Mch. Rwakatare avunjiwa nyumba

Mch. Rwakatare avunjiwa nyumba

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Joined
Dec 27, 2012
Posts
10,346
Reaction score
26,138
Rungu la Sheria limetua kwa Mch.Gertrude Rwakatare,Mchungaji Kiongozi wa 'Mlima wa Moto'.Ni nyumba yake iliyokuwa Mbezi Beach. Alijenga katika eneo la mjane alilolivamia. Hatimaye sheria imechukua mkondo wake. Mjane alilia kwa furaha. Nyumba hiyo ilisajiliwa kwa jina la mtoto wa Mch.Rwakatare. Uboboaji huo ulifanywa chini ya ulinzi mkali wa askari waliokuwa wamesheheni silaha za moto.

Wakati wa ubomoaji,alijitokeza mtu mmoja aliyedai kuwa ni Wakili wa mwenye nyumba akiwa na nyaraka za kimahakama zinazodaiwa kuweka zuio la kubobolewa kwa nyumba hiyo.Hatahivyo,alipuuzwa na ubomoaji kuendelea kama ulivyopangwa. Kweli sheria ni msumeno!

Chanzo: ITV

Serikali yabomoa nyumba za mamilioni Mbezi Beach


mbezi.jpg


Katapila likibomoa moja ya nyumba nne za Tibe John katika eneo la Mbezi Beach, Dar es Salaam jana.
Picha na Beatrice Moses.

Na Beatrice Moses na Ally Nguba, Mwananchi


Kwa ufupi

Nyumba hizo zilizokuwa katika Kitalu namba 314 chenye mgogoro wa umiliki, zilikuwa zinajengwa na John kwa kasi bila kujali kuwa kulikuwa na amri ya Baraza la Ardhi ya kuzuia ujenzi huo hadi mgogoro uliohusu eneo hilo utakapotatuliwa.


Dar es Salaam.

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imebomoa nyumba nne zenye thamani ya Sh800 milioni mali ya Tibe K. John zilizojengwa katika eneo la Mbezi Beach bila kibali na kinyume na sheria za mipango miji.


Nyumba hizo zilizokuwa katika Kitalu namba 314 chenye mgogoro wa umiliki, zilikuwa zinajengwa na John kwa kasi bila kujali kuwa kulikuwa na amri ya Baraza la Ardhi ya kuzuia ujenzi huo hadi mgogoro uliohusu eneo hilo utakapotatuliwa.

Wakati wa ubomoaji huo uliosimamiwa na Manispaa ya Kinondoni chini ya Mhandisi Baraka Mkuya, kulikuwa na ulinzi mkali wa polisi wenye bunduki na mabomu ya machozi, wakiongozwa na Ofisa wa Operesheni, Emmanuel Tille.

Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Alphayo Kidata alisema kuwa ametoa agizo hilo kwa sababu sheria zinapaswa kuzingatiwa na kwamba nyumba hizo zilijengwa bila kuwa na kibali chochote cha manispaa kama inavyotakiwa.

"Kuwapo kwa kesi mahakamani hakuzuii sheria nyingine kutekelezwa, wamejenga hawana kibali," alisema Kidata.

Wakili wa John, Emmanuel Augustino alidai kwamba hatua hiyo imetekelezwa kibabe na katibu mkuu, kwa kuwa kuna kesi wamefungua katika Baraza la Ardhi Kinondoni ambayo inaendelea kusikilizwa.

"Anajua wazi kuwa alichokifanya ni kinyume cha sheria, ameingilia uhuru wa mahakama," alisema.

Augustino alisema hawajui watamshtaki nani ili kudai fidia, hasa kwa kuwa katibu mkuu alitoa agizo la mdomo na hakuna barua yoyote aliyoandika ambayo ingeweza kutumika kama ushahidi.

Wakili wa anayedaiwa kuwa mmiliki wa kiwanja hicho cha Janet Kiwia, ambaye ni Howard Msechu kutoka katika Kampuni ya Uwakili ya Homac, alisema wamefurahishwa na hatua hiyo kwa sababu walikiuka amri ya Baraza la Ardhi ya kupiga marufuku shughuli za ujenzi kuendelea.

CHANZO: Mwananchi
 
kwa mujibu wa ufuo Saro nyumba ni za mbunge viti maalumu Mama Rwakatare ila kaandika majina ya mtoto wake.
 
Mbona hatukuelewi,andika vizuri basi
 
ikiwa hivyo basi haki imetendeka....
 
Hongera sana serikali yangu. Mkosaji ni mkosaji tu. haijalishi hadhi yake
 
Nyumba nne eneo la mbezi beach ikiwamo no. 314 zilizopo ufukweni mwa bahari ya hindi zimebomolewa leo na serikali

Kwa mujibu wa Eng.wa manispaa ya kinondoni kila nyumba ina thamani ya million 30.siku nyingine uwe mchunguzi ili kuitetea serikali.Serikali hii hii inadai kupitia NHC inajenga nyumba za bei nafuu na kupitia habari iliyowekwa hapa JF nyumba ya bei ya chini Ni million 40.huo ufahari unautoa wapi mkuu
 
Hatimaye.......maana hili sakata nililisikia muda mrefu sana mama akawa anatumia njia anazojua yeye kuzima hii issue, hongera Tibaijuka hongera Mdee maana najua lazima kuna nguvu zako mpaka hilo zoezi limefanikiwa.
 
Hapa ndipo ninapoipendea serikali yetu, haijali cheo, hadhi wa fedha za mtu linapokuja suala la kufuata sheria!
 
Nyumba nne eneo la mbezi beach ikiwamo no. 314 zilizopo ufukweni mwa bahari ya hindi zimebomolewa leo na serikali
.....mbona umemumunya maneno????..ungesema tu ni nyumba zinazohusishwa na lile limama Lwakatare.....ambaye tayari anahusishwa na dhuluma na ufisadi....pasipokusahau biashara haramu ya watoto....Alafu anajiita mchungaji......Unafiki wa wanasiasa wetu huu..
 
Back
Top Bottom