakapotatuliwa.


Dar es Salaam.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imebomoa nyumba nne zenye thamani ya Sh800 milioni mali ya Tibe K. John zilizojengwa katika eneo la Mbezi Beach bila kibali na kinyume na sheria za mipango miji.


Nyumba hizo zilizokuwa katika Kitalu namba 314 chenye mgogoro wa umiliki, zilikuwa zinajengwa na John kwa kasi bila kujali kuwa kulikuwa na amri ya Baraza la Ardhi ya kuzuia ujenzi huo hadi mgogoro uliohusu eneo hilo utakapotatuliwa.

Wakati wa ubomoaji huo uliosimamiwa na Manispaa ya Kinondoni chini ya Mhandisi Baraka Mkuya, kulikuwa na ulinzi mkali wa polisi wenye bunduki na mabomu ya machozi, wakiongozwa na Ofisa wa Operesheni, Emmanuel Tille.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Alphayo Kidata alisema kuwa ametoa agizo hilo kwa sababu sheria zinapaswa kuzingatiwa na kwamba nyumba hizo zilijengwa bila kuwa na kibali chochote cha manispaa kama inavyotakiwa.

“Kuwapo kwa kesi mahakamani hakuzuii sheria nyingine kutekelezwa, wamejenga hawana kibali,” alisema Kidata.

Wakili wa John, Emmanuel Augustino alidai kwamba hatua hiyo imetekelezwa kibabe na katibu mkuu, kwa kuwa kuna kesi wamefungua katika Baraza la Ardhi Kinondoni ambayo inaendelea kusikilizwa.

“Anajua wazi kuwa alichokifanya ni kinyume cha sheria, ameingilia uhuru wa mahakama,” alisema.

Augustino alisema hawajui watamshtaki nani ili kudai fidia, hasa kwa kuwa katibu mkuu alitoa agizo la mdomo na hakuna barua yoyote aliyoandika ambayo ingeweza kutumika kama ushahidi.

Wakili wa anayedaiwa kuwa mmiliki wa kiwanja hicho cha Janet Kiwia, ambaye ni Howard Msechu kutoka katika Kampuni ya Uwakili ya Homac, alisema wamefurahishwa na hatua hiyo kwa sababu walikiuka amri ya Baraza la Ardhi ya kupiga marufuku shughuli za ujenzi kuendelea.


CHANZO: Mwananchi​
​
 
Hawa Manabii wa CCM wanakera sana... hata Wajane wanawavamia na kuwadhulumu?... Kwani biashara zake za Sembe hazimtoshi?...
 
Hawa Manabii wa CCM wanakera sana... hata Wajane wanawavamia na kuwadhulumu?... Kwani biashara zake za Sembe hazimtoshi?...
mkuu nadhani pia ni muda muafaka kubomoa Mbowe club aka billcanas. iludishwe NHC. Ruzuku anazojilipa zinamtosha Dj Zero.
 
Ukishaamua kuuza sembe mjane ni kutu gani......huku ukuhubiri neno kwa mapovu mengi.
 
Yap, nimeipenda analysis yako, definitely utakuwa lawyer by profession?
 
Hii ndio hasira ya kiyahudi akimwaga mboga mwaga ugali toboa na sufuria asirudi jikoni kupika tena
 
Kwahiyo unatuambia tufanyeje!

Kwani kila siku habari zikiletwa humu zinakuwa zinataka watu wafanyeje? Hahahaha wewe utakuwa unasali Milima ya Moto wewe pole sana.Maana ya habari kuletwa humu ni kupashana matukio yanayotokea kila pande nne za dunia.By the way wewe kwa nini unaangali taarifa ya habari ama unasoma magazeti?
 
Hivi kuliko hii sheria ya kuvunja nyumba kwa nini isingekuwepo nyingine ambayo kama wewe umedhulumu kiwanja cha mwenzako na mahakama imetoa hukumu, sasa hukumu ingekuwa badala ya kuvunja nyumba iliyopo ni bora mlalamikaji apewe hiyo nyumba sababu ilijengwa kwenye kiwanja chake, akishapewa hapo sasa ni maamuzi yake, aishi ama avunje, kuliko kupoteza nguvu na mali bure na kutiana umaskini wa buure, Mfano huyo mama mjane tayari angeshajipatia mtaji wa kutosha, angemalizia tu kisha angepangisha nyingine na pia angetoa ajira na kodi pia angelipa sirikalini, sasa wamevunja hapo huenda huyo mama hana hata uwezo wa kusimamisha hata nyumba ya vyumba viwili vya haraka, hebu tubadilike jamani, lile lilikua booonge la mtaji kwa mama.
Mbona polisi wakikamata magari ya ujambazi na yakikaa muda mrefu bila kuja kutambuliwa na wenyewe hatusikii kama yalichomwa moto ama kuvunjwa vipande?
Huko ni kuirudisha nchi yetu nzuri nyuma.
 
Mbona picha inaonyesha vinavyovunjwa ni vibanda tu, hekalu (pichani) mbona halionekani likivunjwa??
Hapa nami machale yananicheza pia, mwenye picha kamaili atueleze vizuri tafadhali.
 
Kwahiyo unatuambia tufanyeje!

Kweli anataka kutuelimisha nini? Rwakatare amevunja sheria na amepata haki yake. Pia ni kweli pia kwamba kesi kuwa mahakani haizui Mahakama kuvunja nyumba ambazo zimejengwa kimakosa
 
safi sna hii ni kuonyesha uwajibikaji wa viongozi :::::::tunahitaji nchi hii iendeshwe kwa mifano hii kila idara tutafika
 
Mahakama zisigeuzwe kichaka cha waharifu kubuy time, hili ni fundisho kwa wote

Copy: Zitto
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…