Mch Richard Hananji wa KKKT Usharika wa Kigogo Dar es salaam mfano wa kuigwa kusaidia kundi maalumu

tramadol

JF-Expert Member
Oct 10, 2015
5,383
4,323
Mchungaji huyu wa KKKT Usharika wa Kigogo amekuwa msaada kubwa sana waathirika wa madawa ya kulevya kwa kuwapa msaada wa mahitaji ya mwili na ya kuroho.

Waathirika wengi wa madawa wengi huwaita 'mateja' wanamshukuru sana Mch Richard na kuwa kimbilio lao kila kukicha.

Wengi wao wameacha kutumia madawa ya kulevya na kujishughulisha na kazi za jamii na kurudi ktk familia zao.

Wakijitokeza wengine kama Mch Richard tutaweza kusaidia kundi hili ambayo wengi wao wanasumbuliwa na matatizo mengi kama malazi,ajira,chakula,maradhi kama TB,HIV na Hata mavazi.
 
Kazi ya Kanisa ni kutibu Roho na mwili. Asante Mtumishi wa Bwana kwa kuonyesha Imani kwa vitendo " kuwatafuta walipotea" .
 
Back
Top Bottom